Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Maisha bila uzinzi yanawezekana, na nimetambua hilo baada ya kutimiza miaka miwili+ bila kuwa na uhusiano wala ukaribu wowote wa kimwili dhidi ya mwanamke/binti yeyote ndani ya muda huo.

Changamoto pekee nilivyo Kutana nayo ni kuonekana mwendawazimu hasa kwa majirani zangu wa karibu, watu ambao wanaamini ili mwanaume ukamilike ni lazima ubadilishe wanawake kila weekend.

Kwa mtazamo wao, kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kunaonekana kama jambo lisilo la kawaida, hali iliyofanya nionekane kama mtu asiyeeleweka au hata mwendawazimu machoni pao. Hii inaonyesha changamoto ya mitazamo ya kijamii ambayo mara nyingi huathiri watu wanaochagua maisha tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii.

Wito wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba wanapaswa kujua Uanaume wa kweli haupimwi kwa idadi ya wanawake bali kwa uwezo wa kujiheshimu, kudhibiti matamanio, na kufanya maamuzi yenye busara.

Kujitunza na kudhibiti hisia si udhaifu bali ni ishara ya ukomavu hasa kwa wale ambao bado hawajaingia katika ndoa.

Swali kwa vijana wenzangu, je mnaamini kuwa inawezekana kuishi bila kufanya uzinzi? Na kama ndiyo, ni muda upi mrefu zaidi umewahi kujizuia au kukaa bila kufanya vitendo hivyo?
Mimi nilishawahi kujipa challenge ya mwaka mmoja. Takribani miaka minne nyuma nilipitia hali ngumu sana ya maisha. Nilikaa chini nikajifanyia tathmini.

Moja ya maadhimio niliyojiwekea ni kukaa mbali na mahusiano, kwa sababu niliona mahusiano kwa mwanaume ni liability na yanapunguza focus, nikiangalia nyuma huwa nasema nilifanya maamuzi bora sana yaliyobadilisha maisha yangu

Ule mwaka ambao niliachana na masuala ya mahusiano nilijifunza mambo mengi sana. Niliona uhalisia jinsi mwanaume anatapeliwa na kurudishwa nyuma kimaisha na wanawake. Ukikaa nje ya uwanja unaona mchezo mzima unavyoenda.
 
Sidhani kama 'anajichukulia sheria mkononi' maana sababu zake ameandika.

Kupenda sana Ngono ni matokeo ya umaskini wa fikra ,umaskini wa maarifa, umaskini wa hekima ,umaskini wa busara , ulevi wa anasa na utajiri wa kifisadi au utajiri wa mgao katika mirathi.
Matokeo ya haya yote ni kupenda na kuwa mlevi wa starehe moja rahisi na isiyoshibisha nafsi ambayo ni ngono . Kila baada ya tendo la ngono nafsi hukuta na kukosa amani .

Ngono inaumiza sana nafsi na kudhoofisha roho ndio maana mwili unapenda ngono zaidi ili kuua nafsi na roho .

Mwili kazi yake ni kushindana na roho .
Binadamu alipoumbwa na Mungu alikua anaishi pepoponi kwenye roha ya nafsi ,roho na mwili usio na magonjwa wala kufa au kuzeeka haraka wala kuchakaa kwa sababu roho na nafsi vilifanikiwa kuudhibiti mwili kabla ya Shetani kumjaribu Adam na kuanguka kwenye dhambi ya kuufurahisha mwili .

Matokeo ya ulevi wa ngono ni kifo na majanga mengi ya kibinadam na ya asili ili kudhibiti ongezeko la watu maana ulevi wa ngono ndicho chanzo kikuu cha ongezeko la watu bila mpangilio maalumu duniani .

Peponi Adam hakuzaa watoto na waliishi uchi .
Kwa maana kuwa walikua wawili tu lakini hawakuwa na ashiki au tamaa ya kujamiiana na kuzalishana kwa wingi japo walikua na jukumu la kuleta uzao wa binadamu .
Sasa ni wazi kuwa palikua na utaratibu maalumu wa kuzaa walikua hawajapewa bado .
Dhambi iliwafikia baada ya kutii matamanio ya mwili na kudhoofisha mwili . Umri wao wa kuishi ukapunguzwa sana .

Adam na Hawa walikua na akili nyingi sana na uwezo mkubwa wa maarifa mengi kuliko binadamu wote lakini Mungu hakuwapa michepuko wala mahawara wala waume au wake wengi ili wakuze nafsi zao na roho zao kisha miili yao ipate nguvu za kuishi miaka mingi isiyo na magonjwa na majuto ya mara kwa mara .


