Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Wewe umegundua nini? Hebu tuelezee ulichogundua..ni kama unakitu hivi unataka kusema kuhusu hyo lost life of Jesus ila umebaki pending..
Nimekwisha andika mkuu unaweza ukapitia andiko
 
Unachanganya mambo, mengine keeli, mengine ya kubumba.

Source yako ni nini??
Vyazo ni vingi sana tatizo wengi huzani Spiritual knowledge inachanzo kimoja tuu na ncho kitabu cha dini yake. Kama mkristu anzani ni Biblia au kama Muislam basi ni Koran. Lengo ni kumjua na kumfuata Mungu basi soma vitabu vyote. Soma Biblia, Koran, Hindu Scriptures, Bavgad Gita, Upanishad, The Sufis, The true Scriptures na vitabu vingi vya philosophy. Lengo ni kufika kwa Mungu kwa njia yeyote ile udijali kichochoro ulichotumia. Kwa experience yangu hata vitabu sio jibu sahihi ya kupata elimu ya uungu (God's knowledge)ni motisha tuu. Njia sahihi ni Meditation na Contemplation ili kupata inner spiritual knowledge (elimu ya Rohoni). Any way swali lako ni what is my source?. Ni research niliyofanya juu ya dini na Cults mbalimbali. Kwenye mafunzo yangu ya Yoga na Meditation kwa zaidi ya miaka 40. Buddas na Monkis wanajua sana historia ya Yeshua of Nazzareth (Yesu) kwani ndio walimfundisha elimu ya uungu na kufanya miujiza ndio wale wakiitwa Mamajusi kwenye Biblia.
 
Habari za Mida hii Ndugu Zangu Naomba kuanza kwa kuwatakia Sikukuu njema ya Kuzaliwa kwa Yesu kwa wale wote wafuasi wa imani ya Kikristo na hope mnaenjoy sana Happy noela

Kabla ya yote ningependa kurejea Luka 1:1-3 Kama inavyosema;
..."Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu,.........,"

Miaka 2000 iliyopita katika Mji wa bathelehem ya Uyahudi Alizaliwa Mtoto Aliyepewa Jina la Yeshua/Yehoshua ama yesu au Issa unaweza kumuita utakavyoweza kuita kwa lugha yako ilimradi imani ibaki kuwa alizaliwa Mtoto Ambaye ni Mtu muhimu sana katika historia ya ukombozi wa Wakristo duniani,

Na maandiko yote Yameandika kuhusu yesu kuzaliwa kwake,Miujiza yake mafundisho yake kuishi kwake ,Kusulubiwa kwake na kufufuka kwake na hata kupaa kwake kwenda mbinguni.

Maandiko yote ya biblia yaliyopo yanaanza kuzungumzia yesu kuanzia alipokuwa anazaliwa mpaka akiwa na umri wa miaka 12 (Soma luka 2 yote,pia soma mathayo 2)

Lakini baada ya miaka hiyo 12 Biblia ikawa kimya mpaka tena pale ambapo yesu anatimiza miaka 30 ya maisha yake ndo tunaona yesu anaanza kutajwa tena,kipindi anabatizwa na yohana Mbatizaji..(luka 3:23,Marco 1;9 ,Mathayo 3 kuanzia aya ya 14 na kuendelea)

Lakini miaka yake yote kuanzia umri wa miaka 13 mpaka 29 hakuna sehemu yoyote ya biblia inayotaja maisha yake alikuwa wapi? Alifanya nini? Aliishi wapi? na ilikuwaje?
basi nitajaribu kupitia baadhi ya theory na nakala za vitabu ili tuende sawa katika kujibu haya

HOJA KWA UFUPI

Maisha ya yesu kipindi Akiwa hai hakuna aliyekuwa anayanakili ama kuandika maisha yake kwakuwa Maisha yake na injili hii imekuja kuandikwa Miaka 70 mpaka 140 baada ya kifo chake.
Japo inasemekana historia ya yesu ilikuwa inaelezwa kuwa Masimulizi kumhusu yesu yalikuwa yakifahamika kwa watu wengi Sana kwa muda mchache.
kulingana na Injili ya yohana Yesu alifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu na kulingana na injili za ki"synoptikia" (synoptic gospels) Yaani Luka matayo na marko alifanya kazi kwa muda wa miaka 2 mpaka mitatu kabla ya kifo chake...
Japo kuliandikwa Vitabu vingi sana zaidi ya 100 kuhusu maisha ya Yesu lakini vitabu 4 tu vya injili ndiyo vilivyokubaliwa kuingia katika biblia rasmi iliyoamriwa kutumika...

