Miaka 10 iliyopita nilikuwa na uwezo wa kubeba ndoo mbili kubwa za maji kama nimebeba kamzigo. Leo hii ukinipa ndoo moja hatua tano tu nasimama kupumzika kama mzee wa miaka 60.. nilikuwa nakimbia masaa mawili bila shida. Sasa nikikimbia mita 100 unajikuta unahema kama mbwa..na muda unavyokwenda kwa kasi.juzi tu tulikuwa tunasema
"Happy New Year 2026"? Leo hii tayari tupo katikati ya mwaka. Miezi inakimbia kama utani.ndo maana hata ccm wameanza hekaheka za uchaguzi 2030 wanajua muda sio mrefu mama anaondoka..2030 sio mbali hata kidogo..
Ukiwa na miaka 30 unajiona bado kijana sana. Ukweli ni kwamba ukifikiria vizuri, miaka ya kupambana kwa nguvu zote si mingi kama tunavyodhani. Ukifika 40 mwili hautakuwa na nguvu za miaka 25. Hiyo maana yake una kama miaka 10 hivi ya kusukuma gurudumu kwa kasi ya juu kabla hujaanza kusikia maumivu ya mgongo yakikusalimia kila asubuhi. kutoka 30 kudondokea 40 ni kunusa tu..
Ndio maana wakati mwingine nawaona wale wanaosema wataoa wakiwa na 40 Nawaangalia tu. Sasa wewe unategemea kufikisha 50 ndio uanze kujifunza maisha ya ndoa? Na hapa sizungumzii kuoa kwa sababu ya pressure za watu.Ninamaanisha kutambua kwamba maisha yanaenda haraka sana. Ukiumwa ukiwa peke yako ndipo utajua umuhimu wa kuwa na mtu wa karibu. Kuna wakati mtu haji maishani mwako kupunguza uhuru wako, anakuja kuongeza thamani kwenye maisha yako.Ndoa ina changamoto zake, hilo halina ubishi.
Na kuna wale wajomba zetu ambao leo wana miaka 50 hawajaoa. Ukiwauliza walikuwa na mpango gani, wanasema "Nilikuwa nasema bado mapema...Hiyo bado mapema imechukua miaka 20 bila wao kujua.
Kwa hiyo kwa vijana wa 30+, tusiogope maisha sana. Tusiwe tunasubiri kila kitu kikamilike asilimia 100. Ukisubiri uwe tajiri, uwe na nyumba , gari na maisha yasiyo na matatizo ndipo uoe, unaweza kujikuta umefikisha 55 bado unasema "muda ukifika nitaoa."Muda hauombi ruhusa ya kupita.Leo una nguvu, kesho zimepungua. Leo una miaka 30, kesho una 40. Mungu akitupa uhai, nawaombea wote wenye miaka 30 na kuendelea, mwakan muwe mmeacha kujiita "vijana wanaojipanga." Tuingie kwenye maisha yenyewe.