Miaka miwili ya Wallace Karia madarakani

Smith Rowe

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
4,319
Reaction score
9,003
Miaka miwili imetimia tangu ndugu Karia aingie madarakani lakini hakuna ishu ya msingi aliyoifanya anazurura zurura tuu na wakina Makonda.
 
Hivi wagombea wenzake kwenye nafasi ya urais walikuwa wakina nani?
 
Hii taasisi ni kuiingilia kimafia kama Roman Abramovich
 
Bora hata malinzi alijenga viwanja vya mpira mfano nyamagana,kaitaba na Uhuru
 
Asprin huyo jamaa naona anaangalia maslahi yao tuu sio kwa vilabu sijaona akijishughulisha kupata wadhamini wa ligi hata kwa vilabu vidogo kama watangulizi wake walivyofanya...
 
Mazuri yake kiaina;

Ameiwezesha Taifa Stars kufuzu Afcon baada ya miaka 39, ameongeza timu za ligi kuu kutoka 16 mpaka 20, ameimarisha soka la wanawake na mfano mzuri ni hao Tanzanite, Ameanzisha ligi ya wanawake, ameboresha/kuanzisha mashindano ya vijana ya umri tofauti tofauti kwa lengo la kuvumbua vipaji, nk.

Madudu yake sasa;

Ligi kukosa mdhamini kwa mara ya kwanza tangu enzi za FAT, Kujipendekeza kwa watawala na kushindwa kuficha mahaba yake kwa ccm, ligi kuwa na waamuzi wengi walio lalamikiwa kwa kuboronga kuliko awamu nyingine, kuteua baadhi ya watendaji kwa kujuana au kwa kubebana kama ilivyokua kwa mtangulizi wake Malinzi; mfano uteuzi wa Amunike, Oscar Mirambo na Amy Ninje, kupenda kuzurura huku kukiwa hakuna mpango wowote wa kujenga viwanja vipya mfano kwenye eneo lao la Tanga, kujenga vitega uchumi vya TFF mfano ofisi nzuri za kisasa, hotel, hostel, nk.

Hitimisho: Ikiwezekana uchaguzi ujao, wachaguliwe watu wenye uchungu na mpira wa Tanzania na siyo hao makada na wanachama wa ccm ambao mwisho wa siku wanaifanya timu ya Taifa kama vile ni timu ya ccm.
 
Asprin huyo jamaa naona anaangalia maslahi yao tuu sio kwa vilabu sijaona akijishughulisha kupata wadhamini wa ligi hata kwa vilabu vidogo kama watangulizi wake walivyofanya...
Naweza kukubaliana na wewe ukiniambia ni uongozi upi uliofanya vizuri... na kwa kigezo gani? Kama ligi kupata wadhamini ndio kigezo chako basi bado siko upande wako
 
Yaan tangu kaondoka Mzee Ndolanga aliekuwa hana sapoti yeyote ya Serikals sijaona lolote la maana la Tenga, Malinzi wala huyu Wallace pamoja na sapoti yote ya Serikal
 
Yaan tangu kaondoka Mzee Ndolanga aliekuwa hana sapoti yeyote ya Serikals sijaona lolote la maana la Tenga, Malinzi wala huyu Wallace pamoja na sapoti yote ya Serikal

 
Hivi Mikael Wambura bado tu wamemng'ang'ani jela.

Kesi yake wala siisikii tena, imeishia wapi!

Topic hii imenikumbusha mambo mengi ya hovyo kwenye tasnia ya soka Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…