Mengi tunayoyajua kuhusu yesu Tunayatoa katika vitabu vinne tu vya injili yaani marko,mathayo luka na yohana,japo vitabu vingine ambavyo havikuingizwa kwenye biblia bado vipo na vingi viko maktaba vimehifadhiwa kwa na unaweza ukaviita APOKRIFA GOSPELS na vina mambo mengi sana ambayo huwezi kuyakuta kwenye biblia na mara nyingi huwa hayaruhusiwi kuzungumzwa kwa uwazi na mengine utayakuta kwenye biblia..
Kwanini hawakutaka kuviingiiza kwa kisingizio cha KUVUVIWA ama canonical views ?.....
Baadhi ya Vitabu Hivyo vingine huzungumzia Maisha ya yesu akiwa na umri wa miaka 13 mpaka 29 kama kitabu cha The Gospel of Mary, Injili ya mtoto yesu na vinginevyo....

UCHAMBUZI

Dr.Elizabeth McNamer,Proffesor of theology and religious history wa rocky Mountain college Huko Billings Montana,
ambaye kwa Miaka 14 Amekuwa Mkurugenzi mkuu wa Bethsaida Biblical Archaeological Excavations in Israel ( Machimbo ya Kiakiolojia ya kiblia huko Israel) Pia ni proffesor maarufu kwa ufundishaji wake wa Maandiko huko Asia Na anaposcast yake kuhus Historia ya Biblia.Katika moja ya mahojiano yake aliwahi kunukuliwa akisema
"Ililichukua kanisa miaka isiyopungua 500 kujadili mambo mbalimbali kuhusu Yesu, na kipi kiwemo kwenye biblia na kipi kisiwemo na kipi kiandikwe na kiandikwe vipi na kipi kiachwe kabisa na kisizungumzwe tena Na wengi hawajui kuwa kuandikwa kwa biblia ya sasa kulichukua miaka mingi sana ,Huku pia kanisa likijadili Yesu anatakiwa kuonekana vipi mbele za jamii..."

Hiyo ni wakati akijibu moja ya maswali kuhusu kitabu chake cha Jesus and First-Century Christianity in Jerusalem by Elizabeth McNamer,

View attachment 2457658

Kutokana na kutokuonekana kwa historia ya Yesu Katika miaka 18, hii ni kuanzia miaka 13 mpaka miaka 29 kwenye biblia kumezua mijadala mingi sana katika Jukwaa la wana theolojia na wasomi wa dini wabobezi wa kikristo mpaka ikafika hatua Wakaunda theory zao ama hypothetical Views zao na Wote wakaipa majina miaka hii kama.. The lost years of Jesus Christ "Miaka iliyopotea ya Hostori ya Yesu kristo" na wengine waliita "The unaccounted years of Jesus Christ" Pia huitwa the silent years au the missing years ...

MILA NA DESTULI ZA KIYAHUDI KUHUSU MIAKA ILIYOPOTEA YA YESU NA CHANZO CHA NADHARIA

Hapa tutaangalia mila na desturi za kiyahudi kuhusu miaka hiyo inayosemekana kutokupatikana historia ya yesu Kama wewe ni mfatiliaji wa mila na desturi za kiyahudi na kiAramaiki utakuwa si mgeni wa maneno kama Bar-Mitzvah au Bat-Mitzvah..

