Mhitimu wa UDOM adai Bodi ya Mikopo inamlipisha deni la chuo ambacho hajawahi kusoma

Ndio uzalendo we lipa tu
 
Usikate tamaa , fatilia jambo lako hadi kieleweke
 
Pole sana, ndio maana sitaki Wanangu waje wasomeshwe kwa Mikopo ya Bodi ya Mikopo, Mungu anisaidie katika hilo litimie.
 
bodi ya mikopo kuna wajinga wamejificha kwenye kivuli cha suti za mtumba na tai wanakula hela tu za walalahoi.
 
Nenda mahakamani
 
Yaani huko kwenye mikopo kuna shida kweli. Hata vyuo vingine hawawapi wanafunzi ile hela yote ya boom wanawafyeka halafu wakati wa kulipa analipa hata ambacho hakutumia yeye
 
Hapa kuna mambo mawili
1. Hela kweli imelipwa chuoni na mchezo umefanyika kati ya afisa mikopo MUCE na muhasibu waliendelea kutumia jina lako kwa miaka 3.

2. Afisa wa hapo HESLB ameifanyia makaratee amejengea nyumba kisha kimyaa kanyuti.
Kama walivyokushauri nenda kwanza MUCE kawawakie akili iwakae sawa utamjua tu mwizi wako
 
Sio kweli,unachelewesha tu usingizi,utafikiwa vizuri
 
Kafungue kesi Mahakamani uwashtaki
 

Sasa bro ataendaje MUCE na hajawahi kukanyaga, hivi kweli uende MUCE eti mkopo wangu ulikua unakuja hapa watakuuliza uliwahi soma hapana

Awabane hao hao bodi
 
Wanasheria tupo hamtutumii.

Njoo PM haraka utoe instructions kazi ianze mara moja [emoji28].

Naiona fidia ya mamilioni iko pale inakusubiri kijana [emoji1].
 
Kuna mwanangu naye aliapply kusoma Bachelor,bahati mbaya /nzuri akapata nafasi ya diploma anayopenda akaachana na degree akajisomesha diploma,

Kaja kupata kazi akashangaa anakatwa deni la bodi as if alikopeshwa
 
Bodi ya mkopo ni Wahuni na Wezi utashangaa umeshamaliza deni lao ila bado wanakukata utadhani hawana taarifa

Wahudumu wana nyodo,dharau hii bodi imulikwe na waache kuibia Watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…