Hili tumemlilia sana kuwa inawezekana alivyoambiwa sivyo, humu ameambiwa jinsi haswa ilivyo, tukamuomba basi angalau arekebisha makosa!, kagoma kata kata akiwataka walioona makosa nao watoe machapisho yao kulirekebisha andiko lake!.
hili ni andiko la kutafutwa na ikibidi mwenye nalo alimwage humu!.
Hiki ndicho kitakachofuatia baada ya uzi huu, uandishi wa kitabu ni kipaji, sisi wengine tumejaaliwa critique tuu na sio kuandika.
Hili nimekubali siku nyingi ila Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni class strungle kati ya wenyenacho na wasionacho, kisha wasionacho sio tuu kukalia makazi ya wenyenacho bali pia kuwabaka binti za wenyenacho na kuwafanya wake zao kwa nguvu matokeo yake ni vizalia wenye hasira machungu na visasi!, michango ya vizalia hivyo humu naibaini wazi, kuambiwa ukweli hawataki, undeni tume ya mapatano na maridhiano muambiane mlivyo fanziana kwenye mapinguzi yale, mshikane mikono, msameheane, msonge mbele!, ndio kwanza wengine wanatafuta scapegoat ya hasira zao kuwasingizia wengine kuwa ndio waliopindua ili kujifariji!, tena Waushukuru sana huu Muungano Adhimu, vinginevyo sijui wengine wangekuwa wapi hii leo!.
Pasco.
Pasco,
Sikukwepa kitu chochote.
Huo mtazamo wa kitabaka ni kwa aupendae.
Mimi niliandika kwa ''biographical approach.''
Hii ndiyo staili yangu ya uandishi.
Huyo Dk. Mkenda hakuwa wa kwanza kuliona hilo la katibu wa Dockworkers
ambae hakuwa kuli.
Prof. Shivji alipita hapo kwanza na katika kitabu changu nimetoa jibu.
Hapo Sakura na Kipumbwi Dk Ghassany hakufanya mahojiano na yoyote kwa
sababu watu wenyewe hawakuwapo.
Usihangaike na hilo.
Miongo zaidi ya mine ishapita.
Dk. Ghassany alifika hapo kutafiti mengine katika historia ya mapinduzi.
Nimesoma barua zote Makoko alizokuwa akimuandikia Ally Sykes katika
miaka ya mwishoni 1950 mpaka zile za Makoko alizokuwa akimuonya Ally
Sykes kuhusu Nyerere na mengi tu.
Sikuona haja ya kuziweka katika kitabu changu.
Si hizo barua za Makoko tu nilizoziona na kuacha kuzitumia.
Nimesoma barua za Chief Thomas Itosi Marealle kwa Ally Sykes na zina
mengi kuhusu Nyerere.
Nani wa kufanya tume ya maridhiano?
Fikiri kwanza kablsa hujafungua kinywa kusema.
Pasco haya mambo huna uwezo wa kuyazungumza hujui kitu.
Soma kwanza ndiyo uandike.[/QUOTE]
Pasco
Mkuu hebu fanya sulhu kwanza na hawa waungwana ili tupate kujifunza hapa, usogora wako ndio wafanya tusipate mengi.
Kuhusu hilo la "Biographical Approach" dhidi ya "Mtazamo wa Kitabaka" hata huyo Mkenda na Shivji walito pongezi stahiki kwa kuwa kazi iliyofanyika si haba.
Binafsi sikubaliani na yote ya Mohammed Said, lakini nakubali kuwa ameleta mengi ambayo hayakuwahi kusema popote, mengi yaliyo muhimu.
Huwa nashindwa kuwaelewa watu kama Mag3 na kundi lake wanapojaribu kuonyesha kwamba juhudi zote zilizofanyika ni upotoshaji.