Miaka 25 bila Nyerere: Alikuwa Mjamaa. Je, tunamuenzi kwa vitendo na kumuishi, au ni kwa maneno matupu lakini matendo ni tofauti?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Leo tunaadhimisha miaka 25 bila ya Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maadhimisho rasmi Silver Jubilee yanaendelea kule kijijini kwake Butiama, swali ni "Kwa Miaka hii 25 Bila Nyerere, kwa vile Nyerere alikuwa mjamaa wa kweli, je sisi Watanzania, tunamuenzi kwa dhati kwa vitendo vya kijamaa, na kumuishi , au ni tunamuenzi kwa maneno matupu ya Ujamaa, lakini matendo yetu ni tofauti kabisa ya kibepari?

October 14 ya Kila Mwaka ni Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, yaani Nyerere Day. Siku hii kitaifa huadhimishwa kwa kuzima Mwenge wa Uhuru, kama moja ya namna ya kumuenzi muasisi wa Taifa letu, natoa wito kwa viongozi wetu, tusiishie kumuenzi Nyerere kwa ishara tuu na matukio, bali tuenzi fikra zake, maneno yake, matendo yake na ikibidi kumuishi kwa kumuenzi kwa vitendo na sio kumuenzi kwa maneno matupu.

Makala hii, nitakuwekea baadhi ya nukuu muhimu katika baadhi ya hotuba za Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake kisha tutafakari kwa pamoja kama kweli Watanzania tunamuenzi Baba wa Taifa letu kwa vitendo au ni tunamuenzi kwa maneno tuu, lakini kwa vitendo ni tofauti?.

Kwa vile makala hizi, zinajikita zaidi kwenye mambo ya kikatiba na kisheria, ila mara moja moja tutajikita kwenye issues za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Sifa kuu ya Mwalimu Nyerere alikuwa ni Mjamaa halisi, aliamini kwenye falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kiukweli aliishi kijamaa kabisa, ukiondoa nyumba yake ya Msasani aliyojengewa na Serikali, na ile ya Magomeni aliyojengewa na Amiri Jamal. Miaka yake yote 23 ya urais wa Tanzania, hakuwa na mali yoyote, hata ile nyumba yake ya kijijini kwake kule Mwitongo, Butiama, ile nyumba ni amejengewa na Jeshi.

Leo kwenye viongozi wetu, ni kiongozi gani ni mjamaa?. Ni kiongozi gani ana muishi Mwalimu Nyerere kwa vitendo?, hivyo tunamenzi Nyerere kwa maneno tuu, lakini matendo ni tofauti?.

Ibara ya 3.-(1) ya katiba yetu ya mwaka 1977 inasema “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Je ni kweli Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ya kijamaa?. Bado tuna fuata misingi ya siasa ya Ujamaa na kujitegemea?.

Siasa hii ya ujamaa na kujitegemea, ililetwa na Azimio la Arusha, ambalo pia liliweka misingi ya uongozi. Azimio la Arusha tumeisha liua na kulizika, sasa Tanzania inafuata misingi ya uchumi wa soko, (market economy), hivyo maneno ujamaa kwenye katiba yetu ni maneno tuu, lakini vitendo ni vya kibebari!.

Viongozi wetu, wanaingia kwenye uongozi wakiwa wa kawaida, lakini wakati wanaondoka, wanaondoka wakiwa ni mabepari wakubwa!. Huku ndiko kumuenzi kweli Mwalimu Nyerere?

Mwalimu Nyerere alisimamia katiba ya Tanzania na kuweka misingi mikuu mine ya katiba, Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.

Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.

Je, viongozi wetu wa sasa, wanadumisha haki zote za binadamu?, katiba yetu imetoa haki mbalimbali za msingi, ikiwemo haki ya kuchagua na kuchaguliwa, laki sasa haki hiuo imeporwa, ili mtu uchaguliwe, unalazimishwa lazima ujiunge na chama cha siasa!. Badala ya wananchi kuwa huru kuwachagua viongozi wanaowataka, vyama vya siasa ndio vinatuchagulia viongozi!.

Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.

Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.

Mwalimu aliamini kwenye kukosoa na kukosolewa ni wajibu wa kila mwananchi na kila Kiongozi wa Taifa hili ili viongozi wetu wajisahihishe makosa ambayo wanayafanya na huwezi kuwa Kiongozi bora kama unakataa kukosolewa. Jee viongozi wetu wa sasa wako tayari kukosolewa?.

