Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Maisha bila uzinzi yanawezekana, na nimetambua hilo baada ya kutimiza miaka miwili+ bila kuwa na uhusiano wala ukaribu wowote wa kimwili dhidi ya mwanamke/binti yeyote ndani ya muda huo.

Changamoto pekee nilivyo Kutana nayo ni kuonekana mwendawazimu hasa kwa majirani zangu wa karibu, watu ambao wanaamini ili mwanaume ukamilike ni lazima ubadilishe wanawake kila weekend.

Kwa mtazamo wao, kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kunaonekana kama jambo lisilo la kawaida, hali iliyofanya nionekane kama mtu asiyeeleweka au hata mwendawazimu machoni pao. Hii inaonyesha changamoto ya mitazamo ya kijamii ambayo mara nyingi huathiri watu wanaochagua maisha tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii.

Wito wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba wanapaswa kujua Uanaume wa kweli haupimwi kwa idadi ya wanawake bali kwa uwezo wa kujiheshimu, kudhibiti matamanio, na kufanya maamuzi yenye busara.

Kujitunza na kudhibiti hisia si udhaifu bali ni ishara ya ukomavu hasa kwa wale ambao bado hawajaingia katika ndoa.

Swali kwa vijana wenzangu, je mnaamini kuwa inawezekana kuishi bila kufanya uzinzi? Na kama ndiyo, ni muda upi mrefu zaidi umewahi kujizuia au kukaa bila kufanya vitendo hivyo?
Hongera sana. Pokea maua yako. Mwanamme akiweza kutawala hisia zake, ametatua 90% ya matatizo yake
 
Nimewahi experience hii kitu sio unaonekana kama chizi

Kiukweli unaanza kuwa kama chizi kiasi fulani
Maana kuna muda kama nilikuwa over thinker

Jambo dogo naanza kulichimba kwa ndani sana na pengine halina maana sana hii yote sababu

Nakuwa sina mawazo ya ngono pia nahisi mawazo ya ngono ukiendekeza uchukua nafasi kubwa sana kichwani
 
Upewe soda
 
Ni heri kuwaza mambo mengine kwa kina kuliko kuwaza ngono, na ni kweli kwamba ukikosa sex kwa muda mrefu mawazo yanabadilika, lakini afadhali hivyo kuliko kuwa na mawazo ambayo mwisho wake sio mzuri.
 
Nimewahi experience hii kitu sio unaonekana kama chizi

Kiukweli unaanza kuwa kama chizi kiasi fulani
Maana kuna muda kama nilikuwa over thinker

Jambo dogo naanza kulichimba kwa ndani sana na pengine halina maana sana hii yote sababu

Nakuwa sina mawazo ya ngono pia nahisi mawazo ya ngono ukiendekeza uchukua nafasi kubwa sana kichwani
Mkuu sio kweli saa nyingine vishawishi vya sehemu husika vinachangia kukuchea kuwa na mawazo fulani.
Sisi kipindi tumemaliza masomo ramani hazisomi mm na msela wangu tulienda kijiji kimoja huko kaliuwa ndani kabisa karibu na malizevu huko mkoani Tabora kwenda kufanya shughuli za kilimo.
Tulikaa miezi minane bila kuiona papuchi na nilikuwa normal tu, yaani kuna kipindi kilifika mpaka huku chini mjomba hakawa hasimami asubuhi kama ilivyo kawaida yake mpaka nikaanza kupata mashaka.
Alafu mwanaume ukiendekeza uzinzi kama bado unajitafuta basi umejichimbia kabuli la mafanikio yako.
Mwana mke akiwa na akili uzinzi unaweza kumfaidisha akapata maisha.
 
Uliza mkuu, tupo hapa kujadili pamoja
Sawa sawa Mkuu!

Mosi, Nataka kujua ni sababu gani kubwa, ilikupa msukumo wa kuyaenda hayo (Je ni sababu ya kiroho au )

Pili, Ni njia gani ulizitumia katika kufanikisha jambo Hilo? Nina amini Pengine, ulikutana na majaribu au changamoto!

Tuanzie hapo!
 
Sawa sawa Mkuu!

Mosi, Nataka kujua ni sababu gani kubwa, ilikupa msukumo wa kuyaenda hayo (Je ni sababu ya kiroho au )
Baada ya kupata mtoto akili yangu ilibadilika kabisa, nikawa sina mzuka tena na wanawake muda wote naumiza kichwa ni jinsi gani mtoto wangu ataishi.

Kila nikifikiri kuhusu mapenzi najiuliza kama ni pesa si afadhali nitumie kumhudumia mwanangu kuliko wanawake, nafsi ikawa inanisuta.

Sababu nyingine ni ya kiroho, na hiyo ni baada ya kujifunza kwamba zinaa inaharibu na kuondosha baraka za Mungu katika maisha ya mwanadamu.

Pili, Ni njia gani ulizitumia katika kufanikisha jambo Hilo? Nina amini Pengine, ulikutana na majaribu au changamoto!
Hakuna njia yoyote zaidi ya ku ignore vishawishi hasa kukwepa uwezekano wa kuanzisha mahusiano na wanawake, japo ilikuwa ngumu maana sometimes wadada wanataka wenyewe ila nikaamua kupiga chini na kuziba masikio.
 
Mkuu sio kweli saa nyingine vishawishi vya sehemu husika vinachangia kukuchea kuwa na mawazo fulani.
Sisi kipindi tumemaliza masomo ramani hazisomi mm na msela wangu tulienda kijiji kimoja huko kaliuwa ndani kabisa karibu na malizevu huko mkoani Tabora kwenda kufanya shughuli za kilimo.
Tulikaa miezi minane bila kuiona papuchi na nilikuwa normal tu, yaani kuna kipindi kilifika mpaka huku chini mjomba hakawa hasimami asubuhi kama ilivyo kawaida yake mpaka nikaanza kupata mashaka.
Alafu mwanaume ukiendekeza uzinzi kama bado unajitafuta basi umejichimbia kabuli la mafanikio yako.
Mwana mke akiwa na akili uzinzi unaweza kumfaidisha akapata maisha.
Mimi basi ilikuwa hivyo

Kwa upande wako ilikuaa hivyo
Tunashare experience tu hapa
 
Kijana ukiweza kuku_control nyege umetoboa kimaisha (utajiri)
Screenshot_20250312-215047.png
 
Back
Top Bottom