Wanabodi,
"CCM itatawala Milele" japo ni kauli ya ukweli mchungu, lakini ni kauli ya ukweli kabisa kuwa ni ukweli halisi na ukweli bayana, katika mazingira ya sasa ya nchi yetu na uendeshaji wa siasa za vyama vingi, chini ya katiba hii ya JMT ya mwaka 1977 ambayo ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, kama hakuna kitakachobadilika kama mchezo wa siasa kuchezwa kwenye uwanja range, kupatikana kwa katiba mpya, au kufanyika mabadiliko madogo ya katiba ya kuuondoa vifungu vyenye ubatili ndani ya katiba yetu na kuunda kwa Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi, then rais Magufuli yuko very right kuwa CCM itatawala milele!.
Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga tuu blah blah, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or
Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM alfa na omega, ina mwanzo tuu, lakini haina mwisho!, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!, kwasababu CCM sio tuu ni chama cha siasa, na chama tawala, CCM pia ni chama dola, CCM ni dola!
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu wa CCM (not necessarily ni Mungu Baba) kuiteua CCM na na kuifanya chama dola, na kuipatia hati miliki ya kuitawala Tanzania milele na milele!, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.
Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi
Paskali