Mkuu,
Kwanza kabisa nikushukuru kwa matusi!
Ni kweli kuwa mimi ni mtu wa bara!Na kama ulivyosema yawezekana nikawa mhaya au msukuma au kabila lolote lile!Japokuwa nimeshangazwa wewe kuniita kwa kabila,labda nikukumbushe tu huku tulishaacha habari ya kuitana kwa makabila!Ukabila ulishakwisha!Sisi ni watanganyika sasa!Japo kuwa nyie ndio mlikuwa mkiturudisha nyuma kwa hoja zenu za udini zilizokuwa zikilichafua Taifa!Natumaini mkijitenga mtakuwa mmetusaidia sana kurudisha umoja wetu wa Tanganyika!
Pili,nikukumbushe tu hawa waarabu waliofika bara hawakuja kwa bahati mbaya,walikuja kwa biashara zilezile kubwa walizokuwa wakifanya.Biashara ya pembe za ndovu(ivory),Mashamba ya mkonge na Watumwa.Waarabu wote unaowaona katika mikoa hiyo ni kizazi kinachotokana na waliokwenda kuendesha biashara hizo.
Pia unapaswa kujua kuwa biashara zote zilikuwa ovu.Kwani zilihitaji nguvu kazi ambayo ilifanya nguvu ya ziada ya kuteka watu kwenye vijiji na kuwafanya watumwa itumike!Kwa hiyo familia zilivunjika,Baba alipoteza mke,mama alipoteza mwana na nguvu kazi ya maendeleo katika eneo husika kupotea.Hili si suala la kufurahia hata kidogo!!!!
Watumwa takribani 50,000 waliingizwa kisiwani Zanzibar kutoka bara na waarabu kila mwaka na takribani watumwa 80,000 walikufa njiani kuelekea kisiwani humo!Kwa hiyo kama kweli Una uchungu na hao waarabu ,wahindi na waasia 18,000 waliokufa kutokana na mapinduzi matukufu lazima utakuwa una matatizo kumkichwa!
Kusema kuwa hakuna mzalendo aliyekufa kutokana na utawala wa waarabu,huo ni upotoshaji wa ajabu unaohitaji maombi!
Mwisho,nakuomba upunguze matusi.Yanapunguza nguvu za hoja yako.Na pia hayatawasaidia pale mtakapokuwa mnaijenga Zanzibar mpya,sana sana mtaendelea kulifanya lionekane ni Taifa lenye vichwa 'chakavu'!
Asante!
Mkuu,
Kwa hisani yako tafadhali usifanze nikapatwa na simanzi!...hujui yakuwa weye Mkuu ndo uloanza lugha kali na kebehi/matusi!? Nitake radhi Yakhe,kwa kunivunjia hishma yangu!
Mbona hukujibu nilikuuliza nini maana ya "Muarabu-Koko" kama ulivyotaja!? Acha kujifanza ati weye ndo
Victim sasa!? Teeh! Teeh! Teeeh!
Nakuhakikishia yakuwa...mie hutumia
lugha kali tu pale
inapolazim! Jaribu kupitia ile bayana yako ya awali ilonilazim mie kukujibu
ujionee Mkuu!?
Khalaf tafadhali Mkuu,tuwekeane staha japo kiduchu...hivi umefuatilia bayana zoote hapa jamvini!? Mbona wajitia hamnazo,huwaoni waloanzisha matusi na waendeleao kutukana!?
Mie hiyo Tanga-Nyikwa nafahamu kupita kiasi...ni bakhti mbaya tu yakuwa humu JF hatufahamiani Mkuu! Utastaajabu yakuwa wewe labda ndo itakua mgeni hapo Tanga-Nyikwa!
Kwa hiyo acha kujipa
false hope na ati kujidanganya yakuwa hapo Tanga-Nyikwa hapana ukabila ulokubuhu na pia udini/Islamophobia!? Weye unaishi wapi Mkuu wangu!?
Nina mangi ya kukwambia...lakini tu kiduchu jiulize yale mapigano yalokubuhu mpaka kulazimisha mauaji ya takriban watu 18 kati ya
Wandamba na
Wasu-k.u.m.a kule Ifakara.Malinyi,Mahenge na Ulanga...je ile nini!?
Wafahamu yakuwa ilimlazim IGP wa Police ende pale kwa haraka na baadhi ya majeshi yalokua ile Mikoa ya jirani kuwekwa
on standby!?
Mie kwenye bayana yangu ilopita nimekuuliza
specific questions...lakini nilikhis Mkuu yakuwa hautakua na majawaba yenye
mantik asilan,ndo matokeo yake ati umenijia na hizo
triangular excuses/explanations!? Dah!
Sasa nitajie wapi umeshawahi kusikia pale
Zanzibar...makabila/families zipi ziliuana kwa ukabila!?
Sitarajii kunitajia ule upuuzi wa yale mauaji/nakma ya 1964!?...maana hii nayo ni subject/Topic nyangine kabisa!!
Mkuu mie nduguyo hiyo history/Anthropology na Philology ya dunia/ulimwengu mzima, ninafundisha na ukilazimisha nitakuwekea ushahidi hapa japo kiduchu! Kwa hiyo nina some sort of
authority!
Sikutishi wala si dasturi yangu majigambo asilan...lakini ufahamu yakuwa nafahamu nini ninachozungumza tena kiundani mno na wala sibahatishi! Kwa hiyo huna haja ya kunitumia hayo maelekezo/"hoja" yako
dhaifu!
Nisingalipenda kwa sasa kukutaka ku-
substantiate hizo statistics/figures hapo ulizotaja wala
sources zake...maana itatulazim
chokonoa mangi mno!? Nafikiri mie binafsi utaona nalijaribu kumtahadharisha huyo mleta mada!!
Nimefurahika,yakuwa kwa sasa nakukhis waelekea kurejea kwenye mazungumzo
mema na yenye
staha...basi labda
mnakasha sasa utapoa
dharuba na hoja zilo
njema kutawala!?
Ahsanta.