Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Kuna tafiti inasema wanawake kufanya ngono mara kwa mara kunaathiri uwezo wao wa kudumu kwenye ndoa.

Hii sielewi imekaaje, ukizingatia kuna juhudi kibao za kutoa uhuru kwa jinsia zote, kwenye mambo yote.
Nakubaliana na huo utafiti, mwanamke akiwa mtu wa kufanywa mara kwa mara hasa kabla ya kuolewa anakuwa na nafasi kubwa sana ya kuiharibu ndoa yake, as wanaendeshwa na hisia kuliko uhalisia.
 
Hadi nakwosa la Kusema 🤔🤣kmmae wee utakua unakula mrenda wa mikono sana
 
Maisha bila uzinzi yanawezekana, na nimetambua hilo baada ya kutimiza miaka miwili+ bila kuwa na uhusiano wala ukaribu wowote wa kimwili dhidi ya mwanamke/binti yeyote ndani ya muda huo.

Changamoto pekee nilivyo Kutana nayo ni kuonekana mwendawazimu hasa kwa majirani zangu wa karibu, watu ambao wanaamini ili mwanaume ukamilike ni lazima ubadilishe wanawake kila weekend.

Kwa mtazamo wao, kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kunaonekana kama jambo lisilo la kawaida, hali iliyofanya nionekane kama mtu asiyeeleweka au hata mwendawazimu machoni pao. Hii inaonyesha changamoto ya mitazamo ya kijamii ambayo mara nyingi huathiri watu wanaochagua maisha tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii.

Wito wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba wanapaswa kujua Uanaume wa kweli haupimwi kwa idadi ya wanawake bali kwa uwezo wa kujiheshimu, kudhibiti matamanio, na kufanya maamuzi yenye busara.

Kujitunza na kudhibiti hisia si udhaifu bali ni ishara ya ukomavu hasa kwa wale ambao bado hawajaingia katika ndoa.

Swali kwa vijana wenzangu, je mnaamini kuwa inawezekana kuishi bila kufanya uzinzi? Na kama ndiyo, ni muda upi mrefu zaidi umewahi kujizuia au kukaa bila kufanya vitendo hivyo?
🤔🤔🤔 duh! Inafkirisha 2 years bila kubadilisha oil kwl, aiseee ebu nenda clinic tatzo unamatatzo ya afya ya akili lakn ujui wai mapema kwa ushaur
 
🤔🤔🤔 duh! Inafkirisha 2 years bila kubadilisha oil kwl, aiseee ebu nenda clinic tatzo unamatatzo ya afya ya akili lakn ujui wai mapema kwa ushaur
Huo ndyo mtazamo wa jamii zetu, kwamba usipo fanya ngono inaonekana una matatizo ya akili 😔😔
 
Kuna mtu hafanyi ngono ni kwa sababu hana wa kufanya nae na mwingine hafanyi kwa sababu za kiimani

Mtoa mada kwanini haujafanya for 2 years??
 
Back
Top Bottom