jastertz
JF-Expert Member
- Jul 4, 2020
- 407
- 768
Ulianza kama ufichuzi ambao ungeyeyuka baada ya muda mfupi wa mihemko na lalama.
Lakini kilichoanzia kati kati ya msitu eneo la Malindi Pwani ya Kenya wiki moja iliyopita sasa kinageuka kuwa donda ambalo kumbukumbu zake hazitafifia hivi karibuni.
Kufukuliwa kwa makaburi ya kina kifupi ambayo yametoa miili ya makumi ya watu na kufikisha hadi takriban watu 70 ambao walikufa kwa kuamrishwa kufunga ili kukutana na Yesu.
Mengi kumhusu yanaendelea kujitokeza pindi siku zinavyosonga mbele lakini kuna ya msingi hadi sasa tunayofahamu kumhusu mhubiri huyu tata.
Paul Makenzi alianza maisha katika mji wa Malindi kama dereva wa teksi.
Wengi waliomfahamu wakati huo hawakuweza kutabiri kitakachotokea miaka mingi baadaye ambapo simulizi zao ni kama za filamu inayotumbukia kuwa ya kutisha.
Mwaka wa 2003 wakati kanisa lake lilipoanza kuwavutia wengi , anadaiwa kubadilisha mafunzo na akaanza kuwataka waumini kuchoma vyeti vyao vya utambulisho na hata vya elimu.
Pia wengi waliowahi kuhudhuria kanisa lake wanasema alianza kuhubiri chuki dhidi ya dini nyingine na hapo aliwapoteza baadhi ya waumini wake ambao waliondoka. Hata hivyo wengi waliwaacha jamaa zao-mume aliondoka na kuwaacha mkewe na watoto katika kanisa hilo.
Wengine waliwatoroka jamaa zao na kujiunga na kanisa hilo kisiri wakisakwa kwa miaka bila kujulikana waliko hadi ufichuzi huu ulivyolipuka.
Katika kanisa lake ,watoto hawakuruhusiwa kwenda shule wala kutibiwa hospitalini.
STORY NI NDEFU.
Maswali mengi kuliko majibu, unahisi tatizo ni nini hasa kwenye haya masuala ya kidini na nini kifanyike?