Kuna wazee wawili nimekutana nao mikoa ya Pwani, wametoka huko usukuman zaidi ya miaka 20 iliyopita, wameacha familia zao na wala hawana mpango wa kurudi, wanaogopa kurudiWatu wanapigwa tunguli hadi wanasahau kwao.
Wanawake ni shiiida!
mwana misalaba ni mama yako?
jacana tuna kusubiri kwa hamu hapa kuna maswali Tata yanahitaji majibu
Ukimwambia aende kwao kusalimu anasemaje sasa? Kwa hiyo Hana hata mawasiliano na nyumbani?
Sema shikamoo babu if you are under 20; shikamoo baba if you are under 40 or shikamoo Kaka mkubwa if otherwise. Salimia kikamilifu na kwa heshima zote tafadhali. Tuko na wazee wetu humu jukwaani sema fake id ndio hivyo tena tunajiona tuko sawa.Shikamoo!
Sema shikamoo babu if you are under 20; shikamoo baba if you are under 40 or shikamoo Kaka mkubwa if otherwise. Salimia kikamilifu na kwa heshima zote tafadhali. Tuko na wazee wetu humu jukwaani sema fake id ndio hivyo tena tunajiona tuko sawa.
Kuna kabila moja kidogo ni tofauti. Japo watoro hawakosekani ila wanajitahidi sana kurudi makwao na familia zao walau kila baada ya muda fulani. Ila kuna kabila zingine utadhani watu wamejizaa hawana wazazi wala ndugu mtu yuko uhamishoni miaka zaidi ya 10 hana habari na kwao.Maeneo meng hapo zaman hasa uko vijijini yalijaa ukandamizaj sana kwa kisingizio cha mila na desturi.
wazee walikuwa na nguvu sana silaha yao kubwa ikiwa ni matumiz ya nguvu za giza(uchawi). mzee anakupatia shamba, anakuolesha unaishi hapo chini ya utawala wake na ndugu wengne wa ukoo. akikuambia kesho hutoamka ni kweli huamki na hakuna wa kusema lolote.
hawa walioweza kuondoka ni wale wachache waliopata upenyo na mwanga wa kufika maeneo mengne haswa ya mijini na kushangazwa jinsi watu wanavoishi kwa uhuru pasipo bugudha yoyote ile. maisha ya mijini hayajawah kubadilika kila mtu anapambana kivyake hakuna mtu wa kufatilia maisha ya wenzake.
sasa fikiria ingekuwa ni wew ungefikiria kurudi tena kule matesoni?
Usirudie tena kuzingua usiowajua unless na wao ni wazinguaji kama akina STRUGGLE MAN na Bwana Utam.😆😆😆Huyu atakuwa same age na maza angu...!...au nimwite bamdgo!..yaan tena kuna kipindi nilikua namzengua balaa🙌😄🤸🤭!
Sikumzingua vby...Basi tu kebehi kwa wasukuma😷Usirudie tena kuzingua usiowajua unless na wao ni wazinguaji kama akina STRUGGLE MAN na Bwana Utam.
Umenikumbusha kisa cha profesa mmoja alinogewa na penzi la kimada baa medi hadi kamjengea na kuhamia kwake for good huku akiwa na mke wa ujana wake; mke wa ndoa waliyechuma pamoja. Miaka ikasonga akaugua ngoma hali ilipokuwa ngumu kimada akamtimua. Akaombewa msamaha kwa mkewe akarudi kuugulia pale hadi mauti. Wapendwa tupende na kuthamini kwetu tungali wazima wa afya, wenye nguvu, na nafasi kiuchumi. Tusisubiri hadi tukongoroke.Akishaanza kuugua atarudi tu; mbona Dk shika yupo na ndugu zake wa damu wanamuuguza. Huwa ni suala la muda tu.
Me mwenyewe ninampango nisepe nisijulikane nilipo maana nina ndugu. SIONI IMPACT YAO KABISAAAA
[/Q
Usiseme hivyo,ndugu ni wa muhimu sana,kama huoni umuhimu wao kwako,wewe una umuhimu mkubwa kwao.
Huu uzi umekuwa na shuhuda nyingi sana za utoro kwenye familia! Sikuwahi kuwaza kama ni tatizo kubwa hivi. Serikali na taasisi zifanye sensa ya tatizo hili na kulitafutia ufumbuzi hata awareness kwa wananchi inaweza kusaidia kulipunguza. Otherwise litangazwe janga la kitaifa.Acha Mungu aitwe Mungu, Baba yangu mzazi aliondoka mara baada ya Mama kufariki, nilikuwa bado mdogo sana kipindi hicho, nilikuwa na miaka minne tu, Naanza primary mpaka namaliza secondary mpaka chuo, sikuwahi kumtia machoni, Ndugu hawapajui hata kwao maana alikuja Dar kutafuta maisha tu ila asili yake ni Mtwara, Mwaka 2018, nikasema ngoja nikamtafute kama nitabahatisha kumuona, Sikuwahi kufika Mtwara kabla, ila nilijipa ujasiri nikakata tiketi mpaka Masasi, Basi limeingia Masasi giza lishaingia, nikaenda kwa jamaa baada ya salamu nikamuulezea full story na kumtajia jina la baba, Jamaa akasema Masasi kubwa sana hii, huwezi kumpata mtu kwa kuulizia jina tu, nikamwambia Mzee XXX kwa kule DSM alikuwa ana ujuzi wa kutengeneza bidhaa fulani, jamaa akaniambia kwa Masasi anayotengeneza bidhaa hizo ni mtu mmoja tu, na sipajui anapokaa ila namuona maeneo ya Upanga (Upanga ni kitongoji ambacho kipo ndani ya Masasi) nikachukua pikipiki mpaka mitaa ya upanga, nikaanza kuuliza kwa muuza mtengenezaji wa hiyo bidhaa, mpaka nafikishwa kwake, Usiku umeenda kidogo, basi baada ya kujielezea, mke wake alifurahi sana akanikarimu vizuri sana, Baada ya yeye kuja, alinipita maana hakunijua muda ulishaenda na hakuna umeme kwake, Baada ya kuambiwa mwanao huyo, Mzee alifurahi sana na alinikumbuka, Namshukuru Mungu alitia wepesi kwa hilo.
mkuu mtu haend au kubaki uhamishoni hivihivi tu. mara nyngi ni matatizo na mifarakano ndani ya familia ndo inayokimbiza watu wasitamani wala kufikilia kurudi makwao.Uzi wa utafutaji, uparanganaji, chuki, husuda, kukata tamaa, aibu nk. Pamoja na yote nyumbani ni nyumbani tu good or bad is our home.