Miaka 30+ Sio Umri wa Kujaribu Kujaribu Tena, Huu ni Muda wa Kujillipua

Miaka 30+ Sio Umri wa Kujaribu Kujaribu Tena, Huu ni Muda wa Kujillipua

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Miaka 10 iliyopita nilikuwa na uwezo wa kubeba ndoo mbili kubwa za maji kama nimebeba kamzigo. Leo hii ukinipa ndoo moja hatua tano tu nasimama kupumzika kama mzee wa miaka 60.. nilikuwa nakimbia masaa mawili bila shida. Sasa nikikimbia mita 100 unajikuta unahema kama mbwa..na muda unavyokwenda kwa kasi.juzi tu tulikuwa tunasema

"Happy New Year 2026"? Leo hii tayari tupo katikati ya mwaka. Miezi inakimbia kama utani.ndo maana hata ccm wameanza hekaheka za uchaguzi 2030 wanajua muda sio mrefu mama anaondoka..2030 sio mbali hata kidogo..

Ukiwa na miaka 30 unajiona bado kijana sana. Ukweli ni kwamba ukifikiria vizuri, miaka ya kupambana kwa nguvu zote si mingi kama tunavyodhani. Ukifika 40 mwili hautakuwa na nguvu za miaka 25. Hiyo maana yake una kama miaka 10 hivi ya kusukuma gurudumu kwa kasi ya juu kabla hujaanza kusikia maumivu ya mgongo yakikusalimia kila asubuhi. kutoka 30 kudondokea 40 ni kunusa tu..

Ndio maana wakati mwingine nawaona wale wanaosema wataoa wakiwa na 40 Nawaangalia tu. Sasa wewe unategemea kufikisha 50 ndio uanze kujifunza maisha ya ndoa? Na hapa sizungumzii kuoa kwa sababu ya pressure za watu.Ninamaanisha kutambua kwamba maisha yanaenda haraka sana. Ukiumwa ukiwa peke yako ndipo utajua umuhimu wa kuwa na mtu wa karibu. Kuna wakati mtu haji maishani mwako kupunguza uhuru wako, anakuja kuongeza thamani kwenye maisha yako.Ndoa ina changamoto zake, hilo halina ubishi.

Na kuna wale wajomba zetu ambao leo wana miaka 50 hawajaoa. Ukiwauliza walikuwa na mpango gani, wanasema "Nilikuwa nasema bado mapema...Hiyo bado mapema imechukua miaka 20 bila wao kujua.

Kwa hiyo kwa vijana wa 30+, tusiogope maisha sana. Tusiwe tunasubiri kila kitu kikamilike asilimia 100. Ukisubiri uwe tajiri, uwe na nyumba , gari na maisha yasiyo na matatizo ndipo uoe, unaweza kujikuta umefikisha 55 bado unasema "muda ukifika nitaoa."Muda hauombi ruhusa ya kupita.Leo una nguvu, kesho zimepungua. Leo una miaka 30, kesho una 40. Mungu akitupa uhai, nawaombea wote wenye miaka 30 na kuendelea, mwakan muwe mmeacha kujiita "vijana wanaojipanga." Tuingie kwenye maisha yenyewe.
 
Tatizo kubwa la vijana wa sasa ni kuamini kuwa maisha ni linear process kwamba eti lazima ufike hatua A ndipo uende hatua B.

Kwenye uchumi hii tunaita opportunity cost, unapochelewa kufanya maamuzi muhimu kwa kisingizio cha kujipanga unapoteza compound interest ya maisha, yaani muda, nguvu, na nafasi ya kukua na mwenza wako.

Kufika miaka 40 ukiwa unaanza kujifunza maisha ya ndoa ni high risk gamble.

Mwili unakuwa umechoka, uvumilivu unakuwa mdogo, na mental flexibility inapungua, so deep issue ni kuacha kusubiri perfect conditions, kwa sababu maisha yenyewe hayajawahi kuwa perfect.
 
80% ya vijana wa 90th&2000th wametopea kwenye tamaa na starehe so utulivu kwao ni 0.

Bila kuwa na utulivu wa akili huwezi kuitamani ndoa na hata ukiikurupukia ndo hizi zinadumu miezi 3 zinavunjika!

Hata mimi nilipita huko nikastuka na at 33yrs nikaamua kuoa ndo mambo yangu yaka settle na sasa nakimbizana kusaka mkate na kesho bora ya wanangu.

Vijana badilikeni though maisha yapo chap lakini fursa za kiutafutaji ni nyingi tofauti na zama za wazee wetu.
Jiulize why wazee wetu walimudu kuhudumia ndoa na wakati huo wanakimbizana kutuandalia kesho yetu.
 
Mungu akitupa uhai, nawaombea wote wenye miaka 30 na kuendelea, mwakan muwe mmeacha kujiita "vijana wanaojipanga." Tuingie kwenye maisha yenyewe.
Mkuu maisha hayana formula, NDOA ina umuhimu sana ila pia sio jambo la kila mtu.

Kuna watu leo wanazeeka kwa mateso makali na sababu ya mateso yao ni NDOA, ukiwauliza kwanini mnateseka watakuambia Ndoa.

Otherwise wapo wengine wanazeeka fresh, Raha mstarehe na ukiwauliza watasema Ndoa ndio imechangia.

Vijana jambo muhimu ni kutengeneza kesho yako, jiwekee akiba ya uzeeni. Ukiwa na pesa uzeeni utapata unafuu mkubwa sana hapa Duniani. UOE au USIOE ila make sure unazeeka ukiwa na uwezo kifedha (UNAJITEGEMEA).

Be a Man, Stay taliban.
 
Tatizo kubwa la vijana wa sasa ni kuamini kuwa maisha ni linear process kwamba eti lazima ufike hatua A ndipo uende hatua B.

Kwenye uchumi hii tunaita opportunity cost, unapochelewa kufanya maamuzi muhimu kwa kisingizio cha kujipanga unapoteza compound interest ya maisha, yaani muda, nguvu, na nafasi ya kukua na mwenza wako.

Kufika miaka 40 ukiwa unaanza kujifunza maisha ya ndoa ni high risk gamble.

Mwili unakuwa umechoka, uvumilivu unakuwa mdogo, na mental flexibility inapungua, so deep issue ni kuacha kusubiri perfect conditions, kwa sababu maisha yenyewe hayajawahi kuwa perfect.
😄😄😄 hii comment imewakosha sana masingo maza na mishangazi!!!

Nasemaje hii mbugi bado ngumu sana,yaani kama inakuja ila inakataa.Ngoja tuendelee kuwachakata mpaka kieleweke.

"KAMA UNAPATA MAZIWA KWA URAHISI,YANINI UJICHOSHE KUFUGA NG'OMBE"

🚩Kataaa ndoa,kataa kuwa fala!!!
 
we naye unachuki zako binafsi zinazokutafuna tu! hapo masingo maza wameingiaje au ndio akili finyu?
 
Back
Top Bottom