benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Katika miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Halmashauri nchini zimevuka malengo ya makusanyo ya mapato yaliyowekwa.
Mwaka 2021/22 halmashauri zilikusanya mapato ya ndani ya Sh bilioni 888.7 kati ya Sh bilioni 863.86 zilizoidhinishwa ambayo ni sawa na asilimia 103 ya bajeti ya mwaka ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 131.7 sawa na asilimia 17 ya mapato halisi ya Sh bilioni 757.1 yaliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21.
Katika mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya Sh trilioni 1.012 ambapo katika ya Julai hadi Desemba 2022 zimekusanya Sh bilioni 485.42 sawa na asilimia 48 ya bajeti ya mapato ya ndani iliyoidhinishwa.
Kwa mwaka 2023/24, halmashauri nchini zinakisia kukusanya mapato ya ndani ya Sh trilioni 1.30 sawa na ongezeko la Sh bilioni 288.
Kwa mwendo huu wa makusanyo ni wazi kuwa tupo katika njia sahihi ya kuweza kuendesha na kusimamia miradi yetu kwa fedha za ndani.