Mwalimu Nyerere aliamini kwenye Umoja wa Taifa letu haujashushwa toka mbinguni, bali tumeujenga kwa kipindi kirefu sana, kwa hiyo watanzania tusijidanganye kuwa Umoja huo utaendelea kudumu hata kama misingi ya Umoja wetu tunaibomoa, ni lazima tutengeneze mazingira ambayo Umoja wetu utaendelea kudumu na nguzo kuu ya kudumisha Umoja wetu ni kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa letu wanatende haki kwa makundi yote ya kijamii.

Mwalimu aliamini Cheo ni dhamana, kwa hiyo viongozi wetu tunaowachagua ni lazima walijue hilo kuwa tunapowapa dhamana ya uongozi tunakuwa tumewapa dhamana ya wao kuwa watumishi wa kututumikia, viongozi wetu wa leo, wangapi wanajina ni mungu watu?

Mwalimu alisema tunamchagua Rais ambaye anapaswa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu siku tunamuapisha kuliongoza Taifa letu. Iwapo tutakuwa na Rais ambaye hataki kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu, Rais wa aina hiyo hatufai, Nyerere alisema “Ni bora rais huyo akatuachia Urais wetu na yeye aende kufanya shughuli zake nyingine”, leo viongozi wetu wa sasa ni mara ngapi wanatoa maamuzi kinyume na katiba?

Nimalizie kwa wito wa makala hii nikiwasisitiza Viongozi wetu, tumuenzi Mwalimu kwa vitendo kwa kumuishi na sio kwa maneno matupu na vitendo tofauti.

Asante Mungu kwa Nyerere, Tunakuomba wawezeshe viongozi wetu wamuishi kwa vitendo na sio kwa maneno tu.

Happy Nyerere Day.
Paskali.
 
Viongozi wetu, wanaingia kwenye uongozi wakiwa wa kawaida, lakini wakati wanaondoka, wanaondoka wakiwa ni mabepari wakubwa!. Huku ndiko kumuenzi kweli Mwalimu Nyerere?.

Mwalimu Nyerere alisimamia katiba ya Tanzania na kuweka misingi mikuu mine ya katiba, Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.

Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.

Je viongozi wetu wa sasa, wanadumisha haki zote za binadamu?, katiba yetu imetoa haki mbalimbali za msingi, ikiwemo haki ya kuchagua na kuchaguliwa, laki sasa haki hiuo imeporwa, ili mtu uchaguliwe, unalazimishwa lazima ujiunge na chama cha siasa!. Badala ya wananchi kuwa huru kuwachagua viongozi wanaowataka, vyama vya siasa ndio vinatuchagulia viongozi!.

Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.

Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.

Mwalimu aliamini kwenye kukosoa na kukosolewa ni wajibu wa kila mwananchi na kila Kiongozi wa Taifa hili ili viongozi wetu wajisahihishe makosa ambayo wanayafanya na huwezi kuwa Kiongozi bora kama unakataa kukosolewa. Jee viongozi wetu wa sasa wako tayari kukosolewa?.

Mwalimu Nyerere aliamini kwenye Umoja wa Taifa letu haujashushwa toka mbinguni, bali tumeujenga kwa kipindi kirefu sana, kwa hiyo watanzania tusijidanganye kuwa Umoja huo utaendelea kudumu hata kama misingi ya Umoja wetu tunaibomoa, ni lazima tutengeneze mazingira ambayo Umoja wetu utaendelea kudumu na nguzo kuu ya kudumisha Umoja wetu ni kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa letu wanatende haki kwa makundi yote ya kijamii.

Mwalimu aliamini Cheo ni dhamana, kwa hiyo viongozi wetu tunaowachagua ni lazima walijue hilo kuwa tunapowapa dhamana ya uongozi tunakuwa tumewapa dhamana ya wao kuwa watumishi wa kututumikia, viongozi wetu wa leo, wangapi wanajina ni mungu watu?.

Mwalimu alisema tunamchagua Rais ambaye anapaswa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu siku tunamuapisha kuliongoza Taifa letu. Iwapo tutakuwa na Rais ambaye hataki kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu, Rais wa aina hiyo hatufai, Nyerere alisema “Ni bora rais huyo akatuachia Urais wetu na yeye aende kufanya shughuli zake nyingine”, leo viongozi wetu wa sasa ni mara ngapi wanatoa maamuzi kinyume na katiba?.

Nimalizie kwa wito wa makala hii nikiwasisitiza Viongozi wetu, tumuenzi Mwalimu kwa vitendo kwa kumuishi na sio kwa maneno matupu na vitendo tofauti.

Asante Mungu kwa Nyerere, Tunakuomba wawezeshe viongozi wetu wamuishi kwa vitendo na sio kwa maneno tuu.

