Mhubiri Paul MacKenzie alianzaje safari tata ya kuwashawishi watu kufunga hadi kufa?

Mhubiri Paul MacKenzie alianzaje safari tata ya kuwashawishi watu kufunga hadi kufa?

Ulianza kama ufichuzi ambao ungeyeyuka baada ya muda mfupi wa mihemko na lalama.

Lakini kilichoanzia kati kati ya msitu eneo la Malindi Pwani ya Kenya wiki moja iliyopita sasa kinageuka kuwa donda ambalo kumbukumbu zake hazitafifia hivi karibuni.

Kufukuliwa kwa makaburi ya kina kifupi ambayo yametoa miili ya makumi ya watu na kufikisha hadi takriban watu 70 ambao walikufa kwa kuamrishwa kufunga ili kukutana na Yesu.

Mengi kumhusu yanaendelea kujitokeza pindi siku zinavyosonga mbele lakini kuna ya msingi hadi sasa tunayofahamu kumhusu mhubiri huyu tata.

Paul Makenzi alianza maisha katika mji wa Malindi kama dereva wa teksi.
Wengi waliomfahamu wakati huo hawakuweza kutabiri kitakachotokea miaka mingi baadaye ambapo simulizi zao ni kama za filamu inayotumbukia kuwa ya kutisha.

Mwaka wa 2003 wakati kanisa lake lilipoanza kuwavutia wengi , anadaiwa kubadilisha mafunzo na akaanza kuwataka waumini kuchoma vyeti vyao vya utambulisho na hata vya elimu.

Pia wengi waliowahi kuhudhuria kanisa lake wanasema alianza kuhubiri chuki dhidi ya dini nyingine na hapo aliwapoteza baadhi ya waumini wake ambao waliondoka. Hata hivyo wengi waliwaacha jamaa zao-mume aliondoka na kuwaacha mkewe na watoto katika kanisa hilo.

Wengine waliwatoroka jamaa zao na kujiunga na kanisa hilo kisiri wakisakwa kwa miaka bila kujulikana waliko hadi ufichuzi huu ulivyolipuka.

Katika kanisa lake ,watoto hawakuruhusiwa kwenda shule wala kutibiwa hospitalini.

STORY NI NDEFU.

Maswali mengi kuliko majibu, unahisi tatizo ni nini hasa kwenye haya masuala ya kidini na nini kifanyike?
hii inaitwa"BRAIN WASH"...manake ubongo wako unapigwa deki na kubaki kama kifuu cha nazi kilichochokolea{kuliwa nyama yake},,,,,then hawa jamaa kina makenzie na wenzake kina kibwetere wajanza vichwa vyao manyokanyoka mpaka wanakua kama mataahira,,,,,sasa hawa kina makenzie wakishona sasa wameshaiva ndo wanawafanya kama walivowafanya!!!!................................ndo manake sometimes mara mojamoja unakula ganja kidgo walau mara mbili kwa wiki\111"HAIWEZEKANI HATA SIKU MOJA RASTAMAN AKAFANYIWA UJINGA KAMA HUU....narudia tena,haiwezekani ukamdanganya SNOOP DOGDOG akachezewa namna hiii!!!!!!!
 
Namshukuru Allah kwa neema ya uislamu niliyo nayo.
Uislamu nako kuna maneno angalia Somalia, Afghanistan,Sudan kaskazini,Yemen nk waislamu watupu kule wanatwangana na kuuana kwa maelfu wenyewe kwa wenyewe

Kwa tofauti tu za tafsiri ya kurani

Na wanaouawa kwenye vita za waislamu kwa waislamu ni wengi kuliko wanaokufa kwa imani potofu za Kikristo
 
Mind you.

Ukisoma kwa utulivu huku ukishirikisha ubongo wako vizuri utagundua hata wale wanaofanyiwa brain wash kwamba ukimuuwa mtu wa tofauti na dini yao wanaenda moja kwa moja peponi kufaidi neema za Allah hawana tofauti na hawa.

Tofauti ni hawa wamedanganywa wamejiuwa wao wakati wale wanadanganywa (au sijui kama ni kweli) kwenda kuuwa wengine.
Wale wanaojiita waislamu,hawafanyi kwa imani ya dini,wqnafanya kwa malipo,familia zao hulipwa pesa nyingi tu.Na pia wanaowalipa hawafanyi kwa ajili ýa imani,wanafanya kwa siasa,ili wapate madaraka.
 
Uislamu nako kuna maneno angalia Somalia, Afghanistan,Sudan kaskazini,Yemen nk waislamu watupu kule wanatwangana na kuuana kwa maelfu wenyewe kwa wenyewe

Kwa tofauti tu za tafsiri ya kurani

Na wanaouawa kwenye vita za waislamu kwa waislamu ni wengi kuliko wanaokufa kwa imani potofu za Kikristo
Hawa wanauwana kisiasa ,sio kiimani ya dini.Wanagombea madaraka.Wanatumia mwavuli wa dini,ili waungwe mkono.
 
Unadhani wale mbuzi wa kawe wakiambiwa hawatakubali?
 
Hawa wanauwana kisiasa ,sio kiimani ya dini.Wanagombea madaraka.Wanatumia mwavuli wa dini,ili waungwe mkono.
Sio kisiasa Somalia makundi yanayopigana yana tofauti za kidini
Sudan Kaskazini pia

Waasi wa Sudan kaskazini ni Answar Sunna waliokuwa zamani wakiitwa Janjaweed wafuasi wa Answar Sunna

Raisi wa Sudan kaskazini aliyepo sio Muislamu Answar Sunna
 
Namshukuru Allah kwa neema ya uislamu niliyo nayo.
Allah anayeaminisha kuuwa mtu asiye wa dini yako unapata Mabikra 72,nyie watu wa dini acheni kujihesabia haki.

Mna matendo mabaya kuwaliko wasio na dini
 
Huyo jamaa ni mgonjwa wa akili na muuaji.
 
Ukwel ni kwamba uyu mwamba anatumia nguvu isiyo ya kawaida kushawishi watu kuamini kila asemalo,

kuna jamaa namfahamu kabisa yaan ni msomi mkubwa sana lakin amewezwa na uyu mpuuzi nayeye ni miongoni mwa waliofunga adi kufa. kwa elimu aliyokuwa nayo yule marehemu sifikirii kama alishawishiwa kikawaida. kuna kanguvu ka giza tena kazito kanatumika
 
Wale wanaojiita waislamu,hawafanyi kwa imani ya dini,wqnafanya kwa malipo,familia zao hulipwa pesa nyingi tu.Na pia wanaowalipa hawafanyi kwa ajili ýa imani,wanafanya kwa siasa,ili wapate madaraka.
kabla ya kujibu ingebid kufuatilia ilo kiundani
 
Wale wanaojiita waislamu,hawafanyi kwa imani ya dini,wqnafanya kwa malipo,familia zao hulipwa pesa nyingi tu.Na pia wanaowalipa hawafanyi kwa ajili ýa imani,wanafanya kwa siasa,ili wapate madaraka.
Vipi nikisema hata hao wanaofanya hivyo ktk Ukristo wanakuwa na malengo yao hawafanyi yale Wakristo wanatakiwa kufanya?

Kununua baraka,mchungaji kubagua wanaotoa sadaka kubwa na ndogo etc?nasisitiza hao wako brain washed na kote hizi hufanyika no matter ni waumini au siyo waumini.
 
Back
Top Bottom