Tangu aapishwe Machi 19, 2021 Rais Samia Suluhu amekuwa akifanya jitihada za kuanzisha na kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi.
Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP), Reli ya kisasa (SGR), barabara kubwa na ndogo, miradi ya umeme mjini na vijijini, ahli ambayo imekuwa tija kubwa ya ukuaji wa uchumi nchini.
Hali hiyo imewaibua wananchi na viongozi mbalimbali ambao wameeleza mafanikio yaliyofikiwa, huku wakimpongeza kiongozi huyu kudumisha amani, mshikamano na utulivu wa kisiasa nchini.