Happy Nyerere Day.
Paskali.
Kama Ardhi na Mbingu 🙄 !
 
Azimio la Arusha lilizikwa na azimio la Zanzibar

Lengo kuu ni kufaidi keki ya taifa kwa kikundi kidogo cha watu peke yao

Tatizo kubwa lingine ni sisi wananchi kubaki watazamaji pasipo kuchukua hatua kwa yale ambayo viongozi wanapovunja Sheria na katiba
 
Wanabodi,

Leo tunaadhimisha miaka 25 bila ya Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maadhimisho rasmi Silver Jubilee yanaendelea kule kijijini kwake Butiama, swali ni "Kwa Miaka hii 25 Bila Nyerere, kwa vile Nyerere alikuwa mjamaa wa kweli, je sisi Watanzania, tunamuenzi kwa dhati kwa vitendo vya kijamaa, na kumuishi , au ni tunamuenzi kwa maneno matupu ya Ujamaa, lakini matendo yetu ni tofauti kabisa ya kibepari?

October 14 ya Kila Mwaka ni Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, yaani Nyerere Day. Siku hii kitaifa huadhimishwa kwa kuzima Mwenge wa Uhuru, kama moja ya namna ya kumuenzi muasisi wa Taifa letu, natoa wito kwa viongozi wetu, tusiishie kumuenzi Nyerere kwa ishara tuu na matukio, bali tuenzi fikra zake, maneno yake, matendo yake na ikibidi kumuishi kwa kumuenzi kwa vitendo na sio kumuenzi kwa maneno matupu.

Makala hii, nitakuwekea baadhi ya nukuu muhimu katika baadhi ya hotuba za Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake kisha tutafakari kwa pamoja kama kweli Watanzania tunamuenzi Baba wa Taifa letu kwa vitendo au ni tunamuenzi kwa maneno tuu, lakini kwa vitendo ni tofauti?.

Kwa vile makala hizi, zinajikita zaidi kwenye mambo ya kikatiba na kisheria, ila mara moja moja tutajikita kwenye issues za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Sifa kuu ya Mwalimu Nyerere alikuwa ni Mjamaa halisi, aliamini kwenye falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea, na kiukweli aliishi kijamaa kabisa, ukiondoa nyumba yake ya Msasani aliyojengewa na Serikali, na ile ya Magomeni aliyojengewa na Amiri Jamal. Miaka yake yote 23 ya urais wa Tanzania, hakuwa na mali yoyote, hata ile nyumba yake ya kijijini kwake kule Mwitongo, Butiama, ile nyumba ni amejengewa na Jeshi.

Leo kwenye viongozi wetu, ni kiongozi gani ni mjamaa?. Ni kiongozi gani ana muishi Mwalimu Nyerere kwa vitendo?, hivyo tunamenzi Nyerere kwa maneno tuu, lakini matendo ni tofauti?.

Ibara ya 3.-(1) ya katiba yetu ya mwaka 1977 inasema “Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Je ni kweli Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ya kijamaa?. Bado tuna fuata misingi ya siasa ya Ujamaa na kujitegemea?.

Siasa hii ya ujamaa na kujitegemea, ililetwa na Azimio la Arusha, ambalo pia liliweka misingi ya uongozi. Azimio la Arusha tumeisha liua na kulizika, sasa Tanzania inafuata misingi ya uchumi wa soko, (market economy), hivyo maneno ujamaa kwenye katiba yetu ni maneno tuu, lakini vitendo ni vya kibebari!.

Viongozi wetu, wanaingia kwenye uongozi wakiwa wa kawaida, lakini wakati wanaondoka, wanaondoka wakiwa ni mabepari wakubwa!. Huku ndiko kumuenzi kweli Mwalimu Nyerere?

Mwalimu Nyerere alisimamia katiba ya Tanzania na kuweka misingi mikuu mine ya katiba, Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.

Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.

Je, viongozi wetu wa sasa, wanadumisha haki zote za binadamu?, katiba yetu imetoa haki mbalimbali za msingi, ikiwemo haki ya kuchagua na kuchaguliwa, laki sasa haki hiuo imeporwa, ili mtu uchaguliwe, unalazimishwa lazima ujiunge na chama cha siasa!. Badala ya wananchi kuwa huru kuwachagua viongozi wanaowataka, vyama vya siasa ndio vinatuchagulia viongozi!.

Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.

Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.

Mwalimu aliamini kwenye kukosoa na kukosolewa ni wajibu wa kila mwananchi na kila Kiongozi wa Taifa hili ili viongozi wetu wajisahihishe makosa ambayo wanayafanya na huwezi kuwa Kiongozi bora kama unakataa kukosolewa. Jee viongozi wetu wa sasa wako tayari kukosolewa?.

