Miaka 10 ya Kashfa ya Richmond bila ya Lowassa kufikishwa mahakamani!

List of shame ya Chagadema ilikuwa uzushi na upuuzi mtupu.
 
GREGO hilo bandiko halileti mantiki yoyote ile katika zama hizi ambapo Lowassa ndiye anayeitwa na wana CCM "arudi nyumbani"
 
Angepewa fursa ya kujitetea hadithi ingekuwa tofauti kwa namna wapinzani walivyokuwa wamemkamia? Je, Kamati ile ilifanya kazi kwa muhemko, hila au ilikuwa na lengo la kuwaziba midomo wapinzani na kukijenga chama cha CCM?
Nadhani ni muda mwafaka kwake kuweka kumbukumbu sawa kwa kuwatumia washirika wake kwa sasa ambao walimdhihaki na kumwita majina mbalimbali mabaya kwa kuwataka wawaombe wananchi na wanachama wao radhi kwa kilichotokea huko nyuma. Kwamba, kwa kuwa siasa sio uadui na kwamba siasa ni kupanda juu ya mabega ya mpinzani wako, basi ieleweke kuwa zile zilikuwa ni mbinu za kisiasa tu na hapakuwa na ukweli wowote japo kufanya hivyo kunaweza kukawaondolea imani ndogo iliyobaki kwa wananchi na wanachama wao baada ya kumpokea huyo waliyemdhihaki!
 
Yaliyopita si ndwele!
 
Uchaguzi ukiwa baadae ninampigia kura yangu huyu jamaa.
Alafu ubishi na mtu staki.
 
upuuzi huu

EL ni mwizi, ccm nao wengi ni wezi!..hawawezi kupelekana mahakamani

kutopelekwa mahakamani, hakuondoi huo ukweli
 
upuuzi huu

EL ni mwizi, ccm nao wengi ni wezi!..hawawezi kupelekana mahakamani

kutopelekwa mahakamani, hakuondoi huo ukweli
Ukweli gani?

Umesoma hotuba yake aliyoitoa wakati anajiuzulu? Wewe huo wizi wake unaupima kwa kutumia kigezo gani?
 
Hapo ndipo mzee alianza kutengenezwa kwenda kuivunja upinzani
 
Slaa aliwahi kusema huyu jamaa hasafishiki mkadharau, leo mwaka wa tatu mnaendelea kusafisha tu.
 
Slaa aliwahi kusema huyu jamaa hasafishiki mkadharau, leo mwaka wa tatu mnaendelea kusafisha tu.
Sasa hapo anasafishwa kwa uchafu upi alio nao? Wengine mwaka wa tatu sasa tunauliza jinsi Lowassa alivyohusishwa na suala la Richmond hatujibiwi.

Halafu Slaa kusema kwamba Lowassa hasafishiki ni kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa anatengeneza huo uchafu akidhani kuwa utadumu milele. Siku ile pale kwenye hoteli ya Royal Palm hata baada ya kuongezewa "ushahidi" na kina mwakyembe, bado alimbwelambwela tu kueleza ni kivipi Lowassa alihusika kwenye sakata la Richmond.
 
Ukweli gani?

Umesoma hotuba yake aliyoitoa wakati anajiuzulu? Wewe huo wizi wake unaupima kwa kutumia kigezo gani?

mkuu alijiuzulu, kanywe nae chai....tushaongea humu miaka 10 sasa

unataka justice? haipo kwenye siasa

yeye EL anajua maovu yake, na hawezi akajitetea!!.mnamtetea nyie wengine!!!!!!

kwa nini alizira? kuachia u PM kwa tuhuma tu....??? seriously???? una akili wewe...??? unajua uwaziri mkuu ni nini?? simple like that unatuhumiw haujashiriki unajiuzulu??

EL ni mwizi na alitesa wengi tu, anajua sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…