Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Miaka 10 ya Utumishi: Kumbukizi mbaya ya matumizi ya pesa isiyofutika katika historia ya maisha yangu

Hujachelewa mkuu kwanza nikupongeze kwa kushtuka mapema.Mimi nilidhani hiyo tabia ni kujiendekeza lakini nimegundua katika hiyo stage ya kushika hela umri huo ni ngumu kuepuka vishawishi,miaka 8 iliyopita nilipata kazi arusha Mara tu baada ya kumaliza stashahada ya juu katika fani ya uhasibu nikiwa na umri wa miaka 24,Ukwel kazi ilinilipa vizuri kiasi ningeweza kufanya mambo Makubwa kwani kipato kilikua kinaruhusu,kama unavyojua totoz za kijenge,mushono,pinpoint bila kusahau babilon na maeneo mengine ya Arusha ilikua hatari,kuchukua fastjet kwenda Dar es salaam kula raha kitu cha kawaida sana,kupandisha ndege totoz kuja arusha kitu cha kawaida ,mitungi ndo usiseme .Mimi mwenyewe nilikua nakaa nakumbuka nahisi ni akili yangu ile au nilirogwa?lakini sasa nimeamua kusahau yaliyopita na kusonga mbele na maisha yanaendelea japo mambo si mazuri sana kama wakati ule....
Ni ngumu mno Boss, yaani ule umri ni zaidi ya foolish age
 
Kuna mda huwa tunafanya makosa mengi sana katika maisha tena mengine ya kujitakia kabisa ambayo ukiyakumbuka baadae unayajutia sana. Binafsi kama ningetumia mda vizuri ningekuwa mbali sana sana kimafanikio kuliko nilivo sasa.

Kipindi namaliza O' level baada ya matokeo kutoka nikapangwa Moshi Technical kwa elimu ya Advance, nikabadili kwenda Dar Es Salaam Institute of Technology (DIT) kusoma FTC kwa miaka 3, nilipomaliza tu nikaunganisha degree MIST, nikiwa semister ya kwanza na umri wangu wa 21yrs naelekea 22 MUNGU akawa upande wangu nikaajiriwa nikiwa kijana mdogo kabisa nikiwa na 21 kama technician katika moja ya taasisi inayolipa vizuri sana hapa nchini ikabidi niahirishe chuo kwa mda niingie kwenye ajira hii ilikuwa 2009 mwishoni, kwa kipindi hicho kwa hiyo level yangu nilikuwa nalipwa 840k kama mshahara kwa mwezi, bado kulikuwa na housing Allowance 240k,Transport allowance 200k, posho ya mawasiliano 60k, Lunch 150k na Extra duty ambayo hii tulikuwa tunaingiziwa wafanyakazi wote sawa kila mwisho wa mwezi 350k na bado kukawa na safari nyingi sana ilikuwa ni kawaida kumaliza mwezi sijaona mlango wa ofisi, nakuwa safarini tu huko mikoani site kikazi napambana na per diem kila uchao.

Ofisi ilikuwa inatoa mikopo kwa wafanyakazi wake wapya ya bila riba za kujengea nyumba, kwa level yangu kipindi hicho nilikopeshwa 48m na zikawa zinakatwa kwenye posho na sio kwenye mshahara. Kiukweli kitu ambacho ninakijutia mpaka leo nikikumbuka naumia sana basi ni miaka yangu 4 ya mwanzo kwenye ajira (2009-2012) nilipoteza pesa nyingi sana kwenye mambo ya kijinga kabisa na badala yake nikawa mtu wa hovyo sana kuliko kipindi chochote katika historia ya maisha yangu, nadhani umri na kutopata washauri wazuri pia kulichangia hili, Ile ilikuwa ni zaidi ya "foolish age" nikajikuta nakosa kabisa personal recognition

Nilipopangiwa kituo changu cha kazi nilipewa 3+m za kujikimu, karibia robo tatu za hizi pesa nilitumia kujivinjari na wasichana wa CBE waliokuwa wananitolea nje kipindi cha zamani na kupandisha ndege totoz kwenda kujivinjari mikoani ilikuwa ni jambo la kawaida kwangu na hata nilipopewa pesa ya mkopo wa ofisi sikuweza kufanya la maana kubwa la kuweza kujivunia japokuwa kiasi cha pesa katika huo mkopo nilitumia kuwajengea na kukarabati nyumba ya zamani ya wazazi na mwaka uliofuata nikakopa CRDB tena 15m kupitia mshahara wangu, kipindi nakopa hii pesa nilikuwa nakaribia kwenda likizo yangu ya mwaka na asilimia 80 ya hizi pesa niliitumia kwenye starehe na wanawake kwenye hoteli tofauti tofauti, Sasa nikawa nakatwa kwenye mshahara na posho zinakatwa kulipia madeni ya mkopo nikawa napata kiasi kidogo tu japo kwa matumizi ya kawaida kilikuwa kinatosha kwa kujibana ikizingatiwa wazazi nao tayari nilikuwa tegemeo lao, Nikaanza kuishi kwa kutegemea zaidi per diem za safari za kikazi.

