Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda,
Kwa heshima na taadhima, tunapenda kutoa maoni yetu kuhusu mwelekeo wa elimu ya juu nchini, hususan uamuzi na ufafanuniz wako kwenye hotuba ya jana wa kusimamisha baadhi ya kozi katika vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Tunaamini kuwa hatua hizi, ingawa huenda zinalenga kuboresha, zina madhara makubwa kwa mustakabali wa taaluma, tafiti, na ushindani wa kimataifa wa wahitimu wetu.
Mheshimiwa Waziri, elimu ya juu si mradi wa ndani wa ajira pekee, bali ni elimu ya kimataifa (universal education), inayolenga kuandaa wataalamu wenye uwezo wa kushindana kimataifa katika taaluma, utafiti, ubunifu, na maendeleo ya kijamii.
Maamuzi yanayohusu mabadiliko ya mitaala yanapaswa kutegemea tafiti za kina, muktadha wa kijamii na kisayansi, pamoja na mwelekeo wa kidunia—siyo misukumo ya kisiasa au matarajio ya muda mfupi.
Kuingilia uhuru wa vyuo vikuu katika kutunga na kuendesha mitaala yao ni kuvunja misingi ya taaluma na uhuru wa utafiti.
Vyuo vikuu vina wataalamu waliobobea, ambao ndio wenye dhamana na uwezo wa kuchambua mahitaji ya jamii na kuyatafsiri katika mitaala yenye tija.
Aidha, historia inaonyesha kuwa makosa ya kielimu tayari yalishafanyika. Tulishuhudia kufutwa kwa masomo ya msingi kama Ufundi, Kilimo, na Biashara—na leo tuna uhaba mkubwa wa wataalamu katika sekta hizo. Hali hiyo sasa inajirudia kupitia mabadiliko ya ghafla kama kuchanganya au kufuta masomo ya sayansi kama Fizikia na Kemia, hatua iliyosababisha mkanganyiko mkubwa kitaaluma.
Pia, kauli yako kwamba walimu wanaopaswa kufundisha masomo mawili hawapo imeibua maswali. Je, waliobobea katika maeneo hayo tayari wameajiriwa? Ikiwa bado hawajatumika, kwa nini tusitumie kwanza rasilimali tulizonazo kabla ya kufuta kozi zinazozalisha wataalamu hao?
Tunashauri kwa dhati kwamba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ibaki kuwa chombo cha ushauri wa kitaalamu, badala ya kuwa mamlaka ya kutoa maagizo ya moja kwa moja kuhusu uendeshaji wa mitaala. Vyuo vikuu vipewe uhuru wa kuendesha taaluma zao kwa misingi ya academic freedom na ubunifu wa kielimu.
Mheshimiwa Waziri, ondoa siasa kwenye elimu. Simamia uhuru wa vyuo vikuu, linda heshima ya taaluma. Huo ndio urithi wa kweli utakaosimama na jina lako katika historia.