Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Uaminifu na unyenyekevu ndio shida kubwa,lakini ukiwa na hizo sifa kuu mtaji unaweza kupatikana.
 
Hujui kuwa kuna pombe mpaka za 500 tsh. Hata kama akinywa chupa 20 maana yake anakuwa ametumia elfu 10.


Hivi kwa nchi hii unaweza anza biashara kwa shilingi 10,000. Acheni dharau za kutokuwa na shuruba ya maisha
Jaribu kuwa muelewa... tatizo sio bei ya pombe nimejiuliza tu kwa nini mtu uwe mlevi kisa huna kazi? Unawezaje kupata hata hiyo kazi wakati unajiharibu kwa ulevi? Kwa hiyo wewe unaona ilikuwa sawa anywe pombe sababu hana kazi na sababu pombe ni shilingi 500?
 
So kwako mwalimu kashasha.. Unaushauri gani kwa jiwe kuhusu madaraka aliyonayo na anavyo iongoza nchi...

Halafu hii comments yako pro ccm wameiona kweli !?
 
Achana na yule mzee alisha ji - jitambulisha kuwa ni kichaa Au hamkumuelewa
Na bado Mheshimiwa Rais anatwambia watanzania tutembee vifua mbele kwa kuwa we are in the right track!

Hii damu isiyo na hatia inayomwagika itaendelea kumlilia Jiwe kizazi na kizazi!
 
Hahaha.. Nimecheka sana.. Acha atumie alichonacho kujitapatia pesa asije kujiua bure kwa sababu ya stress za kukosa pesa halafu mkaja kumnanga kama hivi mnavyo mnanga huyu marehemu hapa
Tena wasomi ndo hatari balaa nimemmendea mmoja ana nipiga danadana,mwisho ananiambia tatizo hueleweki una dau gani. Nikachoka
 
Binafsi sijawahi kumlaumu mtu aliyeamua kujiua kwa sababu kifo ni wajibu kwa mwanadamu na viumbe vingine.. Hata kama usipojiua nafasi ya kupitia hatua ya kifo iko pale pale.. Kifo ni kifo tu haijalishi utakufa kwa namna ipi.. Ni kama ambavyo ilivyo safar. Safar ni safari tu iwe kwa miguu.. Gari au bicycle
 
Ila huyu mwanasayansi mungu atamchomaaaaaaa
Maana alimpa kipaji
Yee anaenda kinywea na kujinyongea
Kuna watu wamesoma kiswahili tu au historia na wanalisha ukoo mzima
 
Hivi mtu anasoma aelimike au ili aajiriwe?hata nchi zilizoendelea zina tatizo la ajira.Kwanini asingejiingiza kwenye kilimo kule ajira ni zakumwaga.Ninahisi atakuwa na tatizo la akili.Pia kuna wasomi vichaa.Hata hivyo RIP
 
Kama week kadhaa nilisoma thread ya Mwana JF mwenzetu kuwa alikua anatafuta kazi halali na kwamba Alisoma mambo ya Computer Science! Dogo aliandika akiwa so desperate Sana, Leo nimesoma hii taarifa kuwa kuna Mhitimu kajiua kwa kukosa kazi, je ni yeye?

*Yametokea huko mwanza, mtu kaamua kujiua sababu amekosa kazi japo ana elimu ya chuo kikuu*
mwananchi.co.tz

Mwanza. Musa Ally (25), mkazi wa Kiloleli wilayani Ilemela jijini hapa anayedai wa kuwa na elimu ya chuo kikuu, amejirusha katika jengo la la Rocky City Mall na kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa Musa alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo, kukosa kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Desemba 21, 2018 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea leo saa saba mchana.

Bulimba amesema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16, 2018 na alikamatwa na kuwekwa kituo cha polisi Kirumba, kilevi kilipopungua aliachiwa.

Amesema katika uchunguzi wa awali marehemu alibainisha kuwa alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa kazi licha ya kuwa na elimu ya juu.

Bulimba amesema baada ya polisi kumuachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu na kukutwa na pombe kali na ugoro.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kijana huyo amesema amejiingiza kwenye ulevi na asilaumiwe mtu yeyote. Amesema amechukua uamuzi huo yeye binafsi, pia akidai yeye ni masikini hana baba wala mama,” amesema Bulimba.

Amesema mwili umehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi licha ya kutotaja jina la hospitali hiyo.

Bulimba amesema, maandishi aliyokutwa nayo marehemu yalisomeka kwamba “yeye ana shahada sayansi ya kompyuta aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…