Miaka 57 ya Muungano: Rais Samia ielekeze serikali yako ijenge taifa

Miaka 57 ya Muungano: Rais Samia ielekeze serikali yako ijenge taifa

DENLSON

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
949
Reaction score
1,260
Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano.

Nikupongeze wewe binafsi Mh.Rias kwa salamu ambayo inaonda matabaka na kuleta umoja ndani ya Jamuhuri ya Muungano. Hongera sana kwa ubunifu huu naamini ni mwanzo tu na mengi yatafuata.

Niende moja kwa moja kwenye mada husika, Tumekuwa na awamu tano za uongozi na sasa tuna awamu ya sita ambayo ni ya kipekee kwa sababu inaongozwa na Mama tofauti na awamu zote ambazo ziliongozwa na wababa. Katika awamu hizi tano zilizopita isipokuwa awamu ya kwanza peke yake, zote nne zilijikita katika kujenga nchi na si kujenga taifa, ieleweke kuna tofauti kati ya NCHI na TAIFA. Unapojenga barabara, hospitali, mabwawa na reli unajenga nchi sio taifa. Nchi ni ardhi yenye mipaka halali inayotambulika kisheria na umoja wa mataifa. Taifa ni watu waliokubaliana kufuata falsafa fulani wakiongozwa na sheria halali walizojiwekea kwa kukubaliana yaani katiba. Taifa linaweza likaishi kwenye nchi ya taifa lingine na nchi inaweza kutawaliwa au kukaliwa na watu wa taifa lingine. Mfano. Taifa la Uingereza lilitawala nchi ya Kenya.

Awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilijikita katika kujenga taifa kwa kufanya kila jitihada za kuondoa ubaguzi, makundi na ukabila na kuleta usawa ndani na nje ya nchi yetu.

