Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Babu yangu hata kabla hajamzaa baba, kaka zake wanne,waliondoka kwenda Zambia (Kitwe kwenye machimbo ya shaba, baadae watatu wakaenda ''KuJhoni''(Joharnesburg) Africa kusini kwenye machimbo ya dhahabu, mpaka leo hawajawahi kuonekana, Ni zaidi ya miaka 70 iliyopita...hii ni kutoka Mbeya Rungwe Tukuyu...........
... jambo moja tu naweza kusema kwenye hili saga; "tumshukuru Mungu kwa kila jambo"; that simple.
 
Anko...
Alizamia miaka 18 kwenda kuchimba madini, walikua wawili na Jirani ambaye walikua marafiki sana tangu utoto.
Mwenzake alikaa miaka 12 akarudi kusalimia kwao, akaulizwa mwenzako vipi? Akaseme yupo hataki kuja mpka Afikie malengo yake, japo mpka hapo alikua tayari ameshayapatia maisha vizuri ila kwa malengo yake akaona bado..

Yule Rafiki yake akawa hivyo hivyo anakuja na kuondoka, akimsisitiza mjomba aje, anakataa,
Upepo ukabadilika, mali zikaanza kupukutikaa, Mwenzake yeye alikua na maisha tu ya chini, akaamua kabisa kurudi kwao, Mjomba ndio mambo yakazidi kua magumuu, mama yake(bibi) akawa anaumwa yule rafiki yake akatafuta marafiki wengine kule mgodini ili wamuunganishe na mjomba, ikafanikiwa akamwambia Mama yako Anaumwa sana, furaha yake akuone,

Mjomba akakubali kurudi, alikua hana hata simuu, Ilibidi mawasiliano ya maendeleo ya safari yafaywe baina yetu na konda, watu wakaenda ubungo kumpokea(ilibidi yule rafiki yake naye awepo maana alisema ikitokea mkapotezana na konda hamwezi kumkumbuka) ...

Waliooenda ubungo kumpokea hawakuamini Jamaa alivyochokaa,

Hana simu, nauli alitumiwa, Nguo kaweka kwenya rambo, Yaani kwa ufupi hana hili wala lile,

Safari ya kuja kaskazini ikaanza, huo mpango wa kumrudisha ulifanywa kimya kimya bila mama yake kujua, maana usije alivyokua akimpenda na kumsubiria mara nyingi halafu inabuma, watu wakaona awamu hii wafanye kimya kimya,

Hakuna mtu ambaye alimtambua,
Mama ni mama tuuu, Bibi kusikia tuu sauti ya Hodi Akahamaki kilunga "......... Huyu ni....."
Kuingia ndani, watu hawakuelewa zile nguvu bibi aliziapata wapi za kuamka na kumkumbatia mwanate,
Yeye hakujali amedhoofu wala nini alichofurahi ni kumwona mwanae..

Aliondoka kwa malengo ya kuja kufunika ukoo kwa utajiri, akarudi akiwa ndio maskini zaidi, akatafutiwa kijimtaji akaanza upya, Mama yake alipona akaishi miaka mitatu zaidi, akafariki, yule rafiki yake naye akafariki, ndani ya siku mbili Anko naye akafariki, ilikua mwaka huu.
Amefariki na umaskini wake na hata bila mtoto...

Kama kuna Ndugu, jirani au rafiki anayejua huu mkasa, Basi tunafahamiana.
Karibu ningetoa machozi. Kwa uzoefu wangu nadhani watu wengi wanaoshindwa kurudi nyumbani ni wale hali zao kifeha zinakuwa siyo nzuri huko ugenini walikoenda kwa matarajio ya kutafuta. Wanakuwa kwenye ile hali ya ''ngoja pengine kesho nitafanikiwa ndiyo nirudi kwetu.....'' huku siku zinazidi kwenda. Hasa kwenye migodi kuna haya mambo sana.
 
Yaani hata Babu akawa anamwambia wewe ushakuwa mkosi...hapo dingi yuko bwiru anasoma..anarudi hom hakumkuta sisy ake ...Kuna makabila mpk leo wanaendekeza hizo mila za ajabu na mamfumo dime....nikibarikiwa kupata mtoto wa kike sitaruhusu aolewe kabila langu... Sitaki kbs

Nikupe pole nyingi!

Kama hajazaliwa hadi leo basi tuseme atakuwa tayari kuolewa miaka 20 ijayo, unauona wapi uwezekano wa kumchagulia mke/mme miaka hiyo!

Vipi hao wa kiume, hutowaruhusu pia kuoa kabila lako.?
 
Umenikumbusha jambo moja. Mama yangu alipoolewa alizaa watoto watano wa kwanza wote wanawake. Nasikia watu wakaanza kumsema na bibi yangu anampiga vijembe kuwa anakula chakula cha bure wakati anazaa majike tupu. Alhamdulilah nikazaliwa mimi mwanaume lakini alikuwa ''ameshaionja joto ya jiwe''.
 
Njia nzuri kabisa ya kuepusha mtoto wako wa kike kunyanyaswa ni kumsomesha apate elimu nzuri. Na ikiwezekana apate exposure ya kutembelea au kukaa nchi nyingine zilizoendelea.
 
