Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Wewe umegundua nini? Hebu tuelezee ulichogundua..ni kama unakitu hivi unataka kusema kuhusu hyo lost life of Jesus ila umebaki pending..
Nimekwisha andika mkuu unaweza ukapitia andiko
 
Unachanganya mambo, mengine keeli, mengine ya kubumba.

Source yako ni nini??
Vyazo ni vingi sana tatizo wengi huzani Spiritual knowledge inachanzo kimoja tuu na ncho kitabu cha dini yake. Kama mkristu anzani ni Biblia au kama Muislam basi ni Koran. Lengo ni kumjua na kumfuata Mungu basi soma vitabu vyote. Soma Biblia, Koran, Hindu Scriptures, Bavgad Gita, Upanishad, The Sufis, The true Scriptures na vitabu vingi vya philosophy. Lengo ni kufika kwa Mungu kwa njia yeyote ile udijali kichochoro ulichotumia. Kwa experience yangu hata vitabu sio jibu sahihi ya kupata elimu ya uungu (God's knowledge)ni motisha tuu. Njia sahihi ni Meditation na Contemplation ili kupata inner spiritual knowledge (elimu ya Rohoni). Any way swali lako ni what is my source?. Ni research niliyofanya juu ya dini na Cults mbalimbali. Kwenye mafunzo yangu ya Yoga na Meditation kwa zaidi ya miaka 40. Buddas na Monkis wanajua sana historia ya Yeshua of Nazzareth (Yesu) kwani ndio walimfundisha elimu ya uungu na kufanya miujiza ndio wale wakiitwa Mamajusi kwenye Biblia.
 
Sasa, haya MA theory yanatusaidia mini kwenye karne ya 21! Hayatatui shida za foleni na usafiri Dar, hayaleti mapinduzi kwenye kilimo, na sayansi! Hayaleti ajira,wala huduma Bora za afya, dini zilianza miaka 2000 iliyopita! Walioandika hii biblia,wametafsiri kutoka lugha mama ya kipindi hicho, na kuna makosa kibao wamefanya, ungekuwa unaleta vifungu kutoka lugha mama, angalau!
 
Hivi vitu taabu yake watu hatupendi kuvichimba mpaka ndani. Mfano saayansi, ukiichimba mpaka ndani kabisaaa, itakupeleka kwenye njia mbili.

1. Ukubali kuwa Mungu yupo
2. Uamini kuwa hakuna Mungu

Na hata ukikazana kwenye namba mbili, hautokaa upate majibu milele, zaidi ya kujidanganya.

Na namba moja nayo pia usipokua makini utasema kua Mungu naye katokea wapi, na Mungu wake nae katokea wapi, na kadhalika na kadhalika, mwishowe utajitengenezea ile paradox isioisha.


Meditation ukizifanya, uwe makini sana, zinaweza kukupa kifo cha kiroho, na hiki ni kibaya sana, maana ni cha milele.

Falsafa nayo ukiichinguza kwa undani inakupeleka kwenye spiritual realms and ideologies zilezile zinazoendana na meditations, ambazo unakuwa tuu unaingia kwenye ulimwengu wa kiroho kama kwenye dini. Changamoto ya hizi meditation unakuwa kiumbe huru katika ulimwengu wa kiroho, (independent) pasipo uangalizi (protection) ya mtu au kitu au jambo au spirit yoyote ile.

Kwa mfano, Dini ya kikristo unaweza fanya meditation kwa msaada wa Roho Mtakatifu, na ukaiona Mbingu, ukaona hata Kuzimu, ukaona nyota na sayari, as long as unatii na kufuata vile Roho wa Mungu anavyokuongoza, na kutumika katika ufalme wake.

Kwa wachawi, unaweza pia kufanya utawala wa ulimwengu wa roho, (lakini nadhani hawa wanatumiaga nishati nyingi sana, na nguvu yao ni ya kuwa inaishiaga hapahapa duniani)

Kwa waislamu, sina uhakika, kwa sababu mimi sio muislamu, na sijachunguza kwa undani zaidi.