Turudi kwenye mada kuu, Kumbukumbu pekee ambayo itaifanya awamu ya sita kuwa ya tofauti ni kujenga taifa na itaweza kujenga taifa endapo kama itahusisha yafuatayo:
  • WEZESHA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA: Katiba yetu ya sasa ina mapungufu mengi ambayo yalionekana toka kipindi cha Hayati Mwalimu Nyerere. Je katiba itajenga utaifa? Ndio, kwasababu katiba ndio sheria mama kwa taifa lolote ndio muongozo wa utaratibu wa kiutawala. Katiba mpya itaacha kumbukumbu nzuri na ya muda mrefu kwa uongozi wa awamu ya sita kwasababu itaweza kushughulikia vilio vingi ambazo zinapigiwa kelele na makundi mengi katika taifa letu.
  • JENGA TAASISI HURU NA IMARA: Hakuna taifa imara pasipo kuwepo na taasisi huru na imara, bila taasisi imara tutakuwa tunaenda mbele hatua kumi tunarudi nyuma hatua 100 kila baadaya miaka 10. Tuwekeze kwenye taasisi zinazo weza kufanya mmamuzi kwa maslahi mapana ya nchi kwa miaka 100 ijayo. Tassisi ambazo hata akitokea nchi ikaangukia mikononi mwa pandikizi taasisi ziaweza kudili nae bila woga na bila kusita na hili litawezekana endapo tu hitaji namba moja la Katiba mpya litatekelezwa kwasababu Katiba tuliyonayo haitoi nafasi ya kuwa na taasisi huru na imara kwasababu utendaji wa tasisi hizi unategemea na maono na maamuzi ya kiongozi aliyepo madarakani na kwasababu hiyo utendaji wa taasisi hizi hauna muendelezo wa maono. Taasisi ndio hujenga watu kuwa wa aina fulani, taasisi ndio hujenga falsafa na kushawishi mawazo na maamuzi ya watu. Katiba mpya itatupa taasisi zinanazoweza kujitegemea katika kufanya maamuzi na kuyasismamaia kwa maslahi mapana ya taifa letu.
  • FUMUA NA UUNDE UPYA MFUMO WA ELIMU: Ukiingalia mfumo wetu wa elimu ni kuwa unaandaa watu kuwa wafanyakazi Elimu yetu licha ya kuwa na mapungufu ya kifikira na ujuzi lakini pia inakosa muendelezo wa utaifa. Elimu ilitakiwa imuandae mtu awe mzalendo kwa taifa lake, ilitakiwa iandae viongozi, ilitakiwa iandae watu kujitegemea kifikira, kiuchumi na kimaamuzi iandae watu wenye uwezo wa kutatua matatizo. Fumua mfumo wa elimu ili elimu yetu iwe na tija kwa taifa. Jenga taifa kupitia elimu. Hapa nakushauri kaa na Lowassa muulize kwanini sera yake ilikuwa Elimu, Elimu, Elimu.
  • BORESHA MGAWANYO WA RASILIMALI ZA TAIFA: Miaka 5 iliyopita malaamiko yamekuwa mengi sana kuhusu namna rasrimali za taifa zinavyogawanywa kwa kupendelea upande/mkoa mmoja hili jambo ni hatari kwa utaifa wetu. Isitokee mkoa flani wakahisi wamesahaulika kwenye mgawanyo wa keki ya taifa huku wengine wakijiona ndio wana haki ya kupata kila kitu, historia inaonesha kuwa sehemu nyingi ambapo taifa liligawanyika ni kwasababu ya kutokuwa na usawa wa mgawanyo wa keki ya taifa. Na niseme hili jambo litawezekana iwapo kutakuwa na mambo yafuatayo (i) Katiba mpya (ii) Taasisi huru (iii) mipango endelevu inayozingatia mahitaji na masilahi ya taifa. Hapa niseme kuwa lazima mamlaka ya viongozi yapunguzwe ili kuwezesha hili.
  • PUNGUZA MAMLAKA YA VIONGOZI: Bila kufanya hili ayo mengine hapo juu yanakuwa kupoteza muda bure, maana utafanya leo baada ya miaka 10 ataingia mwengine atafuta na kufanya atakavyo. Tumia katiba mpaya kupunguza madaraka ya viongozi, katiba isiwafanye viongozi kuwa miungu watu, ikitokea wakatumia madaraka vibaya hakuna wa kuwahoji wala kuwazuaia, Leo jiulize ikatokea akapatikana kiongozi mwenye mawazo na mtazamo tofauti na watangulizi wake na akaona hakuna umuhimu wa kulipa mafao ya viongozi wastaafu hivi kuna amabaye ataweza kuhoji au kupinga? Ni Taasisi ipi itakayoweza kumkemema? Lakini pia mamalaka haya makubwa kwa viongozi yana umuhimu kwa karne tuliyonayo?
Nikutakiwe mapumziko mazuri ukiendelea kutafakari Muungano wetu adhimu.

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Huu uhuru wa habari uliowekwa sasa hivi utaibua "wanafalsafa" ambao siamini kama hata wao wanajua wanaandika nini au wanalinganisha nini na kutofautisha nini. Yangu macho!!!
 
Huu uhuru wa habari uliowekwa sasa hivi utaibua "wanafalsafa" ambao siamini kama hata wao wanajua wanaandika nini au wanalinganisha nini na kutofautisha nini. Yangu macho!!!
Huu sio uhuru wa habari. Uwezi kuelewa haya kwa kuwa huna uwezo wa kuelewa yaliyoandikwa hapa. Bila kufanya hayo mambo hapo juu hakuna kitu kitafanyika su kinachofanyika sasa kitabaki salama kwa miaka ijayo.
 
Huu sio uhuru wa habari. Uwezi kuelewa haya kwa kuwa huna uwezo wa kuelewa yaliyoandikwa hapa. Bila kufanya hayo mambo hapo juu hakuna kitu kitafanyika su kinachofanyika sasa kitabaki salama kwa miaka ijayo.
Mimi ni zaidi yako fella!!!
 
Utajengaje taifa wakati likiwa limegawanyika? hakuna nutawala wa sheria, watu wapo magelezani kesi za kisiasa..

Hata nyumbani uchumi hupanda kama baba na mama tendegu la kitanda linapiga kelele...
 
Back
Top Bottom