Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Tuyaenzi kwa 4R za Rais Samia?, JMT Tuitendee Haki Zanzibar?, Tuwatendee Haki Wazanzibari? Mshindi Halali Apewe?

Watayaenzi wazanzibar sio sisi,hayatuhusu
 
Mbona umekazania "awasamehe"?

Kama vile umeshawahukumu serikali waliopinduliwa kuwa wana makosa.

Kwanini makosa yasiwe kwa waliopinduwa?

"Reconciliation" siyo maana yake kusqmehe.

"Reconciliation" ni kupatanisha au kupatana.

Wakati unapatsnisha au unapatana unatakiwa uwe na msimamo wa kufunika sura yote ya zamani na kuanza sura mpya, bila kujali nani mkosaji na nani mkosewa.

Chukulia mfano wa Mandela South Africa.


Mimi nashauri Jamshid asije kabisa naamini mwenyewe hataki kurudi na siioni sababu ya yeye kurudi.
 
Mbona umekazania "awasamehe"?
Nimeshauri hivyo kwasababu Rais Samia ni mtu msahimilivu Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
Kama vile umeshawahukumu serikali waliopinduliwa kuwa wana makosa.
Hii ndio picha ya wapinduzi
Kwanini makosa yasiwe kwa waliopinduwa?
Waliopindua wanajiona mashujaa wakombozi wameikomboa Zanzibar yao toka kwenye makucha ya wavamizi fulani kutoka Oman wakavivamia visiwa vyao, wakavitwaa, sijui walimfanya nini Mwinyi Mkuu, ila wakavitawala kama mali yao bila kujua vina wenyewe!.
"Reconciliation" siyo maana yake kusqmehe.
"Reconciliation" ni kupatanisha au kupatana.
Asante sana kwa somo hili la maridhiano
Wakati unapatanisha au unapatana unatakiwa uwe na msimamo wa kufunika sura yote ya zamani na kuanza sura mpya, bila kujali nani mkosaji na nani mkosewa.

Chukulia mfano wa Mandela South Africa.
Ndio nimeshauri Zanzibar iundwe tume ya Truth and Reconciliation Commission kama ile ya South Africa, jina la Mapinduzi Matukufu lifutwe, uindwe serikali ya kidemokrasia ya Zanzibar na sio SMZ.
Mimi nashauri Jamshid asije kabisa naamini mwenyewe hataki kurudi na siioni sababu ya yeye kurudi.
Hili la yeye kurejea Zanzibar, mimi nimeelezwa, tena huwa naelezwa mengi na kila nikielezwa nakipima kama kinaelezeka nakieleza humu, na mfano mzuri ni hiki nilichoelezwa hapa kwenye HII sauti !
Ila pia kuna vingine naelezwa, havielezeki!, hivyo najikalia navyo tuu! Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
 
Kwa wenye imani na Dini zao wanatakiwa wafahamu kwamba hata kupindua matokeo ya Uchaguzi ni dhulma kama dhulma nyinginezo !
Mtahukumiwa soon !!
 
Jamshid ameshazeeka hawezi kutaka kurudi Zanzibar !!
Huduma za afya vp hapo ZNZ !?
 
Paskali nilikuuliza huko nyuma (labda kama kumbukumbu yangu haiko vizuri) maana naona huwa hutumii Dr. (Mara nying) kwa mheshimwa Rais wetu. Kwa ufahamu wangu kama mimi naitwa Juma Ali nikipita U Dr kwa kusoma naitwa Dr Juma Ali, ila nikipata wa heshima naitwa Juma Ali (Dr) inakuwa mwisho kwenye mabano... Naomba mtazamo wako. Na mbona Baba wa taifa JKN hakutuimia hizo status(alikuwa nazo nyingi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…