Ila kwa wakristo najua, na inawezekana, na huko kote unakua na ulinzi wa Roho mtakatifu na Utiisho wa Malaika wa BWANA wanakulinda katika ulimwengu wa roho.


Sasa inshu sio kumjua Mungu na kumkaribia, maana wengine wanajiita Mungu lakini ni miungu, na wanavaa sifa na utukufu ili wainuliwe juu, na wameshajitengenezea mifumo yap ya kuabudiwa kama Mungu mwenyewe, lakini gharama zake sasa za kuwatumikia ndio zinakukosti sana, mf. Sadaka za damu, nyama na fedha, mali, maagano, n.k.


Kwa mkristo sadaka ilishatolewa moja ya pekee, ambayo ni Yesu Kristo, yeye anakupa ufalme wote wa mbinguni, na mamlaka ya kufanywa kuwa Mwana wa Mungu, Kuhani (au kwa lugha ya sasa, Balozi/Diplomat wa ufalme wa (au serikali ya) Mbinguni, Hii unakuwa na free pass ya kwenda mbinguni hata kama una dhambi, (maana ushakua Balozi, so, serikali inakua inakumiliki), ila pia vigezo na masharti kuzingatiwa..

Nadhani nimeenda mbali sana, nisamehe, ila i hope nimeeleweka japo kidogo
 
Wenzako wanakupinga kwa sababu chanzo cha taarifa zao ni Biblia. Wewe chanzo cha taarifa yako ni kipi??
 
Wenzako wanakupinga kwa sababu chanzo cha taarifa zao ni Biblia. Wewe chanzo cha taarifa yako ni kipi??
Kama umesoma Bandiko lote Nafikiri Kila chanzo Kimeandikwa Labda kama hujasoma andiko nililoandika..

Na kuhusu Biblia Ulitaka Kujua Nini Kuhusu Hicho
 
Man Jau

NAOMBA ufafanuzi hapo kwenye maneno Yako,

"Kwa mkristo sadaka ilishatolewa moja ya pekee, ambayo ni Yesu Kristo, yeye anakupa ufalme wote wa mbinguni, na mamlaka ya kufanywa kuwa Mwana wa Mungu, Kuhani (au kwa lugha ya sasa, Balozi/Diplomat wa ufalme wa (au serikali ya) Mbinguni, Hii unakuwa na free pass ya kwenda mbinguni hata kama una dhambi, (maana ushakua Balozi, so, serikali inakua inakumiliki), ila pia vigezo na masharti kuzingatiwa.."

Swali langu,
Kwa mwamini aliye na Yesu kristo maishani,

Je, anaweza pokelewa mbinguni ,hata Kama alikuwa na maisha ya dhambi ?
 
Nataka kujua je unaziamini Biblia na Quran?kama auziamini Je ni kwann hauziamini, na Je imani yako iko katika upande upi wa quran ama iyo Biblia?
Swala La Imani liko Very Tricky sana!
Lets stands with Facts!
And not Believe!..

Mimi nasoma Vitabu Vyote Quran,Bhagavad Gita,Biblia,The Vedas,The tripitaka, The Anunaki, The Epic of Gilgamesh,The Atrahasis...And All the So called Holly Book you name them!

Ila swala La Kuviamini au Kutokuviamini Bado linabaki so tricky
 
Why is it tricky, baada ya hoja yako ya msingi nataka kufahamu unaamini kwenye imani ipi?
 
Msidanganywe Wala msidanganyike.

1. Yesu Alikuwa kama Binadamu yoyote wa KAWAIDA.
Baba mzazi wake wamjua? kama wasema alikuwa Binadamu wa kawaida hebu tutajie!
Alipotea mbele ya Baba yake na Mama yake wakiwa sokoni
Akaja kuonekana akiwa kwenye Nyumba ya Baba kanisa.
Kanisa hayakuwepo enzi za Yesu. Je unashuhudia uongo mbele yetu wana wa jf?
Kasome historia ya wayahudi vizuri... Kusoma kwao utotoni ni lazima.. hadi leo hii waliitwa watu wa kitabu miaka yao yote
3. Alianza kuifanya kazi ylaliyotumwa na Baba yake akiwa na Umri wa MIAKA 30-33.

TAFADHALI SANA MSIPOTOSHE UKWELI.
 
Why is it tricky, baada ya hoja yako ya msingi nataka kufahamu unaamini kwenye imani ipi?
Ni Tricky na Kama NikimQuote Richard Feynman Mwanafizikia Aliwahi kusema kitu kimoja...

"The problem is not people being uneducated. The problem is that they are just educated enough to believe what they've been taught, but not educated enough to question what they've been taught."


Au Kwa kiswahili..

"Tatizo si watu kuelimika. Tatizo ni kwamba wameelimika vya kutosha kuamini kile walichofundishwa, lakini hawana elimu ya kutosha kuhoji walichofundishwa"

Sasa kama Utaniwia Radhi niambie nini maana Ya Imani ambayo umeing'ang'ania Kuniuliza..?
Na nini maana Ya swali lako..?..

Na nikitaja Imani Yangu Itabadilisha Nini? ...
Au Itakuongezea Ujinga (Ujinga sio tusi) na Kuprove Failure Hypothesis yako ambayo umejitengenezea Kichwani kwamba Kama Ni wa Imani fulani bhasi huyu Kapotea...?

Au kama ni wa Imani fulani Bhasi huyu ni kawaida?

Kwanini Nyinyi kwa Nyinyi Mnawekeana Matabaka?
Vipi Nikikwambia Ni Muislamu Itabdili Facts na Hoja Zangu? Nikikwambia Mkristo itabatilisha Nilichoandika?....

Nikikwambia Mimi Ni Mhindu au Mbudha Utafikiri Nini kuhusu hilo?

Nikisema Ni Mpagani,Sina Dini au Ni msamaria Utaniona Mkosaji kw Kusema Maneno Hayo?

Tujifunze kujibu HOja iliyopo Mezani with Open Mind..
 
Pamoja na kua na arguments nzuri sana naona bado hapa kuna mahali umekosea, yani pasipo hata kujua mimi ni wa mtazamo upi, umesha conclude kua mimi ni mtu wa imani(iwe budha, Hindu, Christian, Muslim etc) na kwamba ukinijibu kama haupo katika imani yangu yani (iwe budha, Hindu, Christian, Muslim etc) basi nitakuambia umepotea. Kwa maana iyo hapo hata tungeendelea na mjadala kuna uwezekano majibu yako kwangu yangekua yanatoka ukiwa na perception ya kua mimi ni mtu imani na dini fulani.

Bro una hoja nzuri, ila epuka kua na majibu ya mtu while you are not in his mind, ni hivi binafsi watu wa imani wote uwa naona ni kama wako katika boksi lilofungwa wasione kweli ipi iko nje ya boksi ilo. Na wala uwa sioni kua wamekosea kuwepo katika imani zao maana wengi wao walizaliwa na kukuta familia na wazazi wakiziishi imani hizo na wao wakajikuta wakiishi humo hadi mbegu zilizopandwa za iyo imani zikamea ndani yao, na wala hawakutaka kuhoji imani hizo. So naami its a matter of time kwa wao kuja kufahamu mengine iwapo wataruhusu kutoka ndani ya boksi ilo. Msingi wa swali langu ulikuja baada sehemu fulani kuona umeelezea jambo kana kwamba u mtu wa imani fulani.

Anyway, thanks bro.
 
I am always standing to be Corrected!..
Nimepokea Marekebisho..

Nilifanikia Kujua Baadhi ya Imani ukiona Nimeandika kama wa Imani fulani bhasi ujue Imani Nyinginr imejaribu kuonyesha Utofauti na Hali ilivyo..

Always natetea Ukweli No.matter upo kwenye Imani gani...

Na ndo Maana Mimi Ni Mixed Conversative..Unaweza nikuta Kwenye Jews,Islam,Xtian etc
 
Mkuu kuna kitabu chochote unachokijua kinachohusu maisha ya Yesu?

Kuna kimoja kinaitwa Jesus live in india, nimejaribu kukitafuta sana nimekikosa

Kama utakuwa unakifaham chengine 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…