AJIRA SASA
Member
- Sep 5, 2018
- 5
- 5
Wana-JamiiForums,
Nimefika kikomo cha uvumilivu. Naandika post hii kwa hasira, masikitiko na maswali mengi ambayo naamini mimi siyo mhanga pekee katika nchi hii.
Mnamo mwaka 2020, nilikamilisha taratibu zote za usajili wa Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Nilipigwa picha, nikatoa alama za vidole, na kuacha nyaraka zote zinazothibitisha uraia wangu. Tangu mwaka huo hadi leo tunazungumza ni mwaka 2026—ni miaka sita kamili imepita, lakini kitambulisho changu hakijawahi kutoka!
Kila nikijaribu kufuatilia kwa kupiga simu huduma kwa wateja (call center) ya NIDA, jibu limekuwa moja tu, kama wamewekewa kanda ya kunasa: "Taarifa zako zipo hatua za mwisho za uzalishaji."
Hivi hii "hatua ya mwisho ya uzalishaji" ya NIDA ina urefu wa kilomita ngapi? Inachukua miaka sita kuzalisha kipande kimoja cha plastiki?
Kero na Maswali yangu ya Msingi kwa NIDA:
Wakuu, mwenye uzoefu au anayejua namna ya kuvuka huu ukuta wa NIDA anisaidie. Je, kuna yeyote aliyekuwa kwenye hatua hii ya "mwisho" na akafanikiwa kukipata?

- Ufanisi Zero: Teknolojia gani inayotumika hapo NIDA inayochukua miaka sita kukamilisha hatua moja ya uzalishaji?
- Majibu ya Kukariri: Kwa nini wafanyakazi wa huduma kwa wateja wanadanganya wananchi kila siku kwa majibu yasiyobadilika badala ya kusema ukweli wa changamoto iliyopo?
- Unyimaji wa Fursa: Kukosa kitambulisho hiki kunatukosesha fursa nyingi za kiuchumi, kibenki, na kisheria ambazo sasa hivi vinahitaji ID namba au kitambulisho halisi.
- Ubaguzi wa Huduma: Mbona wapo wanaojiandikisha leo na baada ya miezi michache wanapata? Kuna mfumo wa "ujuane" au rushwa unaoendelea chini kwa chini?