Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Haijawahi tokea na haitaokea😅. Huwa najiuliza inakuaje wanaume wanahonga? Huwa sielewi ni mechanism gani wanayo. Salute kwenu
🤔😳 Nikichukua siti kwako, na kazi ikawa kazi kwelikweli siwezi kuhongwa?🤸😄🏃
 
Upele humuota asikuwa na kucha. Nalipwa 716k per month, take home 454k yaan nije nilipwe 1.2M kwa mwezi na hiyo 48M mkopo wa masharti nafuu kama hayo uliopewa nadhani ningekuwa mbali sana. Nafanya mambo yalio muhimu. Napanga bajeti yangu ambayo itakuwa chini ya mstari wangu wa matumizi. Nafanya biashara ambayo inamtaji wa wateja na inaleta faida nzuri kulingana na nilichowekeza.

Pole sana. Umri wako bado. Anza upya sahihisha makosa yako. Umewapa vijana somo zuri sana.
Bila shaka mwalimu degree holder.
 
Pole sana ndugu yangu, mimi nimeajiriwa na shirika la serikali yawezekana huelewi kuhusu utofauti wa maslahi kwenye taasisi za umma, ngoja nikupe mifano hai ya ndugu zangu wa karibu kabisa wanne ambao wameajiriwa hivi karibuni baada ya kutoka kapa huko JKT kupitia pale utumishi na wote wako cheo kimoja na elimu yao ni kidato cha nne tu, wameajiriwa taasisi tofauti, tuwape majina A,B,C na D.

"A" alitangulia kuajiriwa TPA mwaka jana japo usaili walifanya wote na akafanikiwa yeye tu kupata ajira hapo miongoni mwao wote kama "Security Guard", amefika kule akakuta mshahara 800+k ukiongeza na overtime ambao wao inachanganywa kwenye mshahara pamoja at the end mshahara unasoma 1.3+m na wana posho 150k kila mwisho wa mwezi,alipelekwa mtwara kituo chake cha kazi na alipewa pesa ya kujikimu zaidi ya 3m.

"B" aliajiriwa Mahakama na akapelekwa mahakama ya wilaya flani huko kama Mlinzi pia mwaka jana hiyohiyo akapewa 500k ya kujikimu na akakuta mshahara laki tatu tu yaani 300k kwa mwezi na hakuna posho yoyote.

"C" Yeye aliajiriwa nadhani mwaka huu hapo DDC (Dar Es salaam Development cooperatin) kama "Security officer" pia, amefika kakuta mshahara 696k kwa mwezi na posho za zaidi ya 300k per month na pesa za kujikimu kapewa 900k

Huyu "D" na yeye ameajiriwa mwaka huu huko Ngorongoro Conservation kama mlinzi ( Askari wa wanyamapori) huyu kafika kule kakuta mshahara 960k na overtime inategemea na masaa yako ya ziada, na posho zingine nyingi na akapewa pesa ya kujikimu 3.4m

Nimejaribu kukupa mifano hii ya watu walioajiriwa vyeo vya chini kabisa ambao ni ndugu zangu wa karibu walioajiriwa hivi majuzi pamoja na kwamba ni kada moja na elimu yao ni sawa lakini unaona hapo kabisa kuna mmoja anaweza kumlipa mwingine mshahara wake wa mwaka mzima kutumia mishahara na posho zake za miezi isiozidi mitatu.

NADHANI UMEGUNDUA KITU HAPA.

Maslahi na mishahara inatofautiana kulingana na taasisi uliyopo boss
Iseee basii walimu was Tanzania tuna shida
 
Watu wanachelewa sana shule. Mimi nimemaliza degree tena ya miaka 4 na miaka 23, 24 kazini.
Yes siku hizi watu wanaanza shule mapema, mi nakumbuka nilianza darasa la kwanza baada ya kuweza kushika sikio la upande wa pili...we nae ulipitia hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka mwalimu degree holder.
Hujakosea kaka. Tukiambiwa jinsi scale za mishahara watumishi wa mashirika ya umma ss waalimu roho hua zinatuuma sana. Imagine mtu ana certificate ya fm 4 anakuwa na mshahara ambao mm degree holder nautafuta miezi mitatu yy anaupata mwezi mmoja aiseeeee afu mtu unafanya mistake kama hizooo yaaaan
 
Hujakosea kaka. Tukiambiwa jinsi scale za mishahara watumishi wa mashirika ya umma ss waalimu roho hua zinatuuma sana. Imagine mtu ana certificate ya fm 4 anakuwa na mshahara ambao mm degree holder nautafuta miezi mitatu yy anaupata mwezi mmoja aiseeeee afu mtu unafanya mistake kama hizooo yaaaan
Boss, yote maisha tu pambania kile mungu alichokujalia
 
umepata pesa bado kijana mdogo sana ni halali yako kufanya hivo.
kwenye maisha kila mtu ni lazma apite hii stage, wachache sana ambao hawapitii huku na uzeeni wengi wao lazma fanya upuuzi wa kushangaza hapo ndio unakuta mtu anachukua mafao anaenda kuolea mke wa pili.

Pambana kwa vile tayari ulishashtuka karibia miaka 5 iliyopita
Sawa Chief
 
Kijana akiweza kuepuka huu ujinga kwenye miaka yake ya mwanzo wa ajira atafanikiwa sana lakini ukweli huwa ni ngumu sana. Mimi nakumbuka nilishauriwa sana lakini bado nilifanya upuuzi mwingi tu mpaka mkopo wangu wa kwanza nikaishia kununua gari ili nioshee kwa wasichana, akili imekuja kunikaa sawa baadae sana jua lishakucha na utawala ni wa magufuli hapo ni mwendo wa kukimbizana sasa.
 
Kijana akiweza kuepuka huu ujinga kwenye miaka yake ya mwanzo wa ajira atafanikiwa sana lakini ukweli huwa ni ngumu sana. Mimi nakumbuka nilishauriwa sana lakini bado nilifanya upuuzi mwingi tu mpaka mkopo wangu wa kwanza nikaishia kununua gari ili nioshee kwa wasichana, akili imekuja kunikaa sawa baadae sana jua lishakucha na utawala ni wa magufuli hapo ni mwendo wa kukimbizana sasa.
Kweli Boss yaani unakuwa na behavior ambazo zinakuwa motivated by some external goals na ile nguvu ya kuzishinda unakuwa huna
Hebu fikiria kipindi hicho kwangu nilikuwa sijifikirii mara mbili kumkatia demu tiketi ya ndege ili anifuate nilipo tubanjuane, Yaani nilianza kumpandisha demu ndege kabla ya wazazi wangu waliohangaika na mimi kwenye mapito ya dhiki... Ujana kweli maji ya moto
 
Hongera kama umetambua ilo mkuu
Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.

Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 MUNGU akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k na bado kukawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi sijaona mlango wa ofisi, nakuwa safarini tu huko mikoani site kikazi napambana na per diem kila uchao.

Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika historia ya maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili, Ile ilikuwa ni zaidi ya "foolish age" nikajikuta nakosa kabisa personal recognition

Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.

Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa, lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi na NDOA ikawa tayari imefungwa kwa mtindo huo then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.

Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.

Baada ya kumaliza chuo 2015 , ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎

Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni

Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.

Japo cheo changu cha Sasa na mshahara ni tofauti na wa wakati huo, lakini bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika kwenye kichwa changu.

Nasherehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu nilizofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo


Yote hayo yamebaki kama "Yaliyopita si ndwele" yenye historia chungu na maisha mengine mapya lazma yaendelee
 
Back
Top Bottom