Hizi ni mila kama mila za kwetu africa au kwetu huko uziguani,Au huko kwetu uzaramoni au umasaini na kwingineko...
Kwakuwa yesu alikuwa ni mmoja wa Wayahudi katika kabila la kiAramaic hivo alifata Tamaduni zote..

"Bar Mitzvah" maana yake halisi ni "mwana (wa kiume) mwenye amri." "Bar" ni "mwana wa kiume" katika Kiaramu, ambayo ilikuwa ni lugha ya watu wa Kiyahudi.
"Mitzvah" ni "amri" katika Kiebrania na Kiaramu.

"Bat" ni binti katika Kiebrania na Kiaramu. (Matamshi ya Ashkenazic ni "bas").

Kitaalamu,Maneno hayo humaanisha mtoto anayekua, na ni sahihi kabisa kwa mila za kiyahudi kumuita mtu kama "kuwa bar (au bat) mitzvah.

"Hata hivyo, neno hili linatumika zaidi ku sherehe za ukuaji zenyewe, na kuna uwezekano mkubwa wa kusikia kwamba mtu "ana bar mitzvah" au "alialikwa kwenye bar mitzvah."

Sasa sherehe hizi zikuwaje na zilimaanisha nini
Mtoto wa kiyahudi zamani hizo mpaka leo kwa kufata sheria za Musa (zilizopo kwenye talmud) Anapofikisha umri wa miaka 13 (kwa mtoto wa kiume) na miak 12 (kwa mtoto wa kike) huhesabika kama amekuwa na hufanyiwa sherehe hiyo ya Mitzvah ili ayavae majukumu yake mapya na ieleweke kwamba mtoto akishafanyiwa sherehe hii hawi tena chini ya uangalizi wa wazazi hiyo umaanisha kwamba hawi chini ya amri ya wazazi na ndo maana ikaitwa Bar/Bat mitzvah..

Na ni mujibu baba kufurahi na kumpa maneno mazuri ya wosia mtoto huyo kwani Baba amejitoa katika responsibikity za mtoto huyo kwahyo dhambi zake na maamuzi huwa yapo chini ya mtoto (hapo mwanzo kabla ya miaka 13 mtoto huwa chini ya kifungo cha miaka na wazazi wake hivyo dhambi na malezi yote huwa chini ya wazazi wake) sherehe hizi hufanyika siku ya sabato....

Na mtoto huwa na ruksa ya kwenda mahali popote atakapo..

(Rejea ya Tamaduni hii ipo katika kitabu cha Talmud na inafanywa na wayahudi mpaka leo)..

Mila hizi zinahusianaje sasa na upotevu wa maisha ya yesu kuanzia miaka 13-29?

Inasemekana kwamba baada ya yesu kuwa tayari amekuwa Bar-Mitzvah akiamua kwenda sehemu mbalimbali kutafuta Elimu huku akiiacha Yerusalem na kurafuta elimu sehemu mbalimbali za nchi zote duniani na Hatimae kurudi Akiwa na miaka 30
(Ambayo pia ni miaka ya Kuhubiri na utume kwa mujibu wa Talmud)

Katika miaka ya 1800-1900 kuliibuka nadharia "Hypothetical views" nyingi sana kuhusu the lost years of jesus christ,Japo wanatheolojia wengi wa kisasa yaani morden theologists wanasema kuwa Yesu aliishi Nazareth na alikuwa akifanya kazi na baba ake kama fundi selemala Japo hili linakosa ushahidi zaidi wa moja kwa moja wa kimaandiko kwenye biblia zaidi ya ushahidi wa mathayo 13:55 na Marko 6:3 japo ukiangalia vizur utagundua ni andiko moja lenye sentensi moja na lenye maana tofauti huku kwwnye mathayo limetajwa tofauti na kwenye marko limetajwa tofauti labda ni katika zile njama Dr Elizabeth McNamer alizokuwa akitueleza..sasa twende kwwnye nadharia hizo kuhusu miaka iliyopotea .....

