Miaka 40 ya mageuzi ya ufunguaji mlango nchini China ni funzo kwa nchi za Afrika

Miaka 40 ya mageuzi ya ufunguaji mlango nchini China ni funzo kwa nchi za Afrika

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
1719819272136.jpeg

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Katoliki cha Kenya Profesa Becky Ndeto, amesema sera zilizotekelezwa na China baada ya kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, zimesababisha ukuaji wa uchumi usio na mfano, kuleta maendeleo ya kiteknolojia, na kupunguza umaskini.
Akiongea kwenye mahojiano maalum na shirika kuu la Utangazaji la China CMG, Profesa Ndeto pia amesema ushirikiano kati ya China na Afrika, pia umeonesha mfano wa jinsi mabadiliko ya kimkakati ya kimkakati yanavyoweza kuharakisha maendeleo. Amesema uzoefu wa China unatoa somo muhimu kwa nchi za Afrika kuhusu kutumia uwekezaji wa kigeni, maendeleo ya miundombinu na kuendeleza viwanda.
Akizungumzia kura za maoni za hivi karibu za Kampuni ya Gallup zinazoonesha uungaji mkono mkubwa wa China barani Afrika, Profesa Becky Ndeto amesema matokeo hayo sio tu yanaonesha uwepo mkubwa wa kimataifa na sura nzuri ya China katika nchi nyingi, lakini pia zinaonyesha nchi hizo kuvutiwa na utawala bora wa China, mafanikio yake kiuchumi, na juhudi za kidiplomasia zenye mafanikio za China.
 
Back
Top Bottom