Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

historia kama yangu,nilikunywa pombe mno miaka yangu miwili ya mwanzo kidogo kazi inishinde, nashukuru nimerudi kwenye reli
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yaani mkuu story yako na mimi naona inapishana viwango vya pesa tu.mpaka nimecheka.

ila nikushukuru mkuu,umenitibu moyo wangu na kunifanya nione taa ya kijani mbele yangu tena,maana nimejua kumbe si mimi pekee nilitereza.

hapa niko na mikakati mikali ambayo imeanza kuload kama 15% hivi,nina mipango mpaka 40,niwe kwenye tathmini ya kuendelea na kazi au kuacha nayo.
 
mkuu sijakuelewa, hebu fafanua zaidi
Iko hivi kaka kampuni kama za qnet na nyingine nyingi zinazofanana na hizo zinawalaghai sana watumishi wa umma na kuwafanya wakope mikopo mikubwa ili wawekeze huko na kuhimwambafai kwamba wataacha kazi na utumishi wao kwamba very soon watakuwa mabilionea. Mwisho wa siku wapo kitaaa wanahaha
 
Mkuu Utumishi wa Umma (Serikalini) kwa level ya FTC/Diploma mwaka 2009 scale yake iwe ni 840k as take home? Na marupurupu na posho zote hizo nina masha na haya maelezo yako.
 
Naona wengi hapa hatujaelewana, watu wanadhani mpaka leo bado nakula msoto nadhani hawajaelewa andiko langu.

Hizo starehe nilifanya mwaka 2009 - 2012 na ndio kipindi nilipochukua hiyo mikopo yote iliyonitesa mpaka 2015 na hapo nikaanza maisha mapya kabisa ambayo nime - win lakini sio kwa hali ambayo nafikiria ningekuwa nayo Kama ningetulia tangu mwanzo
 
Mkuu Utumishi wa Umma (Serikalini) kwa level ya FTC/Diploma mwaka 2009 scale yake iwe ni 840k as take home? Na marupurupu na posho zote hizo nina masha na haya maelezo yako.
Sipo hapa kukulazimisha uamini mkuu unaweza kupuuzia pia.
Lakini nikusahihishe tu hakuna sehemu niliyoandika hiyo ni take home
 
Hahaha mipango mikali, haya mambo haya ww acha tu unaweza ukawa chizi
 
Mwenzako mi mpaka leo najuta kwanini sikuenda kusoma Diploma vyuo vya ufundi nikaenda Form 5. Mkuu, hili ntajilaumu maisha yangu yote.

Anyway, maji yameshamwagika. Fresh tu.
Kwa nini ujilaumu boss?
 
Usiwakule wapangaji wako
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ mkuu mimi nilishtuka 2015 kama ningeshtuka mapema ningekuwa mbali sana

Ile miaka 4 (2009 - 2012) Roughly nilitumia zaidi ya 100+m kwa upuuzi tu ambazo ningewekeza leo ningekuwa mbali
Yani sijui atatokea rais mwingine tupige hela kama enzi za jk mimi kwa upande wangu nilikua nasafiri na ndege tu hadi nikawa nashangaa watu wanawezaje kusafiri na basi unachoka sana ha ha ha ha saizi nimeludi kule kuleee japo nna private car ila ni muoga ku drive njia kubwa
 
Kabisa mkuu haya mambo haya
 
We kama mm tu
Hasa hapo kwenye mke ndo kabisaaaaa
 
Good & Big up mkuu!!

Kuwa na amani na utulivu kwa maisha ambayo uliyoyapitia, utapata utulivu zaidi wa maisha yako ya sasa na ya baadae.

Yaliyopita kamwe huwezi kuyabadilisha japo yanauma sana, kimsingi unatakiwa kubeba funzo tu ya yale uliyoyapitia kuliko kubeba matukio halisi ya yaliyopita.

Tunajifunza kwa makosa tuliyopitia na ndio tunapoinuka juu kila muda baada ya kufanya makosa na kujifunza kupitia makosa.

Enjoy maisha yako ya sasa na ufurahie haswa kila unalolifanya muda huu bila kuumizwa na historia yako. kuwaza matukio yaliyopita sio tu yatakuumiza moyo wako bali yanakupotezea muda (kwanini uwazie mambo ambayo yaliyopita wakati una muda wa kutosha kuinjoy maisha yako ya sasa).

Usijifananishe na wenzio kwani kila mtu anapitia njia yake tofauti ya mafanikio na pia riziki aliyokupangia Mungu ndo utakayoipata na waliyopangiwa wenzako nao wamepewa fungu lao kutoka kwa Mungu. Ishi maisha yako na familia yako kwa fungu alilokupa Mungu na usiumie kwa mafungu waliyopewa wenzako.

Your strory is inspiring!!, Thank you
 
Mkuu ubarikiwe sana kwa hii comment yako
 
Leo hii nilikua nawaza hadi kichwa kinauma..mimi najutia boom la chuo nililitumia vibaya Kuna sehemu niliambiwa ninunue kiwanja Cha laki 3 tu..nikapuuza..kwa Sasa Hilo eneo linauzwa m 10..kila nikiwaza ujinga huu naumia sana.
Nilipopata kazi yangu..nilikuwa nakaa kwa ndugu kwa mwaka mzima lakini sikutunza hata Mia..(ujinga mwingine nalifanya)

Lakini story yako imefutia hatia kumbe kunawaliofanya makosa kuliko Mimi .
Tujirekebishe tusonge mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…