1.EARLY THORIES (about early as possible as 70-1600 Ad)

Nadharia za awali Kuwa kuna uthibitisho gani unaounga mkono imani kwamba Yesu alisafiri maelfu ya maili kutoka Yudea hadi nchi nyingine?
Vyanzo vya kwanza kabisa vinatoka katika maandiko ya Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Bethlehemu ni mahali ambapo inaaminika kuwa Kristo alizaliwa, lakini Injili zinasema familia yake iliondoka mara baada ya hapo na kukaa katika mji wa Nazareti, kutimiza yale ambayo manabii katika Biblia walitabiri; kwamba Yesu ataitwa Mnazareti. Nazareti lilikuwa eneo tulivu, la kilimo na la uvuvi ambapo jamii iliishi maisha yasiyofaa, ikidokeza kwamba hadhi ya Yesu ilikuwa ‘Blue collar’ huku yeye na baba yake seremala

Yusufu wakipata riziki zao duni kama mafundi. Huku kukiwa na matarajio machache ya kazi, nadharia moja ni kwamba huenda Yesu alitafuta kazi fulani umbali wa maili tatu katika mji wenye shughuli nyingi wa Sepphoris katika eneo la kati la Galilaya katika Israeli ya leo, mji uliojulikana wakati huo kwa michoro yake maridadi sana iliyotengenezwa na Waruma. Kukiwa na fursa nyingi za kujenga nyumba na kuta,

Huenda mji huu ukawa ndio hatua ya kwanza kuelekea mahali panapoaminika kuwa mahali pa kuanzia kwa jitihada ya Yesu ya kupata nuru ya kiroho. Ikiwa kama vile wasomi fulani Wakristo wanavyoamini kwamba Yesu alitumia muda mwingi wa miaka hii ya kati akifanya kazi ya seremala katika Galilaya, kuna marejezo machache kuhusu hilo katika Biblia. Pengo la miaka kumi na minane katika maandiko limetokeza nadharia kadhaa za kushangaza, lakini hadi sasa hakuna iliyothibitishwa na ushahidi wa kutegemewa.

2.WALKABOUT (MATEMBEZI)

Nadharia nyingine ni kuhusu Yesu na miaka yake iliyopotea ni kwamba alienda ‘kutembea’ kutoka nyumbani kwao Nazareti. Ikiwa tukio hili linatokea Yesu alikuwa mvulana wa miaka 12, kwa hiyo kijana kama huyo anaonekana alikuwa na uwezo upi wa kihisia-moyo na ujuzi gani ili kuchukua safari kubwa na inayoweza kuwa hatari? Sawa endelea
Yaelekea zaidi alipokuwa akiishi Sepphoris, Kijana Yesu anaweza kuwa alipata ujuzi wake wa mapema wa ulimwengu kupitia lugha ya Kiaramu na kujifunza kusoma. Andiko moja linalodokeza hilo linapatikana katika Injili ya Luka, inayosema kwamba Yesu aliingia katika sinagogi na kusoma kitabu cha kukunjwa cha manabii. Wakati huu akiwa kijana, angepitia moja kwa moja unyanyasaji wa kijamii na kiuchumi wa wakulima wa Kiyahudi wa Kipalestina wa wakati wake, ambao alikuwa sehemu yao. Huenda ujuzi huo ndio uliomtia moyo Yesu kutafuta majibu katika ulimwengu wa nje na huenda ukawa na uvutano juu ya uamuzi wenye utata wa kuacha familia yake.

Wasomi wa elimu ya Historia ya kidini wanaamini kwamba
Yosefu baba wa Yesu alikufa alipokuwa na umri wa miaka 12 hivi na kwamba tukio hilo lenye kuhuzunisha ndio lilikuwa kichocheo kwake, akiwa bado mvulana mdogo, kuanza jitihada ya kibinafsi ya kupata nuru ya kiroho. 'Matembezi' haya yaliyodumu kwa takriban miongo miwili yanaweza kuwa yalianza muda mfupi baada ya kuwa na umri wa miaka 13. Ni katika umri huu hatari ambapo madai ya ‘mengi ya miaka 18 uya upotevu wa historia ya yesu’ huanza na nadharia nyingi za mahali ambapo Yesu alitumia miaka yake ya malezi kukua na kuwa mtu mzima ziko wazi kwa tafsiri nyingi.

