Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Maisha bila uzinzi yanawezekana, na nimetambua hilo baada ya kutimiza miaka miwili+ bila kuwa na uhusiano wala ukaribu wowote wa kimwili dhidi ya mwanamke/binti yeyote ndani ya muda huo.

Changamoto pekee nilivyo Kutana nayo ni kuonekana mwendawazimu hasa kwa majirani zangu wa karibu, watu ambao wanaamini ili mwanaume ukamilike ni lazima ubadilishe wanawake kila weekend.

Kwa mtazamo wao, kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kunaonekana kama jambo lisilo la kawaida, hali iliyofanya nionekane kama mtu asiyeeleweka au hata mwendawazimu machoni pao. Hii inaonyesha changamoto ya mitazamo ya kijamii ambayo mara nyingi huathiri watu wanaochagua maisha tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii.

Wito wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba wanapaswa kujua Uanaume wa kweli haupimwi kwa idadi ya wanawake bali kwa uwezo wa kujiheshimu, kudhibiti matamanio, na kufanya maamuzi yenye busara.

Kujitunza na kudhibiti hisia si udhaifu bali ni ishara ya ukomavu hasa kwa wale ambao bado hawajaingia katika ndoa.

Swali kwa vijana wenzangu, je mnaamini kuwa inawezekana kuishi bila kufanya uzinzi? Na kama ndiyo, ni muda upi mrefu zaidi umewahi kujizuia au kukaa bila kufanya vitendo hivyo?
 
Back
Top Bottom