Acha Mungu aitwe Mungu, Baba yangu mzazi aliondoka mara baada ya Mama kufariki, nilikuwa bado mdogo sana kipindi hicho, nilikuwa na miaka minne tu, Naanza primary mpaka namaliza secondary mpaka chuo, sikuwahi kumtia machoni, Ndugu hawapajui hata kwao maana alikuja Dar kutafuta maisha tu ila asili yake ni Mtwara, Mwaka 2018, nikasema ngoja nikamtafute kama nitabahatisha kumuona, Sikuwahi kufika Mtwara kabla, ila nilijipa ujasiri nikakata tiketi mpaka Masasi, Basi limeingia Masasi giza lishaingia, nikaenda kwa jamaa baada ya salamu nikamuulezea full story na kumtajia jina la baba, Jamaa akasema Masasi kubwa sana hii, huwezi kumpata mtu kwa kuulizia jina tu, nikamwambia Mzee XXX kwa kule DSM alikuwa ana ujuzi wa kutengeneza bidhaa fulani, jamaa akaniambia kwa Masasi anayotengeneza bidhaa hizo ni mtu mmoja tu, na sipajui anapokaa ila namuona maeneo ya Upanga (Upanga ni kitongoji ambacho kipo ndani ya Masasi) nikachukua pikipiki mpaka mitaa ya upanga, nikaanza kuuliza kwa muuza mtengenezaji wa hiyo bidhaa, mpaka nafikishwa kwake, Usiku umeenda kidogo, basi baada ya kujielezea, mke wake alifurahi sana akanikarimu vizuri sana, Baada ya yeye kuja, alinipita maana hakunijua muda ulishaenda na hakuna umeme kwake, Baada ya kuambiwa mwanao huyo, Mzee alifurahi sana na alinikumbuka, Namshukuru Mungu alitia wepesi kwa hilo.