Misosi vipi? Unakulaje na huwa unakula wapi?
Kuna rafiki yangu yeye ana kipato cha kawaida tu, maingizo yake hayazidi 500k ila mchana tu akiwa job anakula buku 5.
Sio kubwa ila kwa kipato chake ni kubwa maana tareh kama hizi anabaki apeche anaishia kukopakopa na hiyo ni karibu kila mwezi.
Kuna vitu labda unafanya wewe unaona ni vya kawaida ila vinakunyonya pesa.
Kuna wengine wanapenda ndani kwake kupendeze, unakuta ana makitu ya bei mbaya humo ndani kwake, mpaka mwaka unaisha kaishia kununua vitu vya ndani tu hamna cha maana alichowekeza.
Tatizo ni wewe wala hujarogwa, angalia matumizi yako na uone pesa yako unaimalizia wapi. Hamna anaekuroga mkuu.
Kumbuka pesa yako ya mwisho uliitumia vipi, usidharau hata hizo jero za bajaji na daladala nazo zijumuishe kwenye hesabu.
NB. Ubahili bila malengo ni utumwa wa kujitakia.