Miaka 63 ya uhuru wenye ukoloni wa mtu mweusi.

Miaka 63 ya uhuru wenye ukoloni wa mtu mweusi.

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Kwanza kabisa poleni na pilika za mwisho wa mwaka, mambo yamekuwa mengi ajali, magonjwa na kila aina ya ubaya unaotulenga sisi binadamu.

Tuwe na mwisho mwema.

Hili suala la uhuru kiukweli mimi sioni kama ni uhuru wenye haki na kufuatwa kwa misingi ya katiba kama inavyoagiza.

Kama haitoshi huu uhuru umeleta nini kimaendeleo?? Jamii zetu zinaishi maisha magumu na umasikini uliokithiri.

Elimu duni huduma za afya duni na kila aina ya huduma ni duni.

Uhuru tulionao sisi ni uhuru usiokuwa na mantiki yeyote ile kwenye jamii yetu isipokua kwa watu wachache.

Kipindi tunapata uhuru nchi ilikua kwenye viwango vizuri kiuchumi ila kwasasa halii ni hoi taabani, nchi haina mwelekeo tena haieleweki inataka nini kwa wakati gani.

Siisikii mipango ya muda mrefu juu ya kuwakwamua wananchi wake kutoka kwenye ufukara, badala yake yanagombaniwa madaraka kwa ajili ya kujineemesha wao wenyewe.

Kwa muda wote ambao tumekua huru tulipaswa walau tuwe tumejiweza walau hata kwenye elimu tu, napo imeshindikana.

Ni ajabu kwamba hata sector ambazo zinalipiwa na wananchi nazo bado zipo hoi, huduma kama za afya, maji safi umeme nakadhalika ilibidi ziwe za uhakika lakini napo hali inasikitisha.

Ukija usalama wa wananchi ni mdogo sana, tena sana tunaishi kwa hofu tukiwa hatuna tumaini lolote lile, hapa kikubwa unapumua na kua mkimya kwa kila jambo ndio angalau utasogeza siku za kula ugali.

Swali la msingi ni kwamba hapa tuna uhuru au tumebalishiwa mkoloni?? Na mkoloni wa sasa ni mweusi tena asiyekuwa na roho ya huruma.

Hii inaonyesha kabisa kwamba mtu mweusi ni mtu wa aina gani, tunaongozwa na watu wenye tamaa,chuki, ukatili na akili finyu.

Hawana mikakati ya kuletea watu maendeleo bali wao wenyewe na baadhi ya wanaowataka wao.

Itoshe kusema uongozi ni kipawa na mtu mweusi hana hicho kipawa.

kazi tunayo na tunapotaka kufika hatutafika kamwe.
 
Uzi kama huu unakosaje replies kabisa?!? Tumefundishwa mkoloni lazima awe na ngozi tofauti, ndiyo maana inakuwa ngumu watu kuamini kwamba wako utumwani.

Sio mbaya, ni jambo la muda,wataelewa
 
Back
Top Bottom