Wanabodi,
Chadema imetimiza miaka 30.
Tangu ile Chadema inazaliwa miaka 30 iliyopita, imezaliwa na kunikuta mimi tayari niko newsroom kwa zaidi ya miaka 2, hivyo Chadema imezaliwa naiona, inakuwa naiona, ilipofika peak naiona, na sasa imeanza kusinyaa naiona, na ikiendelea hivi kwa mwendo huu, naiona kule inakoelekea, hivyo hili ni bandiko la ushauri, ili isifike huko ninakokuona mimi.
Hili ni bandiko la SWOT Analysis, na PEST Analysis, ya Miaka 30 ya Chadema huku nikiwashauri wa imarisheni strengths zao, na kushughughulikia weakness zao, na kama ikibidi to start afresh, Chadema is start a fresh!.
Mtu Asiye Chadema, Anaishauri Chadema Kama Nani?
Japo chama cha siasa ni mali ya wanachama, vyama vya siasa nchini Tanzania, vyenye wabunge na madiwani, ambavyo vinapokea ruzuku ya serikali, sio private parties za wanachama tuu, ni public parties za umma, paid by taxpayers money, ndio maana hesabu zake zinakaguliwa na CAG, hivyo sisi as public, mimi nikiwemo, we have all the rights to ask, know or make comments kuhusu all it's affairs, public as well as private.
Declaration of interest.
Mimi ni kada wa chama cha Mapinduzi, ila chama cha Mapinduzi kina makada wengi na wa aina nyingi na makundi mengi, kada mimi ni type impya ya makada wa CCM, tunaitwa CCM Conteporary, tunaoamini katika kutenda haki bin haki, CCM ikishinda uchaguzi, ishinde kwa haki, katika uchaguzi huru na wa haki, huku tukiamini bila upinzani imara, hakuna CCM imara.
Kiukweli kabisa Tanzania, hatuna upinzani imara, hivyo
huu ni ushauri wa bure, kwa Chadema, wa tathmini yangu ya Chadema ilipotoka, ilipo na inapokwenda, na Chadema mko huru kuusoma au kutousoma, kuuelewa au kutoelewa, kuufuata au kutoufuata, au hata kuupuuzia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu.
Ushauri huu nauweka kwenye points format huku nikionyesha nilishauri nini na nini kikatokea.
Highlights
Into ya Chadema
Chadema ile iliyokusudiwa
Mapito ya Chadema
Uimara wa Chadema
Udhaifu wa Chadema
Makosa ya Chadema
Matokeo ya makosa ya Chadema
Chadema ya Sasa
Chadema ilipo
Chadema inapokwenda
A Way Forward.
Hitimisho.
Nawaomba sasa sana sana kwa sasa, jiuzuie kadri uwezavyo msichangie chochote kwanza kwenye uzi huu hadi nondo zitakapo anza kushuka.
Natanguliza shukrani
Karibuni.
Paskali