Miaka nenda rudi sina hata pikipiki na pesa huwa napata nyingi tu. Huwa najiuliza nini kinatokea. Yawezekana napigwa kipapai?

Tatizo ni aina ya mwanamke upo naye,only that.pia nenda kanisani toa 10%utaanza kufanya mambo makubwa,Nina mshahara mdogo zaid yako lakini Nina mambo makubwa
 
Misosi vipi? Unakulaje na huwa unakula wapi?

Kuna rafiki yangu yeye ana kipato cha kawaida tu, maingizo yake hayazidi 500k ila mchana tu akiwa job anakula buku 5.
Sio kubwa ila kwa kipato chake ni kubwa maana tareh kama hizi anabaki apeche anaishia kukopakopa na hiyo ni karibu kila mwezi.

Kuna vitu labda unafanya wewe unaona ni vya kawaida ila vinakunyonya pesa.
Kuna wengine wanapenda ndani kwake kupendeze, unakuta ana makitu ya bei mbaya humo ndani kwake, mpaka mwaka unaisha kaishia kununua vitu vya ndani tu hamna cha maana alichowekeza.

Tatizo ni wewe wala hujarogwa, angalia matumizi yako na uone pesa yako unaimalizia wapi. Hamna anaekuroga mkuu.

Kumbuka pesa yako ya mwisho uliitumia vipi, usidharau hata hizo jero za bajaji na daladala nazo zijumuishe kwenye hesabu.

NB. Ubahili bila malengo ni utumwa wa kujitakia.
 
nishawai fanya ivo pia
kaka uko wapi?
Tafuta:

chumvi ya mawe
Majani ya Mbaazi
Kivumbasi/malumbalumba
Muosha Fedha
Mvunja homa
Majani ya mashona nguo
Majani ya Mkunde Pori

Ukipata hizi raw material hapo juu unaweza kuanza kujipambania mwenyewe

CHEMSHA HIVI VITU MAJI YAIVE SANA KISHA JIFUKIZE HUKU UKIWA UCHI KAMA DAKIKA 15. NUIZA KILA AINA YA NENO UNALOTAKA


Hizo ni dawa mwana ukome kwa uchawi, mikosi, nuksi, vijicho yani hatari sana hata Mshana Jr anaelewa sana
 
Sijasikia wala kuona sehemu ukikumbuka baba wala mama yako kwa chochote ....

Anzia hapa Kisha akili yako itafakari maisha ulio tokea (tembelea nyumbani) kuna namna fulani ivi akili hufunguka
 
Me mwenyewe age 28 sasa hakuna hustle miaka 8 yote, hakuna nilichofanya zaidi ya kununua kiwanja tu, nimeamua kutulia sifanyi tena kazi nataka kujua alichinipangia Mungu ni kipi
 
Muombe Mungu kwa moyo thabit......pia unuie akupe riziki zako. Kumbuka kutoa sadaka. Saidia masikini mambo hayo hulinda mali zako ikiwemo fedha isipotee. Utanishukuru badae
 
Mifuko Yako imetobolewa sababu "Hulipi ZAKA ", Fungu la kumi.

Lipa ZAKA utarudi Kutoa ushuhuda.

Hakuna mchawi,jini,shetani au CHUMA ulete awezaye kuiba pesa ya mtu alipaye ZAKA.

Ubarikiwe.
 
Katika kiasi unachopata Unakumbuka kutoa Sehemu ya 10 kama zaka kwa Mungu wako?Uchawi ndio hapo rafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…