Miaka 500 yatimia tangu Kanisa Katoliki kumtenga Martin Luther, mwanzilishi wa Kanisa la Kilutheri

Msingi wa mafundisho ya Padre Dr Martin Luther ulikuwa mambo mawili:
1. Sola gratia. Maana yake "kwa neema tu". Kwamba hakuna namna binadamu anaweza kununua wokovu ila tu kwa neema ya Mungu, na ndio uliokuwa msingi wake wa kupinga lile fundisho lililokuwepo wakati ule la watu kutakiwa kulipia toba ama kununua ondoleo la dhambi.
2. Sola scriptura. Maana yake "kwa maandiko tu". Kwamba jambo lolote ndani ya kanisa ni lazima liwe na msingi wake katika maandiko matakatifu ya Biblia. Na aliamini kuwa kulipia toba ilikuwa kinyume na maandiko.

Natamani angefufuka leo aje ashuhudie jinsi kanisa aliloasisi linavyokiuka misingi yake. Sakramenti zinauzwa. Aje amuulize Mch Daniel Mgogo anahubiri Biblia gani katika zile comedy zake kama za Masanja Mkandamizaji. Aulize kama maaskofu wanaongoza ibada za ndoa za maskini au hata maziko ya masikini.

Naongezea yafuatayo kuhusu mada hii:
1. Haikuwa dhamira ya Padre Dr Martin Luther kujitenga na kanisa katoliki. Akiwa Profesa wa Moral Theology katika chuo kikuu cha Wittenberg, Fr Luther aliandika zile 95 theses kuamsha mjadala wa kitaaluma, akiwa na lengo la kupata sauti za wengine pia ili kurekebisha kasoro za kiteolojia alizoziona.
2. Kama zilivyo taaluma nyingine, Theology nayo ina wabobezi wake ambao ni kawaida kukinzana kifikra miongoni mwao. Kulikuwa na different school of thoughts kuhusu hizi 95 theses, wapo waliomuunga mkono Fr Luther, na wapo waliompinga kwa hoja za kitaalamu. Miongoni wa waliompiga ni Fr Konrad Wimpina ambaye aliandika theses 106 kupinga zile 95 za Fr Luther. Mwingine ni Johann Eck ambaye pia alikuwa rafiki na mwanataaluma mwenzake Fr Luther; huyu aliandika majibu dhidi ya zile 95 theses kwa namna iliyosababisha wafarakane na rafiki yake.
3. Hata hiyo misingi ya 'sola gratia' na 'sola scriptura' inatafsirika kitofauti sana miongoni mwa wataalamu, wakianzia na definitions: neema ni nini? Maandiko ni nini? Kumbukeni vitabu vya Biblia vilikusanywa na hawa hawa ambao Fr Luther alikuwa anawa-challenge, lakini yeye akiongozwa zaidi na fani yake ya Moral Theology. Hata moral theologians wenzie alipishana nao katika tafsiri za mambo mbalimbali.
4. Mwisho, kitendo cha kutengwa kwa Fr Luther nadhani kilitokana na a failed dialogue. Palikosena an unbiased moderator wa kusimamia hii dialogue bila mihemuko. Hata hivyo, matokeo yake bado yamekuwa afya kwa kanisa (kwa maana ya Mwili wa Kristo) kwa kiasi fulani, na changamoto zilizobaki tunaishi nazo.
 
Martin Luther alikuwa kidume kweli. Nchi ya Germany in deserve kuitwa HE.
1. Martin Luther
2. Adolf Hitler na wengine wengi wameuoa Ujerumani heshima ya kipekee kabisa duniani
Wajerumani ni akili kubwa na wachapa kazi. Waliishi Tanganyika miaka 20 tu lakini walijenga miundo mbinu ambayo mingine tunaitumia mpaka leo.
 
Martin Luther alikuwa kidume kweli. Nchi ya Germany in deserve kuitwa HE.
1. Martin Luther
2. Adolf Hitler na wengine wengi wameuoa Ujerumani heshima ya kipekee kabisa duniani
Helmoth Kol,Angella Merkel,Willy Brandt,Oliver Khan,Jurgen Klop ,Dietmer Hamman nk
 
Nyie mnaimba,,,,neeendeeeni naaa amaaaniiii,kwanini msiseme tu,nendeni na amani? Mbung'o wa Kawe anasema,Ukimuona hivi na lifimbo lake hivi na likanzu jeupe ujue Ni......
 
Yaliyosemwa ni sawa. Mie siyo PhD wa theology lakini katika kusomasoma tungo za USSR, kuna haya ya kuongenzLa:
G
MOSI
Sapoti kubwa ya ML ndani ya Ujerumani ilikuwa ni ya Mfalme (Chancellor) aliyemuona Papa kama msh8ndani waje Kisiasa. The whole thing was politically motivated "na sisi tuwe nao uhuru wetu. ilijitokeza tena England pale Papa alipokataa kumpa talaka King wa Uingereza ili avmuoe hawara yake. King akaachana na Papa on sovereignty grounds, mpaka leo MYPHITYO.

PILI
ML anaheshimiwa kwa kAufunya Bible iwe ya watu, hapo zamani ilikuwani Kilatini tu. Alichokosea (kama ni kukosea) ni pale alipoikataa Sabato isiwe Jumamosi. Ili kumng'ong'aPapa, ML aliamua KKKT kuwatumie Bible ya Kiebrania tu, si ile ya Kigiriki ilivyokwa mapokeo ya Katoliki. Hadi leo Biblia Katoliki ina vitabu 46 Agano la kale, ya KKKT ina vitabu 39 Agano la Kale, pungufu 7. Alifyanya hivyo kupoza Wasabato, KKKT bado husali Jumapili.

TATU
Enzi za ML kulikuwa na utitiri wa dini, kama vile Mbeya kulivy,o. Kulikuwa na Jan Hus wa Moravia, Czechoslovakia (Moravians), Anglikana England, na Methodists wa Scotland, Austria na USA. Katoliki hawakustuka, walijua ni kuwa .history repeats itself.

Kupama kuna nikichosahau ongezeni,
Regard:
LGF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…