Miaka miwili ya Rais Samia: Halmashauri zavuka malengo ukusanyaji mapato

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Katika miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Halmashauri nchini zimevuka malengo ya makusanyo ya mapato yaliyowekwa.

Mwaka 2021/22 halmashauri zilikusanya mapato ya ndani ya Sh bilioni 888.7 kati ya Sh bilioni 863.86 zilizoidhinishwa ambayo ni sawa na asilimia 103 ya bajeti ya mwaka ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 131.7 sawa na asilimia 17 ya mapato halisi ya Sh bilioni 757.1 yaliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21.

Katika mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ziliidhinishiwa kukusanya Sh trilioni 1.012 ambapo katika ya Julai hadi Desemba 2022 zimekusanya Sh bilioni 485.42 sawa na asilimia 48 ya bajeti ya mapato ya ndani iliyoidhinishwa.

Kwa mwaka 2023/24, halmashauri nchini zinakisia kukusanya mapato ya ndani ya Sh trilioni 1.30 sawa na ongezeko la Sh bilioni 288.

Kwa mwendo huu wa makusanyo ni wazi kuwa tupo katika njia sahihi ya kuweza kuendesha na kusimamia miradi yetu kwa fedha za ndani.
 
Toka Bashungwa aondolewe huko ni kivuruge tuu Wala hakuna Tija yeyote Waziri wenu wa Sasa kaleta.

Kwanza amevuruga ule utaratibu wa kushindanisha Halmashauri Kwa kutoa taarifa Kila robo mwaka Ili kujua Mwenendo wa Halmashauri na pia kuwa summon wale wanaozembea.

Matokeo yake ni kushuka Kwa Makusanyo..

Mfano nusu Mwaka zimekusanywa Bil.485 Bado Bil.815 Kwa mujibu wa Makisio.

Sasa kama miezi 6 hujafikia nusu ya Makusanyo hiyo kuvuka lengo itatoka wapi?

Toeni huyo Waziri wenu wa Tamisemi
 
Sio kwamba zimevuka malengo bali bajeti walizojiwekea wameweka madrio ya chini(underestimate).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…