Mwaka 2011 nilimpa mdada mmoja mimba alikuwa anamalizia diploma yake TPSC ikabidi nikae nae kama mke wangu hata hatukufanya harusi mwenyewe hakutaka kabisa japo wazazi wa pande zote walitaka tufunge harusi kanisani na sherehe ifanyike na kiukweli hata uchumi wangu ulikuwa hauruhusu hili nadhani wife alisoma upepo mapema , Nilimshirikisha Mkurugenzi wangu tulichoafikiana na mwenzangu kuhusu ndoa yetu na jinsi ya kupata cheti cha ndoa ili aweze kupata bima ya afya kupitia kazi yangu kama mke wangu halali, Wakubwa wanajuana bhana, usiku wa siku hiyohiyo ananipigia simu akinitaarifu tujiandae kesho yake anakuja kutuchukua tukasaini cheti cha ndoa nadhani ilikuwa ni RITA pale kama kumbukumbu zangu ziko sawa.


Lilikuwa ni jengo la ofisi za mkuu wa wilaya na mle ndani ndo kulikuwa na hizo ofisi za RITA sikujua hata kimelipiwa bei gani hicho cheti tulisaini tu na mashahidi zetu wawili wa pale ofisini akiwemo mkurugenzi na NDOA ikawa tayari imefungwa kwa mtindo huo (hii NDOA sikutumia hata shilling 100, na tulikuwa watu 4 tu, Mimi, wife, mkurugenzi, Dereva wake na Afisa wa RITA aliyetukabidhi cheti na ilifanyika kwa mda usiozidi dk 15) then tukachukua vyeti tukamrudisha wife nyumbani mimi nikaingia kazini kuendelea na majukumu na hapa ndipo maisha mapya yalipoanza.

Mwaka 2012 nikahamishiwa Arusha na kupewa ruhusa ya kuendelea na masomo yangu ya shahada ATC kwa kujilipia mwenyewe, hapa pia ndipo nilipoanza kufeel ule ugumu wa maisha na kuona utofauti kati ya akili ya kikubwa na kitoto.Posho zina madeni, mshahara una madeni, safari zimepungua kwa sababu niko shule nina mke,mtoto wote wananiangalia mimi , maisha yalikuwa magumu sana kwangu kwa kipindi hicho huku nikiona wenzangu tulioajiriwa nao waliokuwa na umri mkubwa kidogo wao wakiwa mbali sana kimaendeleo na wakawa wananishangaa mimi kuona Inawezekanaje kuishi maisha yale ninayoishi na kwa namna ile tunayolipwa huku nikiwa sina majukumu mengi.

Baada ya kumaliza chuo 2015 , ikabidi nijipange upya na mkopo ukawa umemalizikia na hata biashara sikuwa nayo pamoja na kukopa pesa zote hizo na kuugulia maumivu ya mkopo kwa miaka 5 na dogo nae anatakiwa aanze kindergarten na tayari ana mdogo wake mwingine😀😀 MAISHA HAYA. nikaanza kusuka mipango upya utafikiri ndio nimeanza ajira rasmi, Kibaya zaidi kipindi hicho wenzangu nilioajiriwa nao baadhi wako mbali sana, wana familia, wana nyumba nzuri, wana gari na biashara zao wakati mimi nimepanga chumba kimoja tu wakati huo mpaka namaliza masomo yangu ATC😎

Yale maisha na nikiwaangalia wenzangu itabaki kuwa kumbukumbu mbaya kichwani mwangu, uzuri nilitambua baadhi ya makosa yangu mapema nikajipanga upya nikiwa na akili ya kikubwa zaidi kuliko wakati ule, Japo sio sana ila somehow nime - win kidogo, lakini sio kama hatua walizo nazo wenzangu, ningekuwa na akili ya kikubwa kipindi kile ningekuwa mbali, mwaka jana nimetimiza miaka 10 ya utumishi wa umma nikiwa mwajiriwa na naelekea miaka 32 kiumri miezi michache ijayo bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika katika fikra zangu.unaweza kudhani natania lakini huu ndio ukweli kiasi ambacho nikikumbuka inaniuma sana hata kuandika hapa nakuwa kama napunguza mzigo wa maumivu wa ujinga wangu niliobeba moyoni

Pamoja na yote, mungu alinionesha mwanamke bora sana kwenye maisha yangu ambae hata sikuwahi kufikiria kumuoa ilitokea kama emergency tu hakuwa kati ya wasichana niliodumu nao kimahusiano kwa mda mrefu wala sikuwahi kumpenda, moyo wangu ulipenda kwingine kabisa na hata kwenye mipango yangu hakuwepo kabisa. Lakini kadri nilivoishi nae nimefahamu KWELI MKE BORA ANATOKA KWA MUNGU, mawazo yake yamebadili KABISA maisha yetu , kuna mda naona kabisa huyu kanizidi uwezo wa kufikiri hapa namzidi pesa tu, ni zaidi ya spiritual woman na mrembo haswa ni kivile tu wanaume huwa haturidhiki lazma tukaonje radha zingine nje.

