Mkuu Kawarizimu, kwanza asante kwa kujibu hoja objectively. Literacy work yoyote ama inakuwa complemented na literacy work nyingine, ama inakuwa defeated na literacy work nyingine, ndio maana siku za nyuma kwenye ule uzi kazi ya Maalim Mohamed Said kuhusu maisha ya Wazee wake wa Gerezani, ukishambuliwa left, right and center na watu wakaja na facts za ukweli kabisa kuudefeat urongo wake, walimlazimisha Maalim Mohamed Said ndie atoe toleo jengine lenye ukweli, mimi ni miongoni niliosimama na Maalim kuwa yeye ukweli wake ndio huo, hawa wenye ukweli zaidi na watoe kitabu ili machapisho ya Maalim yawe defeated!.
Kwenye historia ya Zanzibar, nimekuonyesha andiko kuwa wanaodaiwa kuwa wenyeji, Wahadimu na Watumbatu, kule sio kwao!, nikakueleza walipotoka!, tena ni hapa kwetu bara!. Nikakueleza ukiondoa hao Wahadimu na Watumbatu, Zanzibar haina wenyewe ndio maana Sultani katoka zake Oman na kuahamia Zanzibar bila negotions na mtu yoyote kwa sababu kavikuta visiwa havina wenyewe!. Ulichotakiwa kufanya sio tuu kuita watu waongo!. Kama ni waongo, unautaja uongo wao kisha unauweka ukweli wako!. Umeambiwa Watumbatu na Wahadimu asili yao ni bara, kama ni uongo unaiweka ile asili yao ya ukweli unaijua wewe!.
Nimekuambia Sultan Seyyid Said, aliviokota visiwa vya Zanzibar kama sadakalawe, hakukuta mtu pale wala kufanya majadiliano na yeyote kabla ya kuhamia. Sasa wewe kama unazo details alimkuta nani, alifanya majadilano yapi alivitwaa visiwa vya Zanzibar toka kwa nani, tuwekee ukweli huo to defeat uongo uliotangulia!.
Maadamu unayo historia hadi ya malikia wao Mwana wa Mwana, tuwekee nasi tuijue ili tupate kujua huyu Mwarabu alihamiaje hamiaje nchi ya watu hivi hivi tuu, just like that il khali nchi ilikuwa na wenyewe?!.
Ukiweza pia kutueleza hiyo asili halisi ya hao wenyewe tutashukuru, vinginevyo tuanze process ya kuwafukuza wavamizi wa nchi yetu, waliovamia bila ruhusa yetu, wakauweka ufalme wao tulioupindua kwa yale Mapinduzi Matukufu, kisha tuunganishe kabisa nchi yetu iwe "Nchi moja!, Taifa moja! Tujue moja!.
Pasco.