Haidhuru Kijana yesu alikuwa na jukumu gani kwa mama yake na jamaa zake huko Nazareti,
ulikuwa uamuzi wenye kutatanisha kuwaacha watu wake wa karibu katika umri mdogo kama huo, alipokuwa akianza safari ya ajabu na hatari kwa miguu. Hata hivyo, baadhi ya Wakristo wanaamini kuwa miaka iliyokosekana haina matokeo madogo na ufunuo wowote kuihusu hauwezi kuleta mabadililko yoyote...

3.VATICAN'S SECRETS (Siri za Vatikani)

Kumekuwa na uvumi kwa miaka mingi kwamba Vatican ina ushiikilia ukweli huu kuhusu maisha ya Yesu na miaka kumi na minane iliyopotea,kwa madai kuwa Habari hizo zinaweza kubadilisha sana imani ya dini ya kikristo ya leo,
Hata hivyo hakuna kilichofichuliwa kuhusu kuwepo kwa hati hizo na kile ambacho Yesu alikuwa akifanya na mahali alipokuwa kuanzia umri wa miaka 13 hadi 30. Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba alitumia miaka hii isiyo andikwa kusafiri kwenda Uingereza akiwa na 'Yosefu wa Arimathaya', huku wengine wanaamini alisafiri hadi India na Uajemi. Mwishoni mwa karne ya 19 msafiri Mrusi Aitwaye Nicolas Notovitch alidai kwamba aligundua maandishi ya kweli katika nyumba ya watawa huko India ambayo yalithibitisha kwamba Yesu alisafiri na kufundisha huko na kwingineko Mashariki.

ZIKO THEORY NYINGI SANA NITAENDELEA KUZINDIKA KADRI NIPATAVYO UWEZO

CLARIFICATION
To declare interest "Part of the story was done on wasafi Tv the "storybook"
Sasa, haya MA theory yanatusaidia mini kwenye karne ya 21! Hayatatui shida za foleni na usafiri Dar, hayaleti mapinduzi kwenye kilimo, na sayansi! Hayaleti ajira,wala huduma Bora za afya, dini zilianza miaka 2000 iliyopita! Walioandika hii biblia,wametafsiri kutoka lugha mama ya kipindi hicho, na kuna makosa kibao wamefanya, ungekuwa unaleta vifungu kutoka lugha mama, angalau!
 
Vyazo ni vingi sana tatizo wengi huzani Spiritual knowledge inachanzo kimoja tuu na ncho kitabu cha dini yake. Kama mkristu anzani ni Biblia au kama Muislam basi ni Koran. Lengo ni kumjua na kumfuata Mungu basi soma vitabu vyote. Soma Biblia, Koran, Hindu Scriptures, Bavgad Gita, Upanishad, The Sufis, The true Scriptures na vitabu vingi vya philosophy. Lengo ni kufika kwa Mungu kwa njia yeyote ile udijali kichochoro ulichotumia. Kwa experience yangu hata vitabu sio jibu sahihi ya kupata elimu ya uungu (God's knowledge)ni motisha tuu. Njia sahihi ni Meditation na Contemplation ili kupata inner spiritual knowledge (elimu ya Rohoni). Any way swali lako ni what is my source?. Ni research niliyofanya juu ya dini na Cults mbalimbali. Kwenye mafunzo yangu ya Yoga na Meditation kwa zaidi ya miaka 40. Buddas na Monkis wanajua sana historia ya Yeshua of Nazzareth (Yesu) kwani ndio walimfundisha elimu ya uungu na kufanya miujiza ndio wale wakiitwa Mamajusi kwenye Biblia.
Hivi vitu taabu yake watu hatupendi kuvichimba mpaka ndani. Mfano saayansi, ukiichimba mpaka ndani kabisaaa, itakupeleka kwenye njia mbili.

