Miaka 12 ya Samaki Samaki, mjue "Kalito Samaki"

Miaka 12 ya Samaki Samaki, mjue "Kalito Samaki"

Sasa wewe ndy mfano halisi wa baadhi ya watu kwenye jamii ya kitanzania wenye mawazo mgando! Una low self esteem, ndy maana unakuwa una shida na watu wenye mafanikio, na naamini hii shida yako si kwa bwana Kalito tu, itakuwa ni kwa yyt mwingine.....inajidhihirisha wazi kuwa umekata tamaa ktk maisha yako kwa chuki zisizokuwa na mbele wala nyuma kwasababu tu hupendi maisha yako, hupendi maisha unayoishi, na hauna namna ya kujikwamua toka hapo ulipo, kwahy ili kuipa faraja nafsi yako basi unaamua kumchukia mtu yoyote aliekuzidi iwe kipato, elimu, uzuri etc, trust me sweetheart ur not alone on this, wapo wengi kama wewe na shida kama hii inajulikana. My very good advice to you mkuu... Jenga mazoea ya ku appreciate vitu vizuri bila ya kuangalia upande mbaya, itakusaidia sana ktk maisha yako. La, huwezi, wahi kwa 'councillor' ukapate msaada zaidi.

Mimi sina ushahidi wa kuwa alitumia pesa ya kuuza unga kuanzisha biashara yake, wewe ambae unao ushahidi usio na shaka ndani yake uweke basi ili sheria ifuate mkondo wake na wengine wapate somo.

Kwa upande wangu, hoja yangu si namna gani kapata mtaji wa kuanza kufanya biashara( sababu hainihusu, na naamini hata wewe pia haikuhusu), bali hoja yangu mimi ni namna anavyopambana kuendelea kubaki kwenye soko, mbinu anazotumia, ubunifu, n.k. kitu ambacho kipo wazi kinaonekana.

Kuna msemo wa kingereza unasema:

"Stay away from negative people, they always have problem to every solution "

Adios!
Acha kutetea upuuzi na kuandika magazeti mareeefuu yasiyo na point.
Huyu akiwa role model wa watu means wakauze madawa nao waweze kufikia alipo? Nani asiyejua Barman Tanzania analipwa hela mbuzi?
Mtu anayetakatisha fedha huwezi kumsimamisha popote useme muigeni!!!!!!! Fanya kitu halali fanikiwa and BE A GENUINE ROLE MODEL with your creativity !

Nyie ndio watetea ujinga mnafanya watu watafute easy money waishi vizuri, hamuangalii wala kuwa concerned na hela halali mnachoangalia ku win tu whether kwa upanga au kwa kuiba then usimame jukwaani udanganye watu. Cut the crap boy!
 
Ni miaka kumi na mbili (12) tangu kuanzishwe migahawa hii maarufu hapa bongo, kwa ambao washapata huduma za samaki samaki watakuwa mashahidi juu ya ubora, huduma nzuri na kikubwa ubunifu unaotumika kutoa huduma zao.

A man behind all these creativity sio mwingine bali ni Carlos Bastos ama "kalito samaki" kama wengi wanavyomfahamu. Jamaa ni muhispania aliyeishi bongo miaka mingi akiwa ni mtoto pekee kwenye familia yao. Kalito ana watoto watatu, wawili akiwa amezaa na mbongo huku mmoja wa mwisho akiwa amezaa hivi karibuni na muhispania mwenzake.

Licha ya kuwa muhispania kalito ni muabudu mzuri wa tamaduni za kitanzania ambapo mara nyingi utamkuta kavaa kimasai au msuli kama mtu wa pwani, Pia jamaa ni mtu wa watu sana ambapo muda mwingi hujichanganya na wateja zake kitu kilichompelekea kutengeneza marafiki wengi hasa wasanii.

Mnamo mwaka 2014 kalito aligundulika na melanoma (skin cancer) kwenye jicho lake la kushoto hali iliyompelekea kupoteza matumaini ya kuishi kabisa.

"Hii ni aina ya kansa , inayotokea mara chache. Kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu tatizo la kansa sio kwakuwa iko eneo moja itabaki hapo tatizo ni kuwa ina uwezo wa kusambaa mwili mzima na kwa kawaida ikifikia hatua hii una kufa”

Alinukuliwa wakati akihojiwa na mtangazaji maarufu hapa bongo.

“Ile hali ya kuwaza muda wowote utakufa ilibadili sana maisha yangu na kunifanya niwaze tofauti nikaanza kujifunza vitu vipya ni kwa kiasi gani ili kulinda afya yetu tunatakiwa kula vizuri
Nimejifunza kufurahia kila wakati ninaopata kwakuwa sijui ni lini itakuwa siku yangu ya mwisho maisha yangu yakabadilika na sasa nimekuwa makini zaidi na maisha pamoja na ninayoyafanya”

Kalito aliamua kurudi kwao hispania kwa matibabu ambapo alifanyiwa operesheni ya kuondoa jicho la kushoto ambapo akaja na style ya kuvaa kitambaa cheusi (patch) kwenye sehemu ya jicho lake.

Ukiacha maisha yake binafsi Kikubwa kilichonifanya nimzungumzie huyu jamaa leo, ni ile roho ya upambanaji aliyokuwa nayo na ubunifu wa biashara ambapo kiukweli ni jambo la kujifunza. Kuna migahawa mingi sana bongo lakini mgeni huyu ameteka soko na kutengeneza jina kubwa kwenye biashara ya chakula na vinywaji.

Hili ni jambo la kujifunza kwa vijana na watu wanaoamua kujiajiri kuwa kitu chochote unachofanya kinahitaji ubunifu na focus kwenye kufanikiwa.

Wengi wanaweza kudhani jamaa alianzia hapo juu kwenye kumiliki migahawa lakini kiukweli jamaa alianzia chini kama Barman kwenye mgahawa wa CHUI BAY sasa ukifahamika kama Capetown fish market, alihudumu hapo kwa muda kadhaa kabla hajaanza kumiliki migahawa yake mwenyewe (the hustle was real).

Cha kujifunza ni kutokukata tamaa na kuweka malengo bila kusahau ubunifu kwenye kila unachofanya. Keep your dream alive, everything is possible for those who believe.

let's meet at the top. Cheers [emoji1635]View attachment 1231241View attachment 1231242
Huyo jamaa nilianza kumfahamu baada ya kuona video ya linex sunday mjeda na kwenye video alikwepo carlos "Kama vipi tukutane samaki samaki ndio kiwanja nachoenda".

 
Tatizo wengine hapa watakuja wanajifanya wanamjua jamaa baada ya samaki samaki za masaki na mjini maybe na mlimani. Hawajui jamaa alianzia mbezi beach makonde na ndo wa kwanza kuleta theme ya culture kwenye biashara ya bar. Kila sehem watu wakaanza kutengeneza meza za mitumbwi, na vitenge kwa wahudumu.


The dude is good
Ilianza ya Mlimani City ndio the same year ikafata ya Makonde pale..
 
Alichokifanya hapo ni kutakatisha pesa. Alitoa kwenye biashara haramu na kuanzisha biashara halali. Halafu anakudanganya alikuwa muuza Bar mpaka kuanzisha migahawa yake. Thubutu. Hasemi ukweli. Ukweli ni kuwa ni muuza madawa ya kulevya sema anatakatisha tu pesa ili aonekane anafanya biashara halali.
Nakubaliana na wewe 100%,hawa watu huwa wanatudanganya sana na nilianza na kushona viatu,nilianza na mtaji wa elfu 10 mara nilianza na uhausigelo na bla bla bla kibao ,kumbe nyuma ya pazia kuna vitu walifanya wakapata greenlight(wakatusua),haiwezekani barman aje kuwa bilionea ,alikuwa analipwa Tsh ngapi kwa mwezi? Mtaji wa kuanzisha samaki samaki mlimani city ulitokana na mshahara wake?
 
Masikini kalito..nilijuaga swaga tu kumbe ugonjwa umepelekea awe ivyo.

Ila Mimi michoro yake tu na urembo wa masikio yake ndivyo vyaniachaga hoi.
 
Huyo jamaa nilianza kumfahamu baada ya kuona video ya linex sunday mjeda na kwenye video alikwepo carlos "Kama vipi tukutane samaki samaki ndio kiwanja nachoenda".

Yeah ni kweli mkuu, pia amepata kuonekana kwenye nyimbo za wasanii wengine kama fid q n.k
 
Biashara nyingi sana duniani kote huletwa na wageni
Bila wahindi tusingezijua Shanga na bila Italians pasta tungeiona kwenye tv tu
Kutembea pia kunakuongezea maarifa na kujua biashara nyingi na kuzileta kwenu
Tuwakaribishe wa nje kuwekeza kwa manufaa ya nchi na uchumi kupaa
 
Watz bhana,yani ukifanikiwa tu hawakosi tu la kusema,

kama kweli biashara ya unga kuifanya ni rahisi,jaribu kuifanya tuone kama utapita pale airport kirahisi,jaribu pia kumheshimu aliye fanikiwa kupitia drugs business cz siyo kaz rahis eti.
 
Back
Top Bottom