Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Umenena vyema mkuu.
 
hata mimi sijawahi kuona hata kufika kwenye ufunguzi ikiwa kuna mwakilishi sehemu husika
labda ndio utaratibu mpya
 
Kwani nimetaka ' ufafanuzi ' wa Kimantiki au ' mabishano ' nawe? Hopeless!
Wewe ndio hopeless...unataka watu wakujibu kupinganq na unavyowaza wewe!!

Unataka watu wakuunge mkono tu wakati umetaka watu waje wajadili, sasa unamwonaje mwenzio hopeless.

Shida sana aisee!!!!
 
GENTAMYCINE ni popoma tu unajidai mjuaji kila kitu. Mbona kila Mara tumesikia na kuona madirector was usalama Marekani na kwingineko wakitajwa?
 
Mwacheni Magufuli afanye kazi, kila siku yeye tu.
Hivi huwa hamna kazi ninyi, ndiyo maana tumechelewa kimaendeleo kama taifa.
Na wewe mwenye kazi unatafuta nini huku? Au na wewe huna kazi? au kazi yako ni kukusanya habari za mitandaoni?😀😀
 
Bila shaka ni hoja ya kipopoma,you're right.
 
Anateuliwa na kutangazwa hadharani, anaapishwa kweupe ikulu mbele ya paparazi, kafanyakazi sehemu mbalimbali n.k. huko kote ni kutajwatajwa hadharani.

Wewe hapa tayari umetaja kuwa mko wengi humujF. Kjazuia maamuma wa mambo ya intelegensia wasichangie. Wakati mambo kwa maana ya kuyafamu ya itelegensia yako kibao mitandaoni na shule yake iko ukitaka ni kuita na kuisoma. Kisicho fahamika ni opetesheniz zao wanazofanya maana ni siri kama hazijavuja/ kuvuishwa. Watu wa Tiss mliomo humu jf endeleeni kuchangia kama mwenzenu alivyo waomba. Hii haina tofauti na ile unajua mimi nani!!! Kumbe ndio hulka imeshaota mizizi hivi.?

Labda tiss ianzishe utaratibu wa black DG ambaye ndiye atakaye kuwa akimtuma huyu hadharani DG.
 
Huwa napenda na nafurahi sana kukutana na ' Majiniazi ' wachache wa mfano wako hapa Jamvini JamiiForums. Nimekukubali mno.
Ndiyo maana uteuzi wa CDF Ulileta kwaro kwa cheo chake hakutakiwa kuwa CDF wakati mbele yake kulikuwa na Ma Lieutenant General zilikiukwa taratibu.
 
Sidhani anamaanisha hivyo mbona wengine anatambua uwepo wao. Je ingeeleweka vipi anamtambua uwepo mkuu wa polisi asitambue uwepo wake? Hiyo ni itifaki tu
Kwa nini kila kwenye mikutano yake awatambue uwepo wake, kwani hizo hafla zinakuwa zinahusu mambo ya ulinzi?
 
Embu tuwekee picha yake maana hatumjui sie wengine
 
Ndiyo maana uteuzi wa CDF Ulileta kwaro kwa cheo chake hakutakiwa kuwa CDF wakati mbele yake kulikuwa na Ma Lieutenant General zilikiukwa taratibu.

Tunamzungumzia Rais Dkt. Magufuli na Mkurugenzi wa Idara / Taasisi ya Usalama wa Taifa na sijui hilo la Mkuu wa Majeshi Tanzania ( CDF ) hapa limekuwa ' logically connected ' vipi Mkuu.
 
Na kweli wewe popoma, kama Rais mwenyewe anajulikana, sembuse dg tiss?! Nadhani ukikua utaelewa mambo ya aina hii, ma-dg wote wa tiss tangu enzi za mwalimu watu wanawajua mpaka wanakolala!! hebu kula erythromycine kidogo utulize kipindupindu.
 
Ni punguani tu anaweza tetea mambo ya siri siri, dunia ya leo kuna siri??? kwanza hii kasumba ya TISS kuoperate kisi siri wakati wanatumia pesa za walipa kodi ilipaswa ibadilishwe, bajeti yao ni siri, kazi zao ni siri, taratibu za uajiri ni siri..ndio maana mambo mengi sana nchi imefeli..leo tuna mgogoro na ACACIA wakati mambo hayo ya mchanga kusafirishwa na wao walikuwepo, kwa sababu ya usiri siri huo wengi wa wanaoajiriwa ni aidha ndugu wa waliomo TISS au wanafahamiana vyovyote vile..sasa na huyu analeta kukosoa mtu kutambulishwa tu..sasa km yeye hapendi kutambulishwa nini kinamfanya akae high table????
 
Binafsi sioni shida wala kosa, kosa liko kuwataja maafisa [Watumishi] waliochini ambao ndio wahusika wa majukumu ya kazi. Tena tulipofika tumechelewa sana huyu DG wao, manake inapaswa kuwa Taasisi na si Idara. Ili awe na maamuzi rasmi akilipoti kwa Rais na kuwa na wajibu wa kisheria kutenda mamboi kwa maslahi ya Taifa. Mataifa makubwa Mabosi wa Taasisi hizo ufahamika na wala haina shida. Tatizo ni pale mtu atakapotaja watendaji wa chini ambao ndio engine ya taasisi husika hapo kutakuwa na kosa la kiweledi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…