1. Ukubali kuwa Mungu yupo
2. Uamini kuwa hakuna Mungu

Na hata ukikazana kwenye namba mbili, hautokaa upate majibu milele, zaidi ya kujidanganya.

Na namba moja nayo pia usipokua makini utasema kua Mungu naye katokea wapi, na Mungu wake nae katokea wapi, na kadhalika na kadhalika, mwishowe utajitengenezea ile paradox isioisha.

Meditation ukizifanya, uwe makini sana, zinaweza kukupa kifo cha kiroho, na hiki ni kibaya sana, maana ni cha milele.

Falsafa nayo ukiichinguza kwa undani inakupeleka kwenye spiritual realms and ideologies zilezile zinazoendana na meditations, ambazo unakuwa tuu unaingia kwenye ulimwengu wa kiroho kama kwenye dini. Changamoto ya hizi meditation unakuwa kiumbe huru katika ulimwengu wa kiroho, (independent) pasipo uangalizi (protection) ya mtu au kitu au jambo au spirit yoyote ile.

Kwa mfano, Dini ya kikristo unaweza fanya meditation kwa msaada wa Roho Mtakatifu, na ukaiona Mbingu, ukaona hata Kuzimu, ukaona nyota na sayari, as long as unatii na kufuata vile Roho wa Mungu anavyokuongoza, na kutumika katika ufalme wake.

Kwa wachawi, unaweza pia kufanya utawala wa ulimwengu wa roho, (lakini nadhani hawa wanatumiaga nishati nyingi sana, na nguvu yao ni ya kuwa inaishiaga hapahapa duniani)

Kwa waislamu, sina uhakika, kwa sababu mimi sio muislamu, na sijachunguza kwa undani zaidi.

Ila kwa wakristo najua, na inawezekana, na huko kote unakua na ulinzi wa Roho mtakatifu na Utiisho wa Malaika wa BWANA wanakulinda katika ulimwengu wa roho.

Sasa inshu sio kumjua Mungu na kumkaribia, maana wengine wanajiita Mungu lakini ni miungu, na wanavaa sifa na utukufu ili wainuliwe juu, na wameshajitengenezea mifumo yap ya kuabudiwa kama Mungu mwenyewe, lakini gharama zake sasa za kuwatumikia ndio zinakukosti sana, mf. Sadaka za damu, nyama na fedha, mali, maagano, n.k.

Kwa mkristo sadaka ilishatolewa moja ya pekee, ambayo ni Yesu Kristo, yeye anakupa ufalme wote wa mbinguni, na mamlaka ya kufanywa kuwa Mwana wa Mungu, Kuhani (au kwa lugha ya sasa, Balozi/Diplomat wa ufalme wa (au serikali ya) Mbinguni, Hii unakuwa na free pass ya kwenda mbinguni hata kama una dhambi, (maana ushakua Balozi, so, serikali inakua inakumiliki), ila pia vigezo na masharti kuzingatiwa..

Nadhani nimeenda mbali sana, nisamehe, ila i hope nimeeleweka japo kidogo
 
Yeah Unajua Kuna mambo kuyaeleza inabidi moyp pia ukubali kuyatetea na kuyatunza yasiharibiwa na maana za nje...

Kwahyo inakuwaga ni ngumu sana kuwasilisha mambo yanayogusa Hisia Kwa lugha ya Nyepesi ya kueleweka ambayo watu wanaweza kuelewa pasina kujicontradicts....
Wenzako wanakupinga kwa sababu chanzo cha taarifa zao ni Biblia. Wewe chanzo cha taarifa yako ni kipi??
 
Wenzako wanakupinga kwa sababu chanzo cha taarifa zao ni Biblia. Wewe chanzo cha taarifa yako ni kipi??
Kama umesoma Bandiko lote Nafikiri Kila chanzo Kimeandikwa Labda kama hujasoma andiko nililoandika..

