Hakuna anayeweka mapenzi mbele akaukubalu ukweli.....niliacha kushabikia mpira rasmi mwaka 2010; mwaka 2015 nikaanza kurudi pole pole, mpaka sasa bado sijafikia upenzi ule niliokuwa nao ila kwenye soka nimejifunza UNAFIKI uliotukuka kuliko SIASA.
Kama utaniuliza mimi, soka safi na bora kabisa kuchezwa kwenye uso wa dunia, mwisho ulikuwa 1998 kwenye fainali za kombe la Dunia nchini France.
Baada ya hapo, mpira tuushudiao ni kama kujaribu ku-programme ROBOTS to control traffic. Saying so, Messi is nothing but the results of programming the robots.
Kumbuka; Mc Fish, Thuram, Chilavert, Davor Suker, De Lima, Cafu, Claudio Taffarel, Zizou, Petit, Bellions, Romario, Mike Schumaichel, Campos, Okocha, BabaNgida, Baba Yaro, Oliseh, Batistusta, Oriel Ortega, Dunga, Van Bommel, Franco, van Bronchorst, n.k
Nilifurahia soccer back then......kabla siasa za soccer hazijapamba moto; kabla soccer haijatawaliwa na watu wawili tu na kusahau KEY PLAYERS.
Kumbuka robo fainali kati ya Barca na Man Utd, kumbuka robo fainali kati ya Arsenal na Barca, Mattheu Flamini na yule Mbrazil wa Arsenal(Gilberto), utajua soccer ni nini na nani ni nani!
Napenda ku-declare nimeanza kuwa mshabiki rasmi wa soccer la kimataifa fainali za Mataifa uhuru afrika mwaka ule wa Bafana Bafana anampiga Tunisia goli 3 fainali mwaka 1996 kama sikosei.