Miaka 30 ya Chadema, Swot Analysis, PEST Analysis, Imarisheni Strengths, Shughilikieni Weakness, Start A Fresh!.

Pale Chadema 'watapopewa nafasi' mwisho wa kunukuu
 
Ni kawaida ya Wasukuma, hata salamu usipomkatisha utauliziwa habari hadi za majirani wanaendeleaje [emoji2960]...
 
tunashkuru kaka ukichambua mim nipo karibu na wahusika nitaufikisha uchambuz wako wa kitaaalam ufanyiwe kaz maaana kwasasa ata sisi wanachama tunaona kabisa jahaz linaenda mlama na imiendelea ivi ivi kudakia matukio asee 2025 atupat diwan ata mmoja
 
Wewe unapenda haki na wewe haujutii wapinzani kusukwasukwa na jeshi la polisi na wewe huyo huyo unawashauri Chadema wajiimarishe huku ukijifanya hauna habari kuwa kila siku wanashinda mahakamani! Wewe sawa na yule mwanasheria wa Tigo aliyesema hajui kuwa mhe. Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema!
Si jambo jema kumshauri mgonjwa aliyelala kitandani jinsi ya kuimarisha biashara zake, naona kamavile unawajoki.
 
Kuanza upya na Katiba hii ya akina Mutungi, Mahera, Jecha na Sirro haitosaidia chochote. Labda kama unamaanisha kuanza upya kwa Katiba mpya.
 
Yule mwehu wa Chato alijaribu kuifuta akafutika yeye kwanza, sasa na huyu mchawi kutoka visiwa vya nchi jirani ataondoka na kuiacha imara zaidi.
 
Bwana njaa habari yako
 
Ungeishaur ccm na namna inavyotutawala hapo ningekuelewa.Huwa naenjoy kusoma article zako lkn kwenye hili nimeboreka,hata cjajua umemalizaje kuandika.
 
Ukweli ni kwamba vyama vya siasa hapa Tanzania vilianzishwa na kuasisiwa na sana CCM kutimiza matakwa ya CCM mambo mengine ni stories tu, Tundu nadhani alileta mtazamo mpya then he got what he got sidhani kama anaujasiri ule tena aliokuwa nao. So unaweza sema risasi alizopigwa Tundu ziliua future ya upinzani.
 
Comment yako imenitia simanzi from no where! Sijui why and how? Any ways thanks God for 17/3/2021.
 
Sikujua kama Pascal Ni learned brother. Kumbe anajua SWOT na PEST?
 
Mapito ya Chadema ni mengi na yapo wazi, hata sasa wapo katika mapito makubwa

Makosa ya chadema ni pamoja kuwapokea mamluki wa ccm kwa imani kubwa na kuwaruhusu kugombea nafasi za juu za uongozi pasipo kujiridhisha na nia ya ndani ya mamluki hao...hii imechangia kwa kiasi kikubwa sana kuzorota kwa chama pamoja na migogoro ya ndani iliyosababisha chama kuyumba

Uimara wa chadema ni pamoja na kupigania demokrasia,haki na uhuru bila kujali nguvu kubwa inayotumiwa na dola kuwarudisha nyuma au kuwakandamiza,viongozi wao wameumizwa, wamefilisiwa, wamefungwa, wamepitishwa kwenye mateso pamoja na familia zao lakini baadhi hawakuwahi kurudi nyuma...wanatia moyo lakini inasikitisha sana

Shida kubwa ninayoiona, wanachama wa chadema wengi ni wanachama wa mitandaoni, sio wepesi kuchukua hatua, ni wepesi kuchangia chama na kupigania chama mitandaoni, lakini wakati mwingine pesa na vita ya mitandaoni haitoshi, wamewaacha viongozi wenyewe kwenye front line, wao wapo mitandaoni kwa kiasi kikubwa, nguvu ya pamoja ingeweza kuleta tija zaidi

Kwenye udhaifu wa chadema, nizungumzie kususia shughuli zinazohusu maslahi ya taifa kwa ujumla au shughuki za kijamii mfano sherehe za uhuru, misiba ya kitaifa na mengine kama hayo, tofauti za kisera na kiitikadi zinapaswa kuwekwa pembeni tunapokua na jambo la kitaifa, ni hii ndio maana ya siasa za demokrasia

Yafaa chama kufanya tathmini ya wanachama na kuwekeza nguvu kabwa kutengeneza foundation nzuri ya wanachama wenye uthubutu au ujasiri wa kukipigania chama katika ngazi zote kwa vitendo

Chama pia kinapaswa kutafuta namna bora ya kutatua migogoro yao ya ndani pasi kuwapa faida competitors wao, migogoro ya ndani imeleta athari kubwa sana kwa chama

Chama pia kinapaswa kuwa na agenda endelevu zenye mashiko na sio kudakia agenda kutokana na matukio ya kisiasa au ya kijamii...hapo nyuma Chadema ilikua imara na ilisimamia agenda zake kikamilifu lakini kwa miaka michache ikiyopita ni kama hakuna mwelekeo mzuri jambo linalosababisha chama kukosa mvuto

Pamoja na kizuizi cha mikutano ya kisiasa ambayo imechangia chama kuzorota, bado naamini Chadema ni bora na itaendelea kuwa bora kulinganisha na vyama vingine vya siasa

Mungu ibariki chadema.
 
Yaan huyu mzee amefeli kabla hajaanza! Hapa labda tusubiri mabua lkn sio nondo! Huyu mzee ameshapitwa na wakati! Nahisi hapo anatumia wakati wa watu wengine kuishi!
 
Chama kina 30 years ofisi makao makuu kama banda ka UMBWA.
Wizi wa ruzuku kama vichaa. Hapo hakuna Kitu ni threat tu Kwa nchi

Ni kweli kukosa ofisi sio jambo zuri, ila kwa mahitaji ya kizazi hiki cua technology, ofisi suo muhimu tena kwani kila kitu kipo online. Hii sio ile ya miaka ya kwenda kupanga mistari asubuhi na mapema ili kupata huduma kwenye mabenki, TANESCO, TRA, idara ya maji, uhamiaji nk. Emails, WhatsApp, Skype, zoom nk zimeondoa mambo hayo.

Ukitaka kujua ofisi sio issue sana kwa sasa, tazama ofisi za CCM mbali ya uchakavu wake, zimegeuka kuwa vijiwe vya majobless, washirikina, wapiga Majungu nk. Na bado ikifika wakati wa uchaguzi, ccm inategemea vyombo vya dola na tume isiyo huru ya CCM ili watangazwe washindi kinyume na box la kura.
 
Umenikumbusha SWORT na PERT ulikua uwanja wangu huo enzi nafundisha mambo ya Planning!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…