Na kuhusu Biblia Ulitaka Kujua Nini Kuhusu Hicho
 
Man Jau

NAOMBA ufafanuzi hapo kwenye maneno Yako,

"Kwa mkristo sadaka ilishatolewa moja ya pekee, ambayo ni Yesu Kristo, yeye anakupa ufalme wote wa mbinguni, na mamlaka ya kufanywa kuwa Mwana wa Mungu, Kuhani (au kwa lugha ya sasa, Balozi/Diplomat wa ufalme wa (au serikali ya) Mbinguni, Hii unakuwa na free pass ya kwenda mbinguni hata kama una dhambi, (maana ushakua Balozi, so, serikali inakua inakumiliki), ila pia vigezo na masharti kuzingatiwa.."

Swali langu,
Kwa mwamini aliye na Yesu kristo maishani,

Je, anaweza pokelewa mbinguni ,hata Kama alikuwa na maisha ya dhambi ?
 
Nataka kujua je unaziamini Biblia na Quran?kama auziamini Je ni kwann hauziamini, na Je imani yako iko katika upande upi wa quran ama iyo Biblia?
Swala La Imani liko Very Tricky sana!
Lets stands with Facts!
And not Believe!..

Mimi nasoma Vitabu Vyote Quran,Bhagavad Gita,Biblia,The Vedas,The tripitaka, The Anunaki, The Epic of Gilgamesh,The Atrahasis...And All the So called Holly Book you name them!

Ila swala La Kuviamini au Kutokuviamini Bado linabaki so tricky
 
Why is it tricky, baada ya hoja yako ya msingi nataka kufahamu unaamini kwenye imani ipi?
 
Msidanganywe Wala msidanganyike.

1. Yesu Alikuwa kama Binadamu yoyote wa KAWAIDA.
Baba mzazi wake wamjua? kama wasema alikuwa Binadamu wa kawaida hebu tutajie!
Alipotea mbele ya Baba yake na Mama yake wakiwa sokoni
Akaja kuonekana akiwa kwenye Nyumba ya Baba kanisa.
Kanisa hayakuwepo enzi za Yesu. Je unashuhudia uongo mbele yetu wana wa jf?
Hata alipofanya Muujiza kana alimwambia mamayake kuwa wakati wake Bado haujafika

2. Yesu aliendelea kukua zaidi na zaidi Katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu. Luke 2 52.

Aliendelea kumsaidia baba yake Katika kazi za uselemala, kuchonga mbao, ufugaji nk.
Rejea Amepataje kujua kusoma huyo mtoto wa Selemala.
Kasome historia ya wayahudi vizuri... Kusoma kwao utotoni ni lazima.. hadi leo hii waliitwa watu wa kitabu miaka yao yote
3. Alianza kuifanya kazi ylaliyotumwa na Baba yake akiwa na Umri wa MIAKA 30-33.

TAFADHALI SANA MSIPOTOSHE UKWELI.
 
Why is it tricky, baada ya hoja yako ya msingi nataka kufahamu unaamini kwenye imani ipi?
Ni Tricky na Kama NikimQuote Richard Feynman Mwanafizikia Aliwahi kusema kitu kimoja...

"The problem is not people being uneducated. The problem is that they are just educated enough to believe what they've been taught, but not educated enough to question what they've been taught."

Au Kwa kiswahili..

"Tatizo si watu kuelimika. Tatizo ni kwamba wameelimika vya kutosha kuamini kile walichofundishwa, lakini hawana elimu ya kutosha kuhoji walichofundishwa"

Sasa kama Utaniwia Radhi niambie nini maana Ya Imani ambayo umeing'ang'ania Kuniuliza..?
Na nini maana Ya swali lako..?..

Na nikitaja Imani Yangu Itabadilisha Nini? ...
Au Itakuongezea Ujinga (Ujinga sio tusi) na Kuprove Failure Hypothesis yako ambayo umejitengenezea Kichwani kwamba Kama Ni wa Imani fulani bhasi huyu Kapotea...?

Au kama ni wa Imani fulani Bhasi huyu ni kawaida?

