mountain climber
JF-Expert Member
- Aug 31, 2024
- 311
- 461
Niende moja kwa moja kwenye jambo ambalo limekuwa changamoto na kero kwa Watanzania walio wengi. Kero yangu naipeleka kwa mamlaka inayohusika na kutoa vitambulisho vya taifa (NIDA). Kuna baadhi ya watu wamekosea taarifa kama vile alama za vidole kuingiliana, na mwishowe wamekosa namba. Mtu amekaa zaidi ya miaka saba akifuatilia namba bila mafanikio.
Wengi walio na changamoto hii ni wale operators wa biometrics, ambao hawakuwa na weledi wa kutosha kuhusu mashine hizo. Walikuwa wakiwawekea baadhi ya watu alama za vidole bila kujua madhara yake mbeleni.
Ombi langu kwa mamlaka hii ni kufanya namna, kama inawezekana, kuwafutia taarifa hizo ili waweze kujisajili upya. Hili linawezekana kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Watu wengi wamekosa fursa kama ajira, huduma za afya, pamoja na passport kwa sababu ya kukosa kitambulisho cha NIDA.
Kila siku wanasema wanakuja na muongozo mpya, lakini hakuna suluhu yoyote. Ningeomba kwa dhati kabisa mkurugenzi mpya aliyeteuliwa aweze kulifanyia kazi hili, kwani ni watu wengi wanahangaika nalo bila mafanikio.
Mniwie radhi kwa mwandiko wangu usioridhisha, lakini kwa namna fulani nitakuwa nimeeleweka. Ningeomba mods kuupost ili mamlaka husika iweze kulifanyia kazi.