Mkuu unawezaje kukumbuka hadi tarehe na mwezi.?
Na wewe hiyo ‘wizakale’ ni ‘umekuja zamani’, usharudi ulikotoka.?
Wakati anaondoka nikikuwa darasa la sita, nikipomaliza elimu ya sekondari mwaka 1976 niluajiriwa moja kwa moja na Shirika la Reli mjini Tabora. Mwaka 1981 nikahamishiwa Mwanza ndipo nilipomkuta kaka anaendelea kubangaiza maisha yalishampiga sana. Mwishowe mwaka 1988 akaja nyumbani kwangukuniomba nimpeleke nyumbani. Ndipo tarehe 3/9/1988 nikampeleka. Mimi matukio muhimu huwa ninaandika kwenye daftari langu la kumbukumbu.
 
Umenikumbusha jambo moja. Mama yangu alipoolewa alizaa watoto watano wa kwanza wote wanawake. Nasikia watu wakaanza kumsema na bibi yangu anampiga vijembe kuwa anakula chakula cha bure wakati anazaa majike tupu. Alhamdulilah nikazaliwa mimi mwanaume lakini alikuwa ''ameshaionja joto ya jiwe''.

😆😆😆😆😆 maza mtoto wa kwanza had 3 was girls ..baba akamwambia sijakuona uzae mademu nenda kwanza kwenu😆😆! Aliporudi ndo tukapatikana sisi .hahaha..mie men wa hivyo mbona namchinja usk
 
Nikupe pole nyingi!

Kama hajazaliwa hadi leo basi tuseme atakuwa tayari kuolewa miaka 20 ijayo, unauona wapi uwezekano wa kumchagulia mke/mme miaka hiyo!

Vipi hao wa kiume, hutowaruhusu pia kuoa kabila lako.?

Wakiume ntawaruhusu...hakuna watu wana mfuko dume Kama hili kabila..yaan Bora uoe msukuma kuliko kuolewa na msukuma...ukizaa majike shida. Ukiwa na kipato kuzid mume utasemwa ...yaan kila kitu shida .
 
Wakati anaondoka nikikuwa darasa la sita, nikipomaliza elimu ya sekondari mwaka 1976 niluajiriwa moja kwa moja na Shirika la Reli mjini Tabora. Mwaka 1981 nikahamishiwa Mwanza ndipo nilipomkuta kaka anaendelea kubangaiza maisha yalishampiga sana. Mwishowe mwaka 1988 akaja nyumbani kwangukuniomba nimpeleke nyumbani. Ndipo tarehe 3/9/1988 nikampeleka. Mimi matukio muhimu huwa ninaandika kwenye daftari langu la kumbukumbu.

Shikamoo!
 
Maeneo meng hapo zaman hasa uko vijijini yalijaa ukandamizaj sana kwa kisingizio cha mila na desturi.

wazee walikuwa na nguvu sana silaha yao kubwa ikiwa ni matumiz ya nguvu za giza(uchawi). mzee anakupatia shamba, anakuolesha unaishi hapo chini ya utawala wake na ndugu wengne wa ukoo. akikuambia kesho hutoamka ni kweli huamki na hakuna wa kusema lolote.

hawa walioweza kuondoka ni wale wachache waliopata upenyo na mwanga wa kufika maeneo mengne haswa ya mijini na kushangazwa jinsi watu wanavoishi kwa uhuru pasipo bugudha yoyote ile. maisha ya mijini hayajawah kubadilika kila mtu anapambana kivyake hakuna mtu wa kufatilia maisha ya wenzake.

sasa fikiria ingekuwa ni wew ungefikiria kurudi tena kule matesoni?
 
Sisi Watanzania tuache Mambo ya Kulilia Mara Ndugu yangu Kapotea wakati Ata Akirudi Leo Hakuna Msaada Wowote Atakaopata Zaidi Ya Pole na Unafikii Mwingi tu.
Story Nyingi Msaada Zero Kila Mtu Apambane na Life Lake.

Kuna Nchi kama Burundi na wao Wasemaje Kuhusu Ndugu zao Waliopotea.

Sisi huku Bongo Watu wanaamua Kuishi Maisha Yao Kutokana na mfumo mzma wa Jamii no Support.
 
Wakiume ntawaruhusu...hakuna watu wana mfuko dume Kama hili kabila..yaan Bora uoe msukuma kuliko kuolewa na msukuma...ukizaa majike shida. Ukiwa na kipato kuzid mume utasemwa ...yaan kila kitu shida .
Nitakubalina na wewe. Kila nikisikia hotuba za ''mkulu'' anavyowatumia wanawake kama vyombo vya kufikisha humour zake za kulazimisha huwa nakereka sana. Hata anavyom-treat madam wake ni ushahidi tosha. Ila mimi ninavyojua ni kuwa kanda ya Ziwa yote (labda kuondoa kwa wahaya) wana mfumo mbaya sana wa kuwakandamiza wanawake. Tena huko mkoa wa Mara hata watoto ni victims. Nakumbuka niliwahi kumtembelea jamaa mmoja wa Mara, wakati wa chakula watoto walikuwa wamejumuika nasi lakini cha ajabu walikuwa wamezunguka meza kwa kupiga goti moja muda wote wa kula.
 
Kwanza ni marufuku kula pamoja na wanaume...wanaume wanaweza beba chungu Cha mboga na usifanye kitu!😄😄😄! Mie pia nimepitia Sana unyanyasi huo kwa baba...dogo letu mpk leo wanamtreat Kama mfalme!
Nilifight Sana nikajua shortcut ni mm niwe na life zuri . .Kuna ukandamizaji Sana ..Tena ule wa kuumiza ..huoneshwi hata Hati za viwanja zimeandikwaje...yaan unaishi Kama unaelea hewani tu mradi kuche😆😆! Yaan wanaume wa kisukuma ni balaa!...hawa dawa yao uwazidi tu wanakuwaga Kama mavifaranga yenye mdondo
 
Back
Top Bottom