Kwanini Nyinyi kwa Nyinyi Mnawekeana Matabaka?
Vipi Nikikwambia Ni Muislamu Itabdili Facts na Hoja Zangu? Nikikwambia Mkristo itabatilisha Nilichoandika?....

Nikikwambia Mimi Ni Mhindu au Mbudha Utafikiri Nini kuhusu hilo?

Nikisema Ni Mpagani,Sina Dini au Ni msamaria Utaniona Mkosaji kw Kusema Maneno Hayo?

Tujifunze kujibu HOja iliyopo Mezani with Open Mind..
 
Pamoja na kua na arguments nzuri sana naona bado hapa kuna mahali umekosea, yani pasipo hata kujua mimi ni wa mtazamo upi, umesha conclude kua mimi ni mtu wa imani(iwe budha, Hindu, Christian, Muslim etc) na kwamba ukinijibu kama haupo katika imani yangu yani (iwe budha, Hindu, Christian, Muslim etc) basi nitakuambia umepotea. Kwa maana iyo hapo hata tungeendelea na mjadala kuna uwezekano majibu yako kwangu yangekua yanatoka ukiwa na perception ya kua mimi ni mtu imani na dini fulani.

Bro una hoja nzuri, ila epuka kua na majibu ya mtu while you are not in his mind, ni hivi binafsi watu wa imani wote uwa naona ni kama wako katika boksi lilofungwa wasione kweli ipi iko nje ya boksi ilo. Na wala uwa sioni kua wamekosea kuwepo katika imani zao maana wengi wao walizaliwa na kukuta familia na wazazi wakiziishi imani hizo na wao wakajikuta wakiishi humo hadi mbegu zilizopandwa za iyo imani zikamea ndani yao, na wala hawakutaka kuhoji imani hizo. So naami its a matter of time kwa wao kuja kufahamu mengine iwapo wataruhusu kutoka ndani ya boksi ilo. Msingi wa swali langu ulikuja baada sehemu fulani kuona umeelezea jambo kana kwamba u mtu wa imani fulani.

Anyway, thanks bro.
 
I am always standing to be Corrected!..
Nimepokea Marekebisho..

Nilifanikia Kujua Baadhi ya Imani ukiona Nimeandika kama wa Imani fulani bhasi ujue Imani Nyinginr imejaribu kuonyesha Utofauti na Hali ilivyo..

Always natetea Ukweli No.matter upo kwenye Imani gani...

Na ndo Maana Mimi Ni Mixed Conversative..Unaweza nikuta Kwenye Jews,Islam,Xtian etc
 
Vyazo ni vingi sana tatizo wengi huzani Spiritual knowledge inachanzo kimoja tuu na ncho kitabu cha dini yake. Kama mkristu anzani ni Biblia au kama Muislam basi ni Koran. Lengo ni kumjua na kumfuata Mungu basi soma vitabu vyote. Soma Biblia, Koran, Hindu Scriptures, Bavgad Gita, Upanishad, The Sufis, The true Scriptures na vitabu vingi vya philosophy. Lengo ni kufika kwa Mungu kwa njia yeyote ile udijali kichochoro ulichotumia. Kwa experience yangu hata vitabu sio jibu sahihi ya kupata elimu ya uungu (God's knowledge)ni motisha tuu. Njia sahihi ni Meditation na Contemplation ili kupata inner spiritual knowledge (elimu ya Rohoni). Any way swali lako ni what is my source?. Ni research niliyofanya juu ya dini na Cults mbalimbali. Kwenye mafunzo yangu ya Yoga na Meditation kwa zaidi ya miaka 40. Buddas na Monkis wanajua sana historia ya Yeshua of Nazzareth (Yesu) kwani ndio walimfundisha elimu ya uungu na kufanya miujiza ndio wale wakiitwa Mamajusi kwenye Biblia.
Mkuu kuna kitabu chochote unachokijua kinachohusu maisha ya Yesu?

Kuna kimoja kinaitwa Jesus live in india, nimejaribu kukitafuta sana nimekikosa

Kama utakuwa unakifaham chengine 🙏
 
Back
Top Bottom