Mwalimu Nyerere aliamini kwenye Umoja wa Taifa letu haujashushwa toka mbinguni, bali tumeujenga kwa kipindi kirefu sana, kwa hiyo watanzania tusijidanganye kuwa Umoja huo utaendelea kudumu hata kama misingi ya Umoja wetu tunaibomoa, ni lazima tutengeneze mazingira ambayo Umoja wetu utaendelea kudumu na nguzo kuu ya kudumisha Umoja wetu ni kwa viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuliongoza Taifa letu wanatende haki kwa makundi yote ya kijamii.

Mwalimu aliamini Cheo ni dhamana, kwa hiyo viongozi wetu tunaowachagua ni lazima walijue hilo kuwa tunapowapa dhamana ya uongozi tunakuwa tumewapa dhamana ya wao kuwa watumishi wa kututumikia, viongozi wetu wa leo, wangapi wanajina ni mungu watu?

Mwalimu alisema tunamchagua Rais ambaye anapaswa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu siku tunamuapisha kuliongoza Taifa letu. Iwapo tutakuwa na Rais ambaye hataki kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu, Rais wa aina hiyo hatufai, Nyerere alisema “Ni bora rais huyo akatuachia Urais wetu na yeye aende kufanya shughuli zake nyingine”, leo viongozi wetu wa sasa ni mara ngapi wanatoa maamuzi kinyume na katiba?

Nimalizie kwa wito wa makala hii nikiwasisitiza Viongozi wetu, tumuenzi Mwalimu kwa vitendo kwa kumuishi na sio kwa maneno matupu na vitendo tofauti.

Asante Mungu kwa Nyerere, Tunakuomba wawezeshe viongozi wetu wamuishi kwa vitendo na sio kwa maneno tu.

Happy Nyerere Day.
Paskali.
Paskal, Mwalimu ni mwalimu hata madaraka Nyerere hawezi kuwa kama Mwalimu
 
Baadhi ya mabaya au ubovu wa Mwl. Nyerere:-
1. Kuiga, Kuanzisha na kuendeleza Sera na Itikadi Mbaya kabisa ya Siasa za Ukomunisti/Ujamaa hapa Tanzania.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kujenga Msingi mbovu wa Taifa la hovyo kabisa lililopo hivi sasa.
Itikadi na Sera ya Ukomunisti/Ujamaa ikaja kushindwa vibaya Sana huku yeye mwenyewe akishuhudia kwa macho yake kushindwa kwa itikadi yake aliyoileta hapa Tanzania kutoka kwa marafiki zake wa China, Urusi na Cuba.

2. Kutengeneza Taifa la Watu waoga, Wanyonge, dhaifu wa fikra wasiojitambua na Wala wasioweza kuhoji. Taifa la watu 'misukule'.

3. Kutengeneza au kuunda nchi isiyokuwa na Mipango-miji, hususani kupitia kwenye Sera yake mbaya kabisa ya ujamaa/Ukomunisti. Sera au Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti ndio ilikuwa chanzo Cha Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, the Worse Operation that completely destroyed the Country and Town Planning process within the Country.
Arusha Declaration and Operation Vijiji also led to the Death of Real Estate Industry and its development.

Kupitia Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti, Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, Watu wengi sana walinyang'anywa Ardhi zao pamoja na majumba yao waliyokuwa wakimiliki. Nyumba nyingi sana za Watu zilitaifishwa, Leo hii nyumba hizo zinamilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC).

4. Kutuletea Katiba ya nchi ambayo ni mbaya kabisa, isiyofaa na ambayo imesababisha na inaendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa Raia. Katiba mbaya ambayo imewatengeneza Watawala wa nchi hii kuwa 'Miungu Watu.'
 
paragraph ya Nne pekee ndio iko sahihi !
 
Mkuu asante kwa mchango wako. Sina hakika kama unaweza kutuonyesha kwamba Nyerere alikuwa na nia ya kujenga Ujamaa/ Ukomunisti. Mwalimu alikuwa na dhamira ya kutufanya tuendelee kuishi kama jamaa moja- UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Nenda kwenye katiba ya Tanzania ya 1977 imeeleza wazi kusudio la kujenga jamii ya namna gani. Soma makala katika gazeti la Daily News- Tuesday October 15-21, 2024 yenye kichwa cha habari-THE WATER , CLAY THAT MADE, SHAPED MWALIMU itakusaidia
 
Back
Top Bottom