Mhitimu wa UDOM adai Bodi ya Mikopo inamlipisha deni la chuo ambacho hajawahi kusoma

Mhitimu wa UDOM adai Bodi ya Mikopo inamlipisha deni la chuo ambacho hajawahi kusoma

Hapo huyo mwanafunzi hatakiwi kukatwa hilo deni la Mkwawa.. Hapo kesi ni kati ya HESLB na Mkwawa na hao maofisa wa HESLB wanaomjibu kwa ukali wana lao jambo. Kiutaratibu huyo mwanafunzi anatakiwa aombe statement zake zote mbili kisha aandike malalamiko yake kwa barua kwenda kwa mkurugenzi Mkuu wa HESLB. Watakachofanya HESLB watawatuma wakaguzi wa ndani waangalie kama hizo pesa zilitumwa Mkwawa au hazikutumwa Mkwawa. Iwapo zilitumwa Mkwawa basi chuo ndio kitawajibishwa kulipa hizo pesa iwapo hawakuzirudisha HESLB kama inavyotakiwa iwapo mwanafunzi hajaripoti chuoni na kama hazikutumwa kabisa huko basi HESLB watamalizana wenyewe kwa wenyewe huko ndani.

Huyo jamaa akifuata huo utaratibu hapo juu yaani wiki moja/mbili hii ishu itakuwa ime kwisha kabisa na wahuni waliolamba hiyo pesa watajulikana. Yeye aache kudili na hao maofisa wa chini hapo HESLB wanazingua sana. Yeye aandike barua kwa mkurugenzi mkuu halafu aipeleke kwa dispatch nina hakika baada ya wiki mbili ataleta mejesho hapa kuwa suala lake limekwisha.
 
Back
Top Bottom