Kifupi ngono sio mpango sahihi wa kimungu bali ni kipimo cha kumjaribu binadamu ili apate sifa za kurejea peponi kwa kuushinda mwili na kupandisha roho na nafsi katika daraja la juu.

Nabii Sulemani alianguka kwenye jaribio la ngono na matokeo yake akafa mapema kabla ya wakati wake na hekima na maarifa makubwa aliyopewa yakapotea . Suleiman alikua na nafasi ya kuishi zaidi ya miaka 1000 kama Adam kwa sababu alijua siri nyingi za maisha ya duniani na hata ya viumbe wengine na asili ya kila kitu na faida yake .

Shetani kwa chuki zake dhidi ya binadamu akamwangusha kwenye Tamaa ya wanawake na kujikuta muda mwingi anautumia katika kuufurahisha mwili na kudhoofisha roho na nafsi matokeo yake ,hekima maarifa na akili nyingi alizopewa zinaishia kwenye kunufaisha mwili pekee yake na baadae akaelekea kaburini
 
Mimi nilishawahi kujipa challenge ya mwaka mmoja. Takribani miaka minne nyuma nilipitia hali ngumu sana ya maisha. Nilikaa chini nikajifanyia tathmini.

Moja ya maadhimio niliyojiwekea ni kukaa mbali na mahusiano, kwa sababu niliona mahusiano kwa mwanaume ni liability na yanapunguza focus, nikiangalia nyuma huwa nasema nilifanya maamuzi bora sana yaliyobadilisha maisha yangu

Ule mwaka ambao niliachana na masuala ya mahusiano nilijifunza mambo mengi sana. Niliona uhalisia jinsi mwanaume anatapeliwa na kurudishwa nyuma kimaisha na wanawake. Ukikaa nje ya uwanja unaona mchezo mzima unavyoenda.
Sahihi kabisa mkuu, kuna hali ya tofauti mtu unakuwa nayo baada ya kuacha hayo mambo kwa muda, unajihisi tofauti na huru wakati wote.

Kama ulivyosema ukikaa kando unaona mchezo mzima hasa utapeli unaofanywa kwenye mahusiano, sometimes unajihisi mwenye bahati kuepukana na utapeli huo kwa muda.
 
Baada ya kujitunza hivyo una mipango gani? Isijekuwa ndio wale wanaume wapumbavu wanaojitunza ili kumfuraisha mke ajae? Au basi kiafya ni jambo zuri pia isijekua hufanyi zinaa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako labda wewe ni domo zege, au hauna hela za kuhudumia, au hujiamini au unakataliwa kila ukitongoza hivyo umeamua kujificha katika kivuli cha kujifariji kuwa unajitunza na motivation nyingi za kujitetea na kukupublish kama mtu mwema, kumbe ni simba aliyekosa mawindo.

Mimi naamini mwanaume aliyeamua kuachana na hayo mambo suala la kwanza awe ametimiza vigezo vyote vya kumaster ushawishi wa kuwapata wanawake ambavyo nimetaja hapo kama vile kujiamini, uwezo wa kipesa hata kidogo wa kumpata mwanamke angalau hata wa level za chini, pia uwe na sifa ya kutokataliwa hapo ndipo ukitulia tutasema wewe umetulia kwa sababu zako binafsi na si External factors kama kukosa mvuto wa ushawishi kwa wanawake.

Kama kweli una vigezo vya kufanya uamuzi huo basi ni jambo jema, lkn kama ni uamuzi unaufanya baada ya kukosa mawindo basi wewe ni mpuuzi mmoja afadhari hata hawa wanaume malaya+walevi wasioficha tabia.

Naishia hapo.
 
Bora walikuona mwendawazimu kuliko kukupa cheo cha bwabwa, shoga, chakula nk
 
Bora walikuona mwendawazimu kuliko kukupa cheo cha bwabwa, shoga, chakula nk
Vyovyote watakavyo niita au kufikiri, hizo ni fikra zao ndani ya vichwa vyao na mimi hazinihusu.
 
"Machoni mwa watu." "Machoni mwa watu." Duniani umekuja nani? Na unaishi maisha yako kwa ajili ya nani? Kama unajali kuhusu "kuonekana kichaa sababu huvushi bitches" basi unaishi sehemu usiyotakiwa au you're the wrong person.
 
"kuonekana kichaa sababu huvushi bitches" basi unaishi sehemu usiyotakiwa au you're the wrong person.
Sio sehemu ninayo ishi bali ni jamii ya watanzania kwa ujumla wanaamini uzinzi ndyo ujanja.

I'm the right person on my own mind, and that's enough.
 
Back
Top Bottom