Miaka miwili bila uhusiano/ uzinzi iliyopelekea nionekane mwendawazimu machoni mwa watu

Hii inaonyesha changamoto ya mitazamo ya kijamii ambayo mara nyingi huathiri watu wanaochagua maisha tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii.
Kabisa.

Hili suala nimekuja kulielewa hivi karibuni. Vijana wanapata shinikizo kali la kufanya ngono ili waweze kuendana na makundi(fitting in), wakati huo ulazima haujabebwa na sababu zozote za msingi.
 
Umeolewa? Kama bado basi nakupa pole kwani unavyozidi kufanya uzinzi ndivyo unapunguza nuru na heshima yako kwa mume wako mtarajiwa.
Kuna tafiti inasema wanawake kufanya ngono mara kwa mara kunaathiri uwezo wao wa kudumu kwenye ndoa.

Hii sielewi imekaaje, ukizingatia kuna juhudi kibao za kutoa uhuru kwa jinsia zote, kwenye mambo yote.
 
Kabisa.

Hili suala nimekuja kulielewa hivi karibuni. Vijana wanapata shinikizo kali la kufanya ngono ili waweze kuendana na makundi(fitting in), wakati huo ulazima haujabebwa na sababu zozote za msingi.
Wanapata shinikizo na mwisho wakipata majanga kama magonjwa wanaishia kuchekwa na kuonekana wamepotea.
 
Hii mada kiujumla ni ngumu.

Kama watu hawapaswi kushinikizwa kufanya ngono, je, ni katika vigezo gani wanashauriwa kufanya?(Ijadiliwe mitazamo ya kidini na ya kidunia)
Wanashauriwa kuto kufanya ngono na kutunza miili na afya zao, pia kutokufanya hivyo husaidia kuimarisha nafsi na kutengeneza uhusiano mzuri na Mungu.
 
Oa mjomba unawawazisha majirani, wakianza kusema kijana jogoo hapandi mtungi utawalaumu?
fanya vitendo hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…