Japo cheo changu cha Sasa ni kikubwa na mshahara ni tofauti na wa wakati huo, lakini bado ile kumbukumbu inagoma kabisa kufutika kwenye kichwa changu.

Nasherehekea miaka yangu 10 ya utumishi nikiwa na mtazamo mpya kabisa wa kuacha kazi ndani ya miaka 5 ijayo nijikite zaidi kuendesha miradi na biashara zangu nilizofungua ili kufikia malengo yangu niliyojiwekea. Kwa sasa ni baba wa familia, nina watoto kadhaa na mwanagu wa kwanza nimempata nikiwa na miaka 23 tu kwa sasa ana 8yrs anaelekea 9 miezi michache ijayo


Yote hayo yamebaki kama "Yaliyopita si ndwele" yenye historia chungu na maisha mengine mapya lazma yaendelee

Kweli mademu sio watu wazuri.... Wacha nijiunge chaputa tuu huku hela zangu nazichungulia kwenye kibubu changu.

Pole sana m, ee ila vijana wengi wanakoseaga pale wanapopata kazi yenyekulipa vizuri wanaanza mambo ya papuchi... Wakati wa neema ndio muda wakuweka akili sawa na kuishi kimaskini kadri iwezekanavyo hapo ndio utapiga maendeleo.
 
na huyu mwanamke cha kushangaza sikuwahi kumpenda hapo mwanzo, na wala hakuwa kwenye mipango yangu ya maisha nilikuwa kama napiga tu kwa kipindi hicho, moyo wangu ulikuwa umetekwa na wasichana wengine kabisa.

mara paap mambo yakawa vice versa ana mimba ikabidi nivute tu ndani, NOW ndio nafahamu huyu ndiye mungu alipanga awe mke wangu. Kama mwanaume bado naenda mechi za nje but namuheshimu sana

Bora wee unajisemea ukweli kuwa unasasambua papuchi zingine
 
Mitandao imesaidia wengi sana kwa kuanika ukweli na wengi kujifunza kutokana na makosa
Enzi zetu tulijifunza kupitia nyimbo za band mbalimbali ambazo zilikuwa na mafundisho mengi ingawa sio kihivyo kama vijana wa sasa mnavyopata fursa ya kuwaelimisha wengine

Wengi wamebadilika na wengine bado wanaona kama mda bado na kutokuelewa nini maana ya maisha

Big up Mkuu na huu ndio mda wa kutokujiangalia wewe bali wajengee misingi mizuri wanao ili wasihangaike na maisha baadae kwani ni circle of life
Leo tupo na kesho hatupo
 
Mitandao imesaidia wengi sana kwa kuanika ukweli na wengi kujifunza kutokana na makosa
Enzi zetu tulijifunza kupitia nyimbo za band mbalimbali ambazo zilikuwa na mafundisho mengi ingawa sio kihivyo kama vijana wa sasa mnavyopata fursa ya kuwaelimisha wengine

Wengi wamebadilika na wengine bado wanaona kama mda bado na kutokuelewa nini maana ya maisha

Big up Mkuu na huu ndio wa kutokujiangalia wewe bali wajengee misingi mizuri wanao ili wasihangaike na maisha baadae kwani ni circle of life
Leo tupo na kesho hatupo
Kweli mkuu ndicho ninachokimbazana nacho kukifanya kwa sasa
 
Kweli mademu sio watu wazuri.... Wacha nijiunge chaputa tuu huku hela zangu nazichungulia kwenye kibubu changu.

Pole sana m, ee ila vijana wengi wanakoseaga pale wanapopata kazi yenyekulipa vizuri wanaanza mambo ya papuchi... Wakati wa neema ndio muda wakuweka akili sawa na kuishi kimaskini kadri iwezekanavyo hapo ndio utapiga maendeleo.
Shida inakuja kuishinda hiyo tamaa Kipindi ukiwa na pesa na Uhuru wako katika umri huo
 
Nn lakini unataka kumtia presha mwenzio?

Mambo ya X yanatoka wapi? Mwisho utaanza kuropoka kuwa ulikuwa unapasha kiporo,,

Nahisi ni kweli, umeusoma uzi na ukakumbuka story alizokuhadithia x wako ukaunganisha dot,,dot,,

Sent using Jamii Forums mobile app
Ofcouse ila kademu kangu tulisha achana ukweliukweli..!
 
Shida inakuja kuishinda hiyo tamaa Kipindi ukiwa na pesa na Uhuru wako katika umri huo

Bwana wee yaani hapo ndio changamoto... Maana warembo wenyewe ndio kwanza wanajileta huna shida ya kuwatogonza... Unajiokotea tuu kama mizoga.... Its quite challenging kusema ule ukweli.

Naelewa unachoongea maana ilishanitokea mie dah nilizisasambua ila ndio hivyo tena mihela imepotea kichizi alafu huna la maananumefanya.
 
Mkuu haya mambo ni Kama uteja ni ngumu sana kuyaacha kabisa

Ah mie nilishajichokea na kujaribubfight hiyo temptation... Wacha njwagegede tuu hamna jinsi maana pale kati ni patamu... Kujisemea rais mstaafu... Vijana wanapataka wazee wanapata 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom