zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Mkuu Zomba, hili la kutokota, huwa natokota mara kibao!, sambamba na kuchemsha, huwa nachemsha mara chungu nzima, ila pia katika kutokota huko, kuna wakati, nawatokotisha!, na katika kuchemka, kuna wakati nawachemsha!.
Miongoni mwa lugha zangu za kuchemsha ambalo imembidi Maalim Mohamed Said akae pembeni, ni hapa nilipomjulisha, akichangia yeye, kuna wafuasi wake hujitokeza kama mainzi wanavyozingea bucha ya utumbo!, wewe mwenyewe si ulishuhudia jana yale mainzi yalivyonisonga utafikiri yanagombea utumbo!. Ulifikia wakati nikajikalia pembeni, kuyaacha yakipishana mpaka yalipopungua, ndipo nikarejea, na kwa uzoefu wangu wa pilika pilika za mainzi, huwa ni mchana tuu, usiku yanatulia!, si unaona mida kama hii, mnakasha ni burdani kabisa!.
Pasco.
Plagiarism. Nakumbuka hilo la utumbo humu nililileta mimi baada ya wewe kuulizwa swali niliandika "naona nzi haoo wamemtangulia muuza utumbo" na unajuwa kabisa nilimaanisha nini. Unakumbuka?
Ni faraja kubwa kwangu kuwa nawe umeongezea "vocabulary" yako japo "kiduchu" kutoka kwangu.
Kumbuka tu, hilo sasa ni ganda tu la risasi si risasi tena, risasi ilishatumika.
