Miaka michache ijayo (kama 5 hadi 10) hakutakuwa na wakala wa M-Pesa tena

Miaka michache ijayo (kama 5 hadi 10) hakutakuwa na wakala wa M-Pesa tena

Wakuu dunia inaenda kasi ile mbaya mno, na teknolojia ya sasa inaenda kwa speed ya kutisha na watu hawalali wakiwaza jinsi ya kuleta mambo ya teknolojia.

Back to the Point, miaka kama 15 nyuma hakukuwa na hii kitu inaitwa M-Pesa na ukisoma taarifa za Safaricom ambao ndio wamiliki wa M-Pesa wanakuambia walipata shida mno siku za mwanzo kuendesha biashara ya M-Pesa.

Tanzania mtakumbuka wakati inaaza M-Pesa pia hakuna aliyekuwa anaimini na wengi waliona kama utapeli fulani au watapoteza pesa zao.

Leo hii M-Pesa inafanya transaction za trilion kwa siku tu. M-Pesa kwa sasa sio ishu tena.

Ishu ni nini?

Kwa sasa M-Pesa inahama kutoka mambo ya tuma pesa katoe kwa wakala na tumia na kwa sasa inaenda kwenye kutumia Mpesa kwa manunuzi.

Kwamba hutahitajika kutoa pesa kwa wakala ili ukanunue kitu, hutahitajika kwenda kutafuta wakala yuko wapi ili utoe pesa na uzitumie.

Rejeeni MPESA Mastercard.

Tunaelekea kwenye cashless kwa sasa mambo ya kutembea na waleti imetuna pesa yatapotea.

Dunia inaenda speed sana.

So hawa mawakala ni suala la muda tu kabla hawajawa outdated kabisa. Mambo yanaenda speed sana na ukizembea unaachwa nyuma.
Tz kubwa sana,hiyo estimate ya miaka mitano labda useme mijini,sio huku kwetu.OVER
 
Mpesa haimilikiwi na Safaricom. Mpesa ni mali ya Vodafone UK hadi Safaricom ambao wanamilikiwa na Vodafone UK kwa 35pc watakapolipa umiliki na kuhamisha servers kutoka UK kuja Nairobi
 
zingatia kwamba BOT tayari imeshaanza mchakato wa kuingiza mfumo wa cashless transactions uitwao TIPS (TANZANIA INSTANT PAYMENT SYSTEM), initial plan ni kwamba uanze fanya kazi july 2020.

Kwa namna ambavyo serikali ime rollout GePG system, naamini TIPS haitakawia.

yani hata ukienda nunua mkaa or nyanya gengeni ni TIPS ndio itahusika.

Huu uwakala umewapa malaki ya watanzania ajira ambazo coming july 2020 zinaanza pungua maana hakuna atayetaka atoe ela akatwe wakati kuna cashless transactions.

kama tunavyohimizwa sasa kutoa na kuomba risiti, basi tutahimizwa pia kulipa kwa TIPS. hapa ndio Tanzania itaenda kusanya kodi sahihi, pia uchumi wa kati utachochewa kwa kiwango cha juu.
Hii kitu nimeiona kwa I&M bank...Kuna kitu wanaita SPENN account! Lengo ni kuhamasisha cashless transactions inakuwa kama M Lipa, ni kama Mpesa tu ila yenyewe pesa unatolea Bank bure kabisa ila kupitia kwa wakala utakatwa 1% ya pesa unayotoa.
 
Technology unaondoka na ajira za watu... hilo lipo wazi
Ni kawaida tu hata kipindi simu hazijaenea na vocha kuuzwa bei ghali, kulikuwa na watu wengi wamejiajiri au kuajiriwa katika vibanda vya kupigia simu.
Na kabla ya simu janja kuenea kulikuwa na vibanda vya Internet, na wote hao walipoteza kazi zao muda ulipofika.
Sasa hivi imeanza kufanya kazi technology ya maroboti viwandani hali inayolelekea watu kupoteza ajira.
 
Itarahisha sana + usalama

Tigo tayari wana masterpass nadhani taratibu inaendelea kukua. Hii kulipia haina gharama unatuma free.
 
Sasa Kama hujaenda kwa wakala ili azibadilishe hizo hela zako katika mfumo wa kielectronic na kukuwekea kwenye simu yako hayo manunuzi utayafanya vipi? Au hayo malipo utayafanya vipi?
Mfumo wa upokeaji wa pesa utabadilika,yaani vyanzo vyako vya mapato vitapitisha pesa kwa njia ya cashless na utatoa kwa cashless hivyohivyo hata ukipiga/pigwa kizinga cha pesa upokeaji/ utoaji utakuwa kwa njia ya electronic,so hutakuwa na haja ya kuingiza pesa kwa wakala wakati utakuwa na float tyr
 
Back
Top Bottom