Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kutokana na tatizo la Upatikanaji wa huduma Bora za Maji safi Nchini baadhi ya Wadau wamekuwa na mawazo tofauti.
Kwa haya na mengine mengi, ungana nasi katika Mjadala unaoendelea kwenye mtandao wa Twitter.
Bonyeza kwenye Kiunganishi hiki kushiriki mjadala: >>> JF SPACES
Baadhi ya hoja zinazotolewa na wadau katika mjadala
MAPHY: Kutumia kigezo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi inamaanisha ni kushindwa kutumia vyanzo tulivyonavyo kwa usahihi
Nilikuwa Dar es Salaam, hakukuwa na Maji kwa asilimia kubwa. Kama tunakosa Maji, usalama wetu upoje?
MAPHY: Kwanza ni aibu kusema Tanzania tuna tatizo la Maji kwa Dunia ya leo. Nchi yetu imezungukwa na Maziwa na Mito, pia kuna Bahari ya Hindi katika sehemu fulani
Hata Mwananchi unapomwambia kuna uhaba wa Maji na anaona vyanzo vingi vya Maji lazima anashangaa.
Benedict: Mabadiliko ya tabianchi tusikatae yamechangia ukosefu wa maji maeneo mbalimbali hapa Tanzania, hii imetokana na vyanzo vya maji ambavyo mitambo ya maji inayosambaza maji kwa wanajamii imeungwa kwenye mito.
Benedict: Mito mingi ilipungua maji kwa kiasi kikubwa hasa kipindi hiki Cha kiangaza na hii imetokana na uharibifu kwenye vyanzo vya maji hasa kufyekwa kwa misitu na mabadiliko ya tabia nchi kwa ujumla.
Benedict: Kuna ongezeko la wa watu na vyanzo au mitambo imebaki kuwa Ile Ile,idadi ya watu tumefikia milioni 63+,miundombinu ya maji imebaki ile ile lazima kuwa na uhaba wa maji.
Benedict: Solution,
1. Kwanza tukubaliane kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kutumia sera na Sheria zilizopo ambavyo kwa sasa ndo vinategemewa.
2.Tuboreshe miundombinu ya maji hasa Ile ya kukusanya maji na Ile ya kusambaza kwa jamii.
3.Vyanzo mbadala vya maji tofauti na mito tegemewa vitafutwe.
4.Tanzania tuna maji ya kutosha ni nchi kuamua kuwekeza kwenye utaalamu na fedha namna ya kupata maji salama kwa watu.
MECIRA: Takwimu zinaonyesha kila mwaka Tanzania tunapoteza hekta za misitu 460,000 hiz hekta hizi zinasaidia sana kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa vyanzo vya maji.
MECIRA: Kwahiyo tusipojikita kwenye kukabiliana na huu uharibifu hasa kutoa elimu kwa jamii na kufuata taratibu za kisheria bado tutasema tu mabadiliko ni kichaka Ila kiuhalisia ni tatizo kwa usalama wa maji Tanzania.
Erick Masese: Kuna haja ya kuacha Siasa kwenye mambo ya msingi.
Erick Masese: Kuna haja ya kuacha Siasa kwenye vitu vya Msingi kama hivi, ni halali tujenge Barabara kubwa japo ni jambo jema huku Wananchi wanakosa Maji
Ni muhimu kuangalia vitu ambavyo vinasaidia na kugusa kundi kubwa, Serikali isione shida kuwekeza kwenye Maji".
Oscar Aretas: Mabadiliko ya Tabianchi ni kitu ambacho kinajulikana, hivyo kuitumia hiyo kama 'point' ya kukosa Maji ni kichaka, na tatizo la Maji sio ni Tanzania nzima, ni baadhi ya Mikoa. Mfano Dar es Salaam kwa sababu Watu wanaongezeka lakini mifumo ni ileile.
Oscar Aretas: Majiji yanapokua yanatakiwa kwenda sambamba na Maendeleo ya Miundombinu, kukosa Maji kunasababisha kuanguka kwa Uchumi wa Mtu au Watu Binafsi wanaohusika na Maji. Tunavyoendelea kama hakuna mabadiliko tatizo hilo litajitokeza tena na tena baadaye".
Tetere: Kiuhalisia ili kuwe na Maji lazima kuwe na miysitu na lazima kuwe na vyanzo vya Maji, usipotunza vyanzo vya maji utakuwa umeshindwa kulinda maji.
Tetere: Mto Ruaha una Siku 109 hautiririshi Maji, wapo Watanzania ambao hawafikirii manufaa ya wengine wametengeneza njia za kuchukua maji kutoka kwenye Mto huo na kuchangia kukauka".
Tetere ameishauri Serikali kuwekeza katika ulinzi na utunzaji wa Mazingira, kwasababu Wataalamu wanasema Mabadiliko ya Tabia nchi yamesababisha kupoteza 1% ya pato la Nchi, yamechangia 63% ya Ardhi ya Tanzania kuharibika.
Sassination: Ni muhimu kuruhusu taasisi Binafsi kushiriki katika Uwekezaji na usambazaji wa maji.
Amesema kufanya hivyo kutaongeza uwezekano wa ushindani na matokeo yake ni Huduma kufika kwa Watu wengi tofauti na ilivyo sasa.
Pia ameshauri Taasisi zilizopewa Mamlaka ya kusimamia Maji kuwajibika ipasavyo, imefikia hatua tunapaswa kuwekeza Teknolojia katika upande wa Maji. Kinachoonekana suala siyo vyanzo bali hakuna Utaalamu au Teknolojia ya kuyafikisha Maji kwa Wananchi
Ameongeza Changamoto iliyopo ni Matumizi mabaya ya Takwimu kutoka Idara mbalimbali kutotumika katika Mikakati ya Maendeleo, ongezeko la Watu linatakiwa kuendana na Mabadiliko ya Huduma.