Miaka 60+ nchi inajadili uhaba wa sukari?? CCM hebu kaeni pembeni

Miaka 60+ nchi inajadili uhaba wa sukari?? CCM hebu kaeni pembeni

Inasikiitisha sana na kuumiza ukiacha kuudhi, hapa tunasikilizia sijui muda gani watakata, wanatufanya tuwe watumwa muda wote unatizama simu, nchi ya maajabu hii.

Mungu tukumbuke Kwa kutifumbua macho na akili zetu.
 
Kuna Kagera Sugar, Kilombero Sugar, Mtibwa Sugar na T.P.C lkn bado eti tunahangaika. Nani katuloga kama siyo CCM??

Sent from my Nokia 7 plus using JamiiForums mobile app
 
Huyu aliyejipa uenyekiti wa milele ndio tumpe nchi? Kuweni serious basi
Ccm inaiba kura Kwa faida ya wananchi au genge lao!? Hushangai Samia anaogopa kinyang'anyiro cha urais chamani mwake anataka awekewe fomu Moja wakati hajawahi hata mara Moja kupitishwa kwenye chujio la mkutano Mkuu kama waliopita!
 
Suppose kweli wakae pembeni, kuna nani wa kui replaces CCM?.
P

Kwani unadhani atakosa wa kufanya replacement?

Acha uoga hakuna kitakachodumu.

Kwenye chaguzi wapinzani waliposhida hizo sehem waliposhinda kuna kilichosimama kisa hamna mwakilishi wa ccm au mbadala?

Acha hofu za baadae kesho itajijua sio kukariri bila flani mambo yatakwama, mf: Familia ngapi bado zipo na wategemezi wao hawapo? Hata mambo yakienda kombo kisa flani hayupo basi hiyo ndivyo imepangwa iwe!
Sio kuhoji kuna nani wakui-replace ccm!
Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho ni muda tu haujafika na uoga wa Watanzania kufanya maamuzi ila naamini kizazi kinakuja hakita kubaliana na maelezo yako tuombe uzima ujionee!
 
Kwenye nchi yenye ardhi, mabonde, mito na maziwa kibao bila kusahau bahari. Inakuwaje hatujitoshelezi kwa sukari?

Hiki chama ni kipi inajivunia kwa miaka zaidi ya 60?

Sukari!! Aibu naona mimi.

Bora kuzaliwa mende Ulaya kuliko kuwa mtanzania chini ya CCM.
NCHI YA HOVYO HII
MATUNDU YA VYOO MADAWATI ni mjadala
Tunachagua VIONGOZI wa WASIOFAA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Alafu kuna mtu Anazunguka mikoa kibao na misafara yenye magari lukuki
Anatumia gharama kubwa eti kutatua changamoto [emoji1]
-""#£ aise nchi hii ina vituko

Ova
Mtu mwenyewe mpumbavu,kakutana na wapumbavu hivyo lazima awe mwenye kuonekana mwenye akili sababu hata kwenye kundi la wapumbavu Kuna mwenye afadhari.
 
Hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho ni muda tu haujafika na uoga wa Watanzania kufanya maamuzi ila naamini kizazi kinakuja hakita kubaliana na maelezo yako tuombe uzima ujionee!
I'm praying to God to grant me HIS Grace to witness this day! kwasababu mimi ukweli wangu ni huu Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Wanabodi,

"CCM itatawala Milele" japo ni kauli ya ukweli mchungu, lakini ni kauli ya ukweli kabisa kuwa ni ukweli halisi na ukweli bayana, katika mazingira ya sasa ya nchi yetu na uendeshaji wa siasa za vyama vingi, chini ya katiba hii ya JMT ya mwaka 1977 ambayo ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, kama hakuna kitakachobadilika kama mchezo wa siasa kuchezwa kwenye uwanja range, kupatikana kwa katiba mpya, au kufanyika mabadiliko madogo ya katiba ya kuuondoa vifungu vyenye ubatili ndani ya katiba yetu na kuunda kwa Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi, then rais Magufuli yuko very right kuwa CCM itatawala milele!.


Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga tuu blah blah, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah tuu, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton's laws of motion, ile kanuni ya "a body in motion" or

Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM kama chama, ina mwanzo hivyo ni lazima nayo iwe na mwisho, unless CCM ndie Mungu mwenyewe, ambaye Yeye ndiye Pekee Alfa na Omega hivyo CCM hii iliyopo sasa nayo ni CCM alfa na omega, ina mwanzo tuu, lakini haina mwisho!, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, ndicho chama pekee chenye hati miliki ya kuitawala Tanzania milele!, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote, tuupokee, tuukubali na tuutekeleze. Wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli kabisa watapata taabu sana!, kwasababu CCM sio tuu ni chama cha siasa, na chama tawala, CCM pia ni chama dola, CCM ni dola! CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

Umilele wa CCM kuitawala Tanzania, unatokana na mungu wa CCM (not necessarily ni Mungu Baba) kuiteua CCM na na kuifanya chama dola, na kuipatia hati miliki ya kuitawala Tanzania milele na milele!, ndio maana katika baadhi ya makala zangu za nyuma, niliwahi kushauri tuifute ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, tuifute ruzuku kwa vyama vya siasa, Tanzania turejee kuwa nchi ya chama kimoja cha milele, CCM.
Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Paskali

P
 
Back
Top Bottom