Teknolojia itabadilisha namna ya kujifunza, si kuondoa shule.
Darasa si sehemu ya kufundisha nadharia pekee, ni mazingira ya kujenga fikra pevu, nidhamu, ushirikiano, maadili na kufanya mazoezi ya vitendo chini ya uangalizi wa walimu.
Teknolojia na elimu mtandaoni vitapanua upatikanaji wa maarifa, lakini havitaondoa umuhimu wa taasisi za elimu. Ila vitazibadilisha tu.
Ndiyo maana vyuo vikuu bora duniani vinaendelea kuwekeza katika elimu ya ana kwa ana pamoja na teknolojia